13 Nov 2019 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
13 Nov 2019 in Senate:
nyingi, kiasi ambacho Wakenya hawawezi kupeleka kesi zao mahakamani ili zitatuliwe. Kwa hivyo, upatanishi na usuluhishi utasaidia pakubwa kupunguza gharama ya kupata haki katika jamii yetu. Kfungu cha nne, yaani Part 4, kinatoa fursa kwa wale ambao labda hawakuweza kuelewana, kwenda mahakamani kutatuliwa tatizo lao, baada ya kushindwa kutatua tatizo hilo kupitia kwa upatanisho na usuluhishi. Hii sheria inaleta mwongozo, kwamba kabla ya kwenda mahakamani, watu waweze kupewa fursa ili wakae chini, wajaribu kutatua mzozo ule bila ya kwenda kwa mahakama, kama nafasi ya kwanza ya kujaribu kutatua tatizo hilo. Sheria hii inatoa nafasi ya kukaa chini kabla ya kwenda ...
view
13 Nov 2019 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
13 Nov 2019 in Senate:
Ningependa kuunga mkono Mswada huu wa Sen. Kasanga. Nawasihi Maseneta wenzangu wausome kwa kina, na waunge mkono swala kama hili. Asante, Bw. Naibu Spika.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninaomba msamaha kwa kuchelewa kufika Bungeni kwa wakati uliyotengwa. Hii ni kwa sababu tulipata shida ya usafiri kutoka kiwanja cha ndege hadi hapa jijini kwa sababu ya msongamano wa magari. Tunaomba ile Express Highway itengenezwe haraka kwa sababu tunapoteza wakati mwingi barabarani. Hata hivyo, ninaomba kuuliza taarifa yangu.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeombwa Bungeni na Seneta wa Wajir, Sen. (Dr.) Abdullahi. Kwa hakika---
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ya Senator wa Wajir, Sen. (Dr.) Abdullahi. Kwanza, ninampongeza kwa kuleta Taarifa hii Bungeni. Madeni yamekua ni donda sugu katika kaunti zetu. Hii ni kwa sababu kila kaunti ina madeni ya mamilioni ya pesa. Singependa kukosoa maelezo yaliyotolewa na Sen. Cherargei, kwamba, madeni yamebaki Kshs33 bilioni, lakini kusema ukweli, ripoti ya madeni yote ambayo yako katika kaunti iko mbele ya Kamati ya Uhasibu. Kamati hiyo imekua ikiwahoji magavana tofauti tofauti ili kuthibitisha ni pesa ngapi ambazo wanadaiwa na wananchi ambao ni wanakandarasi katika kaunti hizo. Sio kwamba hakuna sheria; sheria iko ...
view
12 Nov 2019 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Mabibi wamekimbia kutoka kwa nyumba nyingi kwa sababu ya madeni ambayo yamekumba familia ambazo zimepatiwa kandarasi na kaunti. Ukiangalia gazeti siku ya Jumatatu na Jumanne, utapata kwamba kurasa zaidi ya kumi zimeandikwa orodha ya watu ambao wanadaiwa na benki, ambao nyumba zao na mali yao zinauzwa kwa sababu ya kushindwa kulipa madeni kutokana na kazi ambazo wamefanyia kaunti. Swala hili pia haliathiri serikali za kaunti pekee; ulipaji wa madeni umekuwa shida hata kwa Serikali kuu. Kwa hivyo, ningeomba kwamba Kamati husika, itakapoangalia swala hili, itoe mapendekezo ya mambo ambayo tunaweza kufanya kwa haraka; hata kama itabidi Controller of Budget aombwe ...
view
7 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu la Seneti. Ningependa kumpongeza Sen. Cherargei kwa kutayarisha taarifa hii. Nimechangia pakubwa katika utayarishaji wa taarifa hii, kwa hivyo, baadhi ya kongole pia zinafika kwangu.
view