Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1791 to 1800 of 1994.

  • 30 Apr 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa ugavi wa pesa za Serikali kwa muhula wa mwaka wa 2019/2020. Kwanza, ninaunga mkono lakini kwa masharti. Ni lazima ufanyiwe marekebisho kwa sababu mapendekezo ya Kamati ya Fedha ya Seneti yalipuuzwa wakati Mswada ulipopitishwa katika Bunge la Kitaifa. Mapendekezo kwamba pesa ziongezwe kutoka Kshs314 billion zilizotolewa mwaka huu mpaka Kshs335 billion. Mapendekezo hayo yalipuuzwa na Bunge la Kitaifa. Kupuuzwa huko ilikuwa ni dharau kwa Bunge la Seneti kwa sababu Seneti ndiyo inayoangalia maslahi ya kaunti zote. Bunge la Seneti ikisema kwamba pesa zinazotosha ni Kshs335 billion ni kwamba wamepima ... view
  • 11 Apr 2019 in Senate: Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa fursa hii ili niwakaribishe wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Kenya Navy Mtongwe, Mombasa. Ni furaha kupokea wageni kama hao kutoka Mombasa na ninatumaini ya kwamba wataweza kujifunza mengi ambayo yanafanyika hapa, haswa katika Bunge la Seneti. Nachukua fursa hii kuwakaribisha. Karibuni tena. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Petition iliyoletwa na ndugu yangu Sen. Mwaruma anayewakilisha Taita-Taveta. Swala la watu kulipwa fidia kutokana na matumizi ya ardhi zao limekuwa donda sugu. Serikali inajizatiti kuhakikisha kwamba kuna maendeleo. Licha ya hayo, maafisa wengi wa theNLC wamekuwa watepetevu katika kulipa fidia kwa watu ambao ardhi zao zinachukuliwa. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Hivi majuzi, Kamati ya Uchukuzi ilikuwa na kikao hapa Nairobi. Kuna watu ambao hawajalipwa fidia miaka minne baada ya aliyepewa kandarasi kuanza kutengeneza barabara. Wale wote ambao ardhi yao ilichukuliwa hawajalipwa chochote mpaka sasa na hawajui watalipwa pesa ngapi. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Kule kwetu Mombasa, bado watu hawajalipwa kutokana na ardhi iliyochukuliwa kwa ajili ya mradi wa the Standard Gauge Railway (SGR). Sasa inaelekea miaka miwili. Kwa hivyo, hili ni donda sugu na lazima Waziri wa Usafiri na Maendeleo ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Miundombinu na mwenzake wa Ardhi waitwe hapa ili waeleze kwa nini hawalipi watu kwa wakati. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Watu wengi wanaotakikana kulipwa ni walalahoi. Wanalazimishwa kungojea fidia yao wakati watu wengine Serikalini wanakula pesa na kufanya maombi jinsi wanavyotaka. Kwa hivyo, Mawaziri hao wawili wanafaa kuitwa ili kueleza kwa nini watu hawajalipwa wakati barabara inaendelea kutengezwa. view
  • 9 Apr 2019 in Senate: Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Arifa ya Sen. (Dr.) Milgo kuhusiana na maswala ya watu kujitoa roho kwa sababu ya matatizo ya maisha. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu tunaona ya kwamba Wakenya wengi wanaendelea kupoteza maisha kwa sababu ya taabu za kidunia ambazo zinawakumba. view
  • 9 Apr 2019 in Senate: Serikali inafaa kuangalia kwa makini chanzo cha watu kujiua kwa sababu wengi wanaojiua ni watu ambao wana akili timamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba tunapoteza watu katika hali kama hizo. Tunafaa tuangalie kama miundo msingi ya nchi yetu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 9 Apr 2019 in Senate: inapotea. Mmomonyoko wa maadili na mambo mengine kama hayo yana sababisha watu waone kwamba ni rahisi kuchukua maisha yao kuliko kuendelea kuishi maisha yao. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus