18 Jun 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, Wabunge au magavana pia wanabagua sehemu ambazo hazikuwapigia kura. Utapata sehemu zilizopigia kiongozi fulani kura kwa wingi zinapelekewa miradi kwa wingi, na kule kwingine hakupati miradi yoyote. Kwa hivyo, jambo hili linasababisha kutokuwa na usawa wa maendeleo katika sehemu tofauti za kaunti moja. Kwa hivyo, hili ni donda sugu. Ni lazima tutafute njia mwafaka ya kuhakikisha kwamba miradi inakamilishwa kwanza kabla ya kuanzishwa miradi mipya na serikali za kaunti au Serikali Kuu. Vile vile, lazima maendeleo yasambazwe katika maeneo yote katika kaunti ama nchi kwa usawa, kwa sababu sote tunalipa kodi katika mfuko mmoja. Haiwezekani kwamba ...
view
18 Jun 2019 in Senate:
Nikimalizia, hii miradi lazima ikamilishwe kwa wakati unaofaa ndio wananchi wafaidike na miradi iliyonuiwa kufanyika.
view
18 Jun 2019 in Senate:
Naunga mkono Mswada wa Sen. Kibiru.
view
13 Jun 2019 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ya Seneta wa Kaunti ya Kericho, Sen. Cheruiyot. Maswala ya pasipoti imekuwa donda sugu kwa wakaazi wa pwani kwa jumla hususan wale waumini wa dini ya Kislamu. Sheria inayotumika kuwapa Waislamu pasipoti ni tofauti na sheria inayotumika kuangalia maombi ya pasipoti ya Wakenya wengine.
view
13 Jun 2019 in Senate:
Hivi majuzi tulikuwa na mchakato wa kuandikisha Huduma Namba. Stakabadhi zilizokuwa zinahitajika kuandikisha Huduma Namba zilikuwa kadi ya kitambulisho au cheti cha kuzaliwa pekee lakini kupata pasipoti, unahitajika kuleta vyeti vya kuzaliwa za babu na babu.
view
13 Jun 2019 in Senate:
Babu yangu alipozaliwa, Kenya haikuwa imepata uhuru. Kenya ilipata uhuru mwaka wa 1963. Kwa hivyo, sitapata cheti cha kuzaliwa cha babu yangu kuonyesha kwamba yeye ni Mkenya kwa sababu Kenya haikuwa imepata uhuru alipozaliwa. Donda sugu la pasipoti limekuwa likiwapa Wakenya wengi hususan wale wa kaunti ya Mombasa na miji mingine ya pwani shida kubwa.
view
13 Jun 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, maeneo mengine penye ofisi za pasipoti ni kama Kisumu, Nakuru, Kisii, Embu na maeneo mengine ambapo mwendo ni kama kilomita 100 au 50 kutoka Nairobi. Wale wanaohitaji huduma hizi kwa wingi wamenyimwa nafasi za kuwa na pasipoti. Kwa mfano, pwani nzima, ofisi ya paspoti ni moja tu mjini Mombasa.
view
13 Jun 2019 in Senate:
Naunga mkono taarifa hii ili tuhakikishe Wakenya wanaweza kupata pasipoti kwa njia rahisi. Nafasi za kazi hapa Kenya ni adimu, kwa hivyo wengi wakiwa na pasipoti, wataweza kuenda kufanya kazi katika nchi zingine ili waweze kujielendesha kimaisha. Ikiwezekana, Kamati husika inafaa kutembelea ofisi za pasipoti ili wajionee shida zinazowakumba Wakenya.
view
13 Jun 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, Wakenya wengine wenye dini ya Kiislamu huambiwa kwamba lazima wafanyiwe vetting . Hakuna sheria inayosema kwamba lazima mtu afanyiwe vetting ndipo aweze kupata pasipoti. Ikiwa mtu ana kitambulisho au cheti cha kuzaliwa, hafai kufanyiwa vetting anapotafuta paspoti.
view
29 May 2019 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia arifa ya Sen. Pareno. Bw. Naibu Spika, hili swala la kulipwa ridhaa kwa wale wanoathirika na miradi ya Serikali limekuwa donda sugu sasa. Kule Mombasa, walijenga SGR ambayo imeweze kufanya kazi kwa muda wa miaka mbili. Lakini, mpaka sasa, kuna watu ambao hawajalipwa ridhaa ya ardhi yao. Pia mali yao ilichukuliwa wakati wa ujenzi wa reli lakini hawajahi kulipwa ridhaa. Hivi sasa, kuna mradi wa Magongo Road ambao unaendelea. Contractor tayari yuko kwenye mradi huo na amelipwa lakini wale ambao wameathirika hawajalipwa. Zile fidia ambazo zinatakikana kulipwa, zimetengenezwa kwa njia ambayo ...
view