Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1781 to 1790 of 1994.

  • 21 May 2019 in Senate: Bw. Naibu Spika, la msingi ni kwamba, hii Katiba ambayo tuliipigania kwa muda mrefu na kuiopitisha, hivi sasa inachukuliwa kama karatasi tu. Katiba inasema kwamba yeyote anayeshtakiwa mahakamani, apewe bond mara moja iwapoatazuiwa kwa zaidi ya masaa 24. Licha ya Mhe. Malalah kuwa Seneta wa Kaunti ya Kakamega, aliwekwa ndani kwa siku tatu. Waswahili wanasema kwamba, ukiona mwenzako ananyolewa, tia kichwa chako maji. Sasa ninaona upande wa Serikali katika Bunge hili unaona kwamba kweli yale malalamiko ambayo maseneta wa upinzani walikuwa wanalalamika, yanaweza kuwafikia. Tulilalamika hapa wakati Babu Owino aliwekwa korokoroni bila sababu yoyote. Tulilalamika wakati Wabunge sita waliotambulika kama ... view
  • 21 May 2019 in Senate: Bw. Naibu Spika, bahati nzuri Mahakama ya Shanzu ikaona makosa yale hayakuwa na msingi wowote na wakayatupilia mbali. Mkuu wa Polisi ameajiriwa tu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 21 May 2019 in Senate: juzi hata miezi miwili haijaisha. Ni aibu kuona polisi chini yake wakivunja sharia ovyo ovyo. Lazima Mkuu wa Polisi na Waziri Matiang‘i waje hapa. Wakati tulipozungumzia ulaghai wa shamba la Ruaraka, kuna wale waliyosema kwamba Matiang‘i ni mweupe kama theluji, lakini sasa wanaona zile shida ambazo tunapata kutoka kwake. view
  • 15 May 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Ripoti ya Uwiano ambayo imeletwa hapa na Sen. Ndwiga. Kwanza nampongeza Sen. Ndwiga pamoja na wenzake ambao walikaa katika Kamati ya Uwiano wakakubaliana na kuleta mapendekezo kuhusu The Warehouse Receipt System Bill, 2017 . Bunge inafaa kufuata njia hii ili kuondoa mtafaruku kati ya Senate na National Assembly. view
  • 15 May 2019 in Senate: Kulikuwa na umuhimu wa kuwepo kwa The Warehouse Receipt System Bill. Tukipitisha Ripoti hii itakuwa imepitia bunge zote mawili. Sisi kama Wabunge tuna kiapo kimoja kwamba tutakuwa waaminifu kwa Jamhuri ya Kenya na Katiba yake. Sioni kwa nini kuwe na mvutano baina ya Mabunge haya mawili. Wenzetu walipokutana kule Mombasa, walitumia fursa hiyo kutukashifu. Walisema kwamba sisi hatufanyi kazi yetu kama Senate. Katiba imetoa mwongozo kwamba kuwe na bunge mbili; Seneti na Bunge la Taifa. Tunajua kila Bunge lina kazi yake. Katiba pia inasema kuwa iwapo Mswada utapitishwa katika Bunge moja na ukataliwe katika Bunge jingine, tunafaa kuwa na Kamati ... view
  • 15 May 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, tulijadili hapa tarehe 30 mwezi uliopita, tulijadili hapa The Division of Revenue Bill na tukapendekeza marekebisho fulani ambayo yamekataliwa na Bunge la Taifa. Hayo yanafaa kushughulikiwa na kamati ya uwiano ambapo kuna Maseneta ambao watawakilisha Bunge hili ili kujadili Mswada huo. view
  • 15 May 2019 in Senate: Maseneta wote hapa wana tajriba ya kutosha kuwawezesha kukaa katika kamati yoyote na kuongoza katika nyadhifa zozote wanazopewa. Kwa hivyo, hatuna shaka kwamba watawasilisha maslahi yetu na maslahi ya kaunti zote katika Jamhuri ya Kenya kikamilifu. Sisi kama Seneti tutakubaliana na uamuzi wao. view
  • 15 May 2019 in Senate: Jana Kiongozi wa Wengi katika Seneti alisema kuwa Mswada ulitiwa sahihi na Rais kuwa sheria bila ya sisi kuhusishwa. Ni jambo la kustaajabisha kwamba Kiongozi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 15 May 2019 in Senate: wa Wengi katika Seneti alipeleka kilio matangani. Hiyo ni sawa na kupeleka kilio matangani kwa sababu yeye kama Kiongozi wa Wengi katika Seneti anakaa katika the Senate Business Committee (SBC). Kwa hivyo, wao ndio viongozi wa Seneti. Wamechukua hatua gani kuhakikisha kwamba malamiko yetu yanafikia ofisi husika? Wangeandika barua ya malalamiko kwa Mkuu wa Sheria, Spika wa Bunge la Taifa na Ofisi ya Rais kwamba Sheria hiyo ilipitishwa bila ya kujadiliwa na Seneti kama inavyoeleza Katiba. Kwa hivyo kuja hapa kutulilia haitasaidia chochote kwa sababu tayari sheria imepitishwa na sisi kama Bunge la Seneti inafaa kuwapa mamlaka ya kusonga mbele ... view
  • 15 May 2019 in Senate: Bi. Spika wa Muda, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuchangia. Hii ni mara yangu ya kwanza kuongea katika muhula huu ambao tumeanza jana, ninawatakia Waislamu wote na Maseneta wezangu Waislamu katika Jamhuri ya Kenya Ramadhan Mubarak. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus