19 Feb 2020 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Ninampongeza Sen. Iman kwa kuleta maombi haya kwa Bunge la Seneti. Hili ni swala nzito sana kwa watu wa North Eastern kwa sababu swala la Al Shabaab ni la kitaifa. Si la jamii moja ama eneo moja. Uamuzi wa kwenda Somalia kupigana na Al Shabaab haukufanywa na watu wa North Eastern. Ulifanywa na Serikali ambayo iko Nairobi. Leo Serikali ile imeamua kuondoa walimu kutoka eneo lile ili wanafunzi wasiweze kusomeshwa. Je, ipo haja ya hili swala la uajiri wa waalimu lipelekwe Mashinani ili kila kaunti iwe na tume yake ya kuajiri walimu; ...
view
19 Feb 2020 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Feb 2020 in Senate:
Bw. Naibu Spika, wanafunzi katika maeneo yale watafanya mitihani sawa na wengine katika nchi ya Kenya lakini wanaweza kuwa hawasomeshwi kwa muda wa mwezi mmoja kwa sababu walimu wote wamehamishwa. Pia, kuna swala la mitihani ambayo inakuwa centralized na kuchapishwa na Kenya National Examinations Council (KNEC) lakini ukiangalia, maeneo mengi hayana huduma kama zile zinazopatikana katika miji mikubwa. Ipo haja ya kuangalia swala hili kwa undani Zaidi na ipendekezwe kwamba swala la mitihani na lile la uajiri wa walimu lipelekwe katika kaunti ili kila kaunti iwe na sehemu yake ya kuajiri walimu wanaotaka.
view
19 Feb 2020 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nilikuwa na hoja ya nidhamu kwa ndugu yangu, Sen. Madzayo.
view
19 Feb 2020 in Senate:
Bw. Naibu Spika, Sen. Madzayo anapozungumzia umri fulani, je ni wazee wavivu au ni kukosa chakula cha samaki?
view
19 Feb 2020 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia pendekezo la mabadilisho ya sheria ya uvuvi, usimamizi wa uvuvi na utekelezaji wake. Mswada huu umekuja katika wakati mwafaka. Tumeona uchumi wa Kenya umekuwa ukiregerega kwa sababu ya zile nyanja tofauti ambazo zinasimamia uchumi wa Kenya zimelemaa katika utendakazi wake. Uvuvi unaweza kutupa fursa nzuri ya kuongeza mapato ya nchi, hususan samaki wale wakitayarishwa na kusafirishwa katika nchi zingine ile wauzwe katika soko za nje. Vile vile, uvuvi unatoa fursa kwa Wakenya kupata chakula ambacho hakina madhara, isipokuwa sehemu za uvuvi ambako maji yameingiliwa na mchafuko kutokana na ‘ contamination ’ ...
view
19 Feb 2020 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Feb 2020 in Senate:
Bw. Naibu Spika, naunga mkono mapendekezo ambayo yametolewa na Sen. Kajwang’, isipokuwa moja inayopendekeza mkurugenzi mkuu kukaa ofisini kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu. Wakurugenzi wengi hukaa ofisini kwa muda wa miaka matatu, na huo umekubalika kama wakati mzuri wa kufanya kazi na kuendelea na mambo mengine. Wavuvi wetu wengi hawana uwezo wa kununua vifaa vya kuwaezesha kuvua samaki katika sehemu za bahari kuu, ambako kuna samaki wengi kuliko mikono ya bahari kama Tudor, Port Reitz na kwingineko. Kwa hivyo, ipo haja ya serikali za kaunti kutoa ruzuku kwa hao wavuvi, ili kuhakikisha kwamba wavuvi wanapata vifaa vya kisasa ...
view
19 Feb 2020 in Senate:
Bila shaka, Bw. Naibu Spika.
view
19 Feb 2020 in Senate:
Bw. Naibu Spika, naweza kunena bila hofu au kutatizika kwamba ukila papa m’bichi, una hakika kwamba utajenga nguvu za kutosha mwilini za kupambana na athari yoyote ya kiafya.
view