23 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Kuambatana na kifungu cha 47(1) cha Kanuni za Bunge la Seneti, nimesimama kutoa taarifa hii kuhusu mipango ya Serikali Kuu kujenga, kwa niaba ya kaunti tano za eneo la Pwani, makao makuu ya Idara ya Uvuvi katika eneo la South C, Jijini Nairobi. Bw. Spika wa Muda, kama unavyojua uvuvi ni mmojawapo ya huduma ambazo zimegatuliwa kuligana na Katiba ya Nchi. Huduma hizi, hivyo basi, zinapaswa kutolewa na Serikali za Kaunti, na maswala yote kuhusu uvuvi kusimamiwa na serikali zizo hizo. Kama inavyojulikana uvuvi unapatikana zaidi maeneo ya Pwani, maeneo ya ...
view
18 Jul 2019 in Senate:
On a point of order, Madam Temporary Speaker.
view
18 Jul 2019 in Senate:
On a point of order, Madam Temporary Speaker. To the best of my knowledge, there is no Division of Revenue Act (DoRA) that has been assented to. Can Sen. Halake clarify?
view
18 Jul 2019 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kupunguza muda wa Mswada wa DORA ambayo imewasilishwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti. Kwanza, ninachukua fursa hii kuwapongeza viongozi, Spika na Maseneta wote ambao walijitolea asubuhi ya leo kufika mahakamani ili kuwasilisha kesi muhimu ambayo itaangalia mustakabali wa sheria kwa muda mrefu utakaofuata. Kilikuwa ni kitendo cha ujasiri na vile vile ni kitendo cha ustaarabu kwa sababu hatuwezi kuwa tunapigana saa zote wakati kuna taasisi za kisheria.
view
18 Jul 2019 in Senate:
Naomba unilinde kutokana na Sen. (Dr.) Milgo, kwa sababu wanashauriana kwa sauti zaidi.
view
18 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nimeona ya kwamba, ni kitendo cha ujasiri na pia cha kistaarabu kwa sababu sisi kama Wabunge hatufai kogombana hadharani kwa muda mrefu. Kilikuwa ni kitendo cha ujasiri na tunakiunga mkono na tutakuwa tayari sisi mawakili ambao tuko katika Bunge hili kuwakilisha kesi hii mpaka itakapofika tamati. Mswada ambao uko mbele yetu ni muhimu kwa sababu tumeona ya kwamba, DORA haijapitishwa, ilhali Bunge la Kitaifa lilipitisha Appropriations Bill . Inafaa tupitishe hiyo Division of Revenue Bill (DORA) kwa haraka zaidi ili kusiwe na upungufu wowote wa huduma kwa wananchi ambao wanategemea pesa hizi ziwafikie ili waweze kupata ...
view
18 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, tumeona kwamba kumekuwa na mvutano wa---.
view
17 Jul 2019 in Senate:
Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kiswahili ni lugha ya taifa. Tunajua kwamba wengi wetu sio mahiri katika lugha hii. Lakini ni sawa kuwaruhusu Seneta wenzangu wazungumze lugha ya Kiswahili bila kutatizwa na hoja za nidhamu ambazo nyingine hazina msingi. Bw. Spika, ufasaha wa lugha unatokana na uzungumzaji wa lugha mara kwa mara. Kwa hivyo, nakubali kwamba ndugu yetu, Seneta, kutoka Gatuzi wa Narok hana uzoefu wa kuzungumza Lugha ya Kiswahili katika Bunge hili lakini akipewa fursa ataweza kuzungumza lugha hii kwa ufasaha kwa sababu alizaliwa kama Mmaasai na sio Mwingereza. Kawaida huwa anaongea lugha ya Kingereza kama Mwingereza. ...
view
17 Jul 2019 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Hatufai kumsulubisha Sen. (Dr.) Zani kwa kutumia neno “mzungumzishi”. Hii ni kwa sababu lugha ya Kiswahili ni lugha ambayo inakuwa. Kwa mfano, katika msamiati au Kamusi ya Kiswahili hatukuwa na neno ‘tarakilishi.’ Lakini kwa vile lugha inaendelea kukua tumepata maneno mengi mapya. “Mzungumzishi” ni baadhi ya maneno ambayo yamekuja baada ya kukua kwa Lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, badala ya kumsulubisha Sen. (Dr.) Zani, angepewa muda wa kuwasilisha ushahidi kwamba neno hili linakubalika katika Lugha ya Kiswahili. Nafikiri hiyo ndio itakuwa njia sawa ya kumsaidia na kutusaidia sisi ambao tuko hapa. Lakini napinga ufafanuzi wa Sen. ...
view
16 Jul 2019 in Senate:
Mr. Deputy Speaker, Sir, I would agree with Sen. Wetangula, that it will be more cost effective if the Attorney-General could take up a class action suit, rather than each of the families making a separate application, which may be cumbersome and time consuming. Therefore, it would be better for him to take over the matter and apply jointly for the death certificates of all the victims. Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir.
view