9 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Arifa ya Sen. Nyamunga kumpongeza Sen. Halake kwa kuteuliwa kama Mwenyekiti wa Taasisi ya Demokrasia ya Vyama Vingi katika nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika, naungana na Sen. Nyamunga kumpongeza kwa moyo wangu wote Sen. Halake kwa kuchaguliwa kwake. Ni jambo la kutia moyo kwamba ni mara ya kwanza kwa Sen. Halake kuteuliwa kama Seneta na kuchaguliwa kama Mwenyekiti wa Taasisi ya Demokrasia ya Vyama Vingi nchini Kenya. Bw. Spika, nimefuatilia kwa karibu utendakazi wa Sen. Halake na ninaona ya kwamba anatosha kuendesha Taasisi ile wakati huu ambapo siasa ya vyama ...
view
9 Jul 2019 in Senate:
ndiye anaamua maamuzi yote ya chama wakati wanachama wenyewe hawana fursa yote ya maamuzi. Bw. Spika, ningependa kuchukua fursa hii kueleza kwamba bado demokrasia kamili haijakamilika hapa nchini. Hii ni kwa sababu watu wengi bado wanagadamizwa katika haki zao za kibinafsi na kibinadamu. Juzi kule Murang’a, wanafunzi kadhaa walifukuzwa shule kwa sababu walikuwa wamevaa hijab . Nina furaha kwamba aliyechaguliwa kuendesha mambo ya Taasisi ya CMD ni Sen. Halake ambaye anavaa hijab wakati wote anapokuwa Bungeni na nje.
view
9 Jul 2019 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ya taanzia kutoka kwa Seneta wa Vihiga kuhusiana na Marehemu Joe Kadenge. Kwanza ningependa kuchukua fursa hii kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya watu wa Kaunti ya Mombasa kupeleka rambi rambi zetu kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa mwendazake Kadenge kutokana na kifo chake hapo juzi. Joe Kadenge alikuwa mchezaji mpira mzuri, shupavu na vile vile aliiletea sifa nyingi nchi yetu ya Kenya. Kule Mombasa tuliweza kumtuza, ijapokuwa kwa uchache, mwendazake Kadenge na jina la barabara; ile barabara kuu inaoenda mpaka Stadium imeitwa jina lake ‘Joe ...
view
9 Jul 2019 in Senate:
Mwingine ambaye tuko na yeye Mombasa ni Mzee Ali Kaja ambaye pia alikuwa mchezaji. Aliwahi kucheza mpira kwa timu ya taifa la Kenya pamoja na marehemu Joe Kadenge. Kwa hivyo tunapozungumzia kifo cha Joe Kadenge, tuzingatie kwamba kwa sasa kuna haja ya serikali kutilia mikazo zaidi maswala ya michezo kwa sababu michezo ndiyo inasaidia kukuza vipaji vya vijana wetu. Michezo kama riadha inapatia Kenya pesa nyingi kutokana na ushindi ambao huwa tunapata. Wanamichezo wengi wanapata shida kwa sababu hawajakuwa mentored . Hao hufikiria ya kwamba watazidi kupata pesa wanapozidi kukimbia na hiyo ndiyo huwafanya wajimalize kimchezo. Mbali na kujenga taasisi ...
view
18 Jun 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja ambayo imeletwa mbele ya Bunge na Sen. Kibiru, Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga, ambaye tulisoma naye Chuo Kikuu cha Nairobi. Hoja hii imekuja katika wakati mwafaka, kwa sababu kila mwaka kuna malimbikizi ya pesa na madeni katika kaunti. Serikali Kuu ya Kenya inazidi kuongeza madeni kwa sababu ya miradi ambayo inafanywa bila ya kukamilishwa. Bi. Spika wa Muda, kiasi cha Kshs360 billion sio pesa kidogo, ikikumbukwa kwamba Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Mheshimiwa Rais mstaafu Kibaki ilikuwa Kshs240 billioni. Kwa hivyo, sasa tuna kiasi Kshs360 billioni ambazo ...
view
18 Jun 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, kuna miradi mingine ambayo imeanzishwa na hizi serikali za ugatuzi ambazo zimekuwa mamlakani kutoka mwaka wa 2013 hadi 2017, na wakarejea tena kwa muhula wa miaka ya 2017 hadi 2022. Miradi hii pia imekwama kwa sababu ya kukosa kulipa wanakandarasi. Tuliwahi kuzuru Kaunti ya West Pokot, ambapo tuliona miradi mingi iliyoanzishwa na Gavana aliyetangulia. Miradi hii imekwama katika serikali ya Gavana wa sasa, Gov. Lonyangapuo. Miradi hiyo imekwama ilhali pesa nyingi zimetumika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard ...
view
18 Jun 2019 in Senate:
Wananchi wanapata shida kwa sababu miradi ambayo ilikuwa imekusudiwa kama vile zahanati, shule za chekechea, barabara za kutumika kupeleka mazao sokoni haraka na wakati unaofaa. Zote hizo zimekwama kwa sababu miradi hiyo haijakamilika, na sasa imaekuwa donda sugu. Malimbikizi ya madeni inakabili serikali za kaunti. Vile vile, waliofanya kandarasi zile kwa pesa zao na kwa mikopo wanapata shida, kwa kushtakiwa na mali yao kuuzwa na madalali.
view
18 Jun 2019 in Senate:
Ukitazama gazeti la jana la Daily Nation, utapata kurasa zaidi ya kesi kumi ambapo madalali wanauza mali ya Wakenya kwa sababu ya kushindwa kulipa mikopo. Mikopo yenyewe ni ya wale waliopewa kandarasi za kazi za kaunti au serikali na kushindwa kulipa hiyo mikopo, kwa sababu Serikali Kuu au serikali za kaunti zimekataa kuwalipa. Kutokamilishwa kwa miradi kwa wakati unaofaa kunaleta athari kwa serikali na uchumi wa nchi. Hii ni kwa sababu hatutatumia kikamilifu miradi iliyofanywa, ilhali pesa zimetumika na miradi kukwama. Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii kwa sababu itasaidia kuhakikisha kwamba serikali za kaunti na ...
view
18 Jun 2019 in Senate:
Juzi, Kamati ya CPAIC ilizuru Kaunti ya Samburu, ambako tulipata miradi mingi imekwama kwa sababu ya ukosefu wa fedha, ilhali kila mwaka tunaomba fedha za kuendesha miradi hii. Kila mwaka, watu wanatengeneza Annual Development Plans (ADP) ili kusaidia kutekeleza Vision 2030, ambayo ni ramani inayotumika na Serikali kuhakikisha tunapata maendeleo nchini. Kila miradi inapokwama, maendeleo yanabaki nyuma, na Serikali inashindwa kufikia Millennium Development Goals (MDGs), ambazo zimekwama katika Ruwaza ya 2030 katika mwongozo wa miradi ya Serikali. Ni muhimu kabla ya miradi mipya kuzinduliwa, ile iliyopangwa kufanyika katika mwaka fulani wa fedha za serikali ikamilishwe. La sivyo, ni muhimu kuweka ...
view