7 Nov 2019 in Senate:
La msingi, Bw. Spika, ni kwamba uhuru wa Mahakama ni kiungo muhimu katika demokrasia ulimwenguni kote. Ndio maana katika kila sehemu, mahakama zinapewa uhuru wao ili kuhakikisha kwamba zinaamua haki baina ya wananchi na serikali; na pia baina ya wananchi kwa wananchi. Kwa hivyo, ni muhimu kwetu, kama Bunge la Seneti, tusisitize juu ya umuhimu wa uhuru wa mahakama. Uhuru wa mahakama uko mara mbili; kuna uhuru wa utenda kazi, ili kwamba mahakama zinapofanya kazi haziingiliwi kwa njia yoyote. Ndio maana tuko na Judicial Service Commission (JSC), ambayo inasimamia mahakama, kama vile hapa Bunge, tuko na Parliamentary Service Commission (PSC).
view
7 Nov 2019 in Senate:
Bw. Spika, kwa siku za karibuni, uhuru wa Kamati hii ya usimamizi wa mahakama umeingiliwa katika utendakazi wake. Hii ni kwa sababu mapendekezo ambayo yamepelekwa kwa Serikali kuhusiana na uchaguzi ama uteuzi wa majaji umekwamishwa. Huko ni kuingilia uhuru wa mahakama, na ni lazima sisi Wabunge wa Seneti tukemee jambo hilo.
view
7 Nov 2019 in Senate:
Karibu, Bi. Spika wa Muda. Uhuru wa kifedha ni muhimu, kwa sababu unaipa taasisi ile ya Serikali uhuru wa kupanga matumizi na ukusanyaji wa fedha zake, ambao unaipa mahakama fursa ya kupanga kazi zake na matumizi yake bila ya kuingiliwa na taaasisi yoyote nyingine ya Serikali.
view
7 Nov 2019 in Senate:
Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, mahakama Kenya zimepata misukosuko ambayo imsesababisha kuangalia utendakazi wake. Vile vile lazima mahakama zilindwe, kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
7 Nov 2019 in Senate:
sababu ndipo mahali pekee ambapo raia wanaweza kukimbilia wakati wamepata matatizo.
view
7 Nov 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, suala la uhuru wa mahakama ni muhimu sana katika demokrasia. Hii ni kwa sababu mtu yeyote atakapopatikana na matatizo, lazima aende mahakamani ili kuhakikisha kwamba haki zake zitalindwa. Hivi sasa, Serikali imeingia katika vita dhidi ya ufisadi. Vita vile haviwezi kupigwa wakati mahakama hazina fedha na majaji wa kutosha kusimamia kesi zile. Vita dhidi ya ufisadi haviwezi kufaulu iwapo mahakama zitakuwa hazina nyumba za mahakama, na vilevile wafanya kazi kuhakikisha kwamba kazi zile zinafanyika.
view
7 Nov 2019 in Senate:
Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, lazima tukemee vitisho vya Serikali kupunguza ruzuku kwa mahakama, na mawazo ya Serikali kwamba wanaweza kuendelea kujaribu kukwamisha utendakazi wa mahakama. Ni lazima tukemee upokonyaji wa uhuru wa mahakama, kwa sababu Uhuru huu utakapopokonywa, wananchi ndio watakuwa wanalalamika na kupoteza haki zao.
view
7 Nov 2019 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii.
view
6 Nov 2019 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I beg to lay the following Paper on the Table of the Senate today, Wednesday, 6th November, 2019 - Report of the Parliament of Kenya Delegation to the 64th Commonwealth Parliamentary Conference (CPC) held in Kampala, Uganda, from 22nd to 29th September, 2019.
view
6 Nov 2019 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view