Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1731 to 1740 of 1994.

  • 24 Jul 2019 in Senate: kwa lugha ya Kiingereza . Tumeelezwa kwamba kaunti nyingi hazina kamati za ukaguzi au uhasibu. Tunaambiwa kuwa kaunti nyingi hazina vidhibiti ambavyo vinaweza The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 24 Jul 2019 in Senate: kufuatiliwa kulingana na sharia ili kuhakikisha kwamba fedha za umma hazifujwi ovyo ovyo. Jambo linguine ni kuwa kuna udhaifu katika rasilimali ya binadamu, yaani human view
  • 24 Jul 2019 in Senate: kwa Kiingereza. Kwanza, utapata kwamba katika kaunti nyingi, uajiri wa wafanyikazi unafanywa kwa kikabila. Utapata kwamba asilimia zaidi ya 70 ni wa kutoka kabila moja, na hii inavunja sharia. Inamaanisha kwamba wafanyikazi hawawezi kuajiriwa kulingana na uwezo wa kufanya ile kazi. view
  • 24 Jul 2019 in Senate: Vile vile, kaunti nyingi zina jopo la wafanyikazi lililo vimba, yaani a bloated view
  • 24 Jul 2019 in Senate: kwa Kingereza. Utapata kwamba wafanyikazi wengi wamekaa maofisini na hawafanyi kazi yoyote. Jana tulikuwa na Gavana wa Garissa, aliyesema kwamba yuko tayari kuchukua makarani waliokuwa wengi katika kaunti ile, ili waende wakafanye kazi kama waalimu wa shule za chekechea. Hicho ni kioja, kwa sababu karani ambaye amekaa ofisini hajui ni mambo gani yanayotakikana kufundishwa katika shule za chekechea. Pale ndipo panatikana msingi wa wanafunzi kufuata masomo kulingana na vile ambavyo anaweza kuelewa. Bi. Spika wa Muda, tatizo la uvimbe wa jopo la wafanyikazi linaathiri karibu kaunti zote. Vile vile, katika hao wafanyikazi, kuna ukosefu wa usalama wa kazi. Utapata kuwa ... view
  • 24 Jul 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, matatizo haya yaliyoko katika kaunti hizi pia yako katika Serikali Kuu. Lakini kwa vile Ripoti inazungumzia serikali za kaunti tu, inamaanisha kwamba hatutapata fursa ya kuyaangazia yale maovu ambayo yako katika Serikali Kuu. view
  • 24 Jul 2019 in Senate: Mwisho, Bi. Spika wa Muda, ni kwamba ofisi ya Mkaguzi Mkuu imeweza kufanya kazi nzuri sana, ijapokuwa kuna upungufu hapa na pale--- view
  • 24 Jul 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Mkaguzi Mkuu amefanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba anaangazia yale madhambi ambayo yanatendeka katika kaunti hizi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 24 Jul 2019 in Senate: Nakubali pia kwamba Controller of Budget anafanya kazi, lakini madhambi mengi yangeweza kuepukika iwapo angekuwa akifanya kazi sawa sawa. view
  • 24 Jul 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus