29 May 2019 in Senate:
Miradi yote ya Serikali imekwama kwa sababu Serikali imeshindwa kufidia watu.
view
29 May 2019 in Senate:
Wakati Kamati itakuwa inashughulikia swala la Sen. Pareno, wadau wa sehemu nyingine ambazo zimeathiriwa, kwa mfano, Mombasa, Makueni, Elgeyo-Marakwet ambako kuna mradi wa Bwawa la Kimwarer na hata hapa Nairobi ambapo kuna ujenzi wa barabara kule Westlands waitwe ili tulitatue swala hili mara moja.
view
23 May 2019 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa kuchangia Taarifa hii iliyoombwa na Seneta wa Kaunti la Kilifi, Mhe. Madzayo. Hili swala la watu kuvunjiwa nyumba na makazi kiholela limekuwa donda sugu katika Kaunti za Kilifi an Mombasa. Mnamo tarehe moja Mwezi huu wa Tano, ambayo ilikuwa siku kuu rasmi ya Serikali, watu wa sehemu ya Mukani kule Bamburi walivamiwa alfajiri na polisi wenye bunduki. Walivunjiwa makazi yao wakati huo ambapo walikuwa na majadiliano na Kamishna wa Kaunti ya Mombasa kuhusu ardhi hiyo.
view
23 May 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, watu wanavunjiwa makazi bila kupewa makazi mbadala. Kuna sheria maalum kuhusiana na maswala ya watu kubomolewa nyumba zao. Kama ni
view
23 May 2019 in Senate:
lazima yule anayetakikana kuondolewa apewe arifa sawasawa na makazi mbadala wakati atakapohamishwa. Lakini utapata kwamba mahamisho mengi yanafanyika siku ya Jumapili ama siku ambazo ni siku kuu rasmi za Serikali. Amri za The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
23 May 2019 in Senate:
mahakama hazifai kutekelezwa siku za Jumapili, Jumamosi ama siku kuu rasmi ya Serikali. Tulitarajia kwamba hili donda sugu litatatuliwa na National Land Commission (NLC). Lakini Tume hiyo ilitumia muda wake wa miaka sita na ambao uliisha bila kuondoa tatizo kubwa la dhuluma za kihistoria kuhusiana na ardhi katika miji ya Mombasa na Kaunti za Kilifi na Kwale. Bw. Spika wa Muda, tungeomba Kamati ya Seneti ambayo itapatiwa jukumu la kuchunguza swala hili, iingilie kwa undani swala hili; ichunguze sehemu ya Kilifi na Pwani nzima ambako kuna dhuluma za kihistoria. Mpaka sasa miaka karibu kumi baada ya kuwa na Katiba mpya, ...
view
21 May 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono maombi ambayo yameletwa na wakaazi wa Kisumu. Ni kweli kwamba kwa sasa, Serikali haina utaratibu kwa maswala ya nyumba. Kwa mfano, kule Mombasa, nyumba zinazomilikiwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
21 May 2019 in Senate:
na National Housing Corporation (NHC) hususan National Housing Estate Magongo, wakaazi wamekuwa wakipata shida sana. Kodi zimeongezwa ilhali wanaishi katika hali duni. Nyumba zao zimeezekwa au zimefunikwa juu na mabati ya asbestos ambayo inadhuru afya ya binadamu. Bw. Spika, huu ni wakati mwafaka wa kuunga mkono maombi ya watu wa Kisumu kwa sababu maswala ya nyumba yanaathiri sehemu zote za nchi. Ujenzi was nyumba ni mojawapo ya Big Four Agenda ya Serikali. Lakini utapata mpaka sasa nyumba ambazo watu wengi wanaishi hususan wafanyikazi wa Serikali ni duni sana. Kwa mfano, nyumba zote katika Mbaraki Police Line zinafaa kupigwa marufuku kwa ...
view
21 May 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ya Sen. Cherargei wa Kaunti ya Nandi. Kwanza ninalaani kitendo cha polisi chakumkamata Seneta wa Kakamega pamoja na aliyekuwa waziri wa michezo na Mbunge wa Matungu, kufuatia ghasia zinazotokea katika maneo ya Matungu. Kama wabunge na viongozi, tuna haki ya kuheshimiwa na kupewa fursa ya kujiwasilisha katika Makao Makuu ya polisi ama mahali popote polisi atatuhitaji kuliko kutushika hadharani, kututia pingu na kutupeleka kama ambao ni wahalifu. Kisa cha Mhe. Gikaria, Mbunge wa Nakuru Mjini ni cha kusikitisha sana. Hii ni mara ya pili mwaka huu yeye kushikwa. Kila anaposhikwa, ...
view
21 May 2019 in Senate:
Alitengamana na washukiwa wengine waliokuwa korokoroni na ikawa maisha ya kawaida kama vile anavyoishi kama mheshimiwa. Ninafikiri huo ni uzoefu wake wa nyuma uliyomfanya kuwa na uvumilivu wa aina hiyo alipoingia maeneo ya shida.
view