Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1541 to 1550 of 1581.

  • 7 Jun 2018 in Senate: Bi. Spika wa muda, “Spika” ni neno la Kiswahili na akipenda, naweza kumpa kamusi sasa hivi ili ahakikishe kwamba hilo ni neno la Kiswahili. Kwa hivyo, kama hajui, aelezwe. view
  • 7 Jun 2018 in Senate: Kuna mmomonyoko wa maadili--- view
  • 7 Jun 2018 in Senate: Asante, Sen. Wario. Nilikuwa nimesema “Bi. Spika.” Inaonekana kwamba katika Jamhuri yetu ya Kenya, kuna mmomonyoko wa maadili. Ndipo unapata kwamba watu wako na nguvu za kwenda mpaka kuvamia shule na kuwanajisi wanafunzi wa kike katika bweni lao wakati wamelala. Hivi majuzi pia tumeona katika vyombo vya habari watoto wadogo wadogo wananajisiana na kulawitiana wenyewe kwa wenyewe. Hilo linamaanisha kwamba kuna mmomonyoko wa maadili. Wizara Ya Elimu inapaswa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya mkasa wa Solai ambayo imeletwa na Seneta wa Kaunti ya Nakuru; Sen. Kihika. Kwanza, ningechukua fursa hii kutuma rambirambi zangu kwa mara nyingine tena kwa watu wa Nakuru kwa janga hilo lililowapata. Ninawaombea Mungu wale ambao Mwenyezi Mungu aliwachukua na aweke roho zao mahali pema peponi. Vile vile, ningependa pia kuchukua fursa hii kutuma rambirambi zangu kwa watu wa Kaunti ya Tana River ambao wamepata mkasa wa mafuriko na pia sehemu zingine zote za nchi ya Kenya ambazo kuna janga la mafuriko kwa sasa. Kwa hakika, majanga kama haya ... view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Ndio, ni mfereji. Asante Bw. Naibu Spika. Mifereji ya mafuta ilipopasuka, mpaka leo wale ambao waliathirika bado hawajalipwa ridhaa. Kwa hivyo, imekuwa ni mwelekeo kwamba janga linatokea, watu wanaomboleza siku mbili, wanatoa hotuba kali kali, lakini baada ya hapo, inakuwa ni jambo la kawaida. Kwa upande mwingine, tunaona kwamba janga la ufisadi ni kubwa zaidi. Hii ni kwa sababu zile pesa ambazo zingekwenda kwa matibabu ya watu wote ambao hawajiwezi na kusaidia wazee wale wanaolipwa ruzuku na Serikali, zote zinafujwa kwa sababu ya ufisadi. Bw. Naibu Spika, kwa hivyo, tungeomba kwamba Serikali ichukulie majanga kama haya hatua kali zaidi kuliko ... view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Seneta ‘spesheli’ Sakaja. view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, naondoa neno ‘Super Senator’. Nasema Sen. Sakaja ambaye ni Seneta wa Kaunti ya Nairobi. Ni Seneta wa jiji kuu kama vile mimi, Seneta wa Kaunti ya Mombasa na Seneta wa Kaunti ya Kisumu. view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, nakubaliana nawe na ninaondoa hiyo. Sina haja ya kuomba msamaha kwa sababu ni jambo ambalo ni zuri kwake. view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika. Kwa hivyo, ninasema kwamba maswala yale ambayo yanawakumba ndungu zetu wanaoishi katika vitongoji duni ni maswala ambayo lazima tuyaangalie na tuhakikishe Sheria imetumika sawa sawa katika sehemu zote za Jamhuri ya Kenya. Tumeona kwamba maswala ya ubakaji katika maeneo yale ni maswala ya kawaida. Mimba zisizopangwa na uwaviaji mimba kiholela ni mambo ambayo yanatokea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 5 Jun 2018 in Senate: Bw. Naibu Spika, ndugu yetu Seneta wa Laikipia angetumia msemo “usipoziba ufa, utajenga ukuta.” Huo ndio ungekuwa msemo mwafaka kwa kumalizia hotuba yake. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus