9 Apr 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, nachukua fursa hii kuchangia Hoja ya mbolea ya samadi ambayo ni rahisi kupatikana katika kila sehemu ya nchi. Wengi wetu tuna mifugo kama kuku, mbuzi, ng‟ombe, kondoo, ngamia---
view
9 Apr 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Rais kwa Seneti na Bunge la Kitaifa. Kwanza ningependa kumpongeza Rais kwa Hotuba yake ambayo alilihakikishia Taifa kwamba nchi itaongozwa kwa sheria. Alikataa sheria kutumiwa vibaya na hiyo inamaanisha kwamba nchi itaendelea kuongozwa na Katiba yetu ambayo tulianzisha mwaka wa 2010.
view
9 Apr 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ningependa pia kumpongeza Rais kwa hakikisho lake kwamba ataunga mkono ugatuzi. Ugatuzi ndiyo jambo kubwa ambalo lililetwa na Katiba ya mwaka wa 2010. Mpaka sasa alithibitisha ya kwamba karibu trillioni moja na billioni mia saba zimeweza kutumika katika Kaunti zetu, ambazo zimeleta maendeleo tofauti tofauti.
view
9 Apr 2019 in Senate:
Ukiangalia sura ya nchi, inabadilika kila sehemu kwa sababu ya ugatuzi. Ijapokuwa kuna changamoto nyingi katika kutekeleza ugatuzi, pesa zile zimeweza kuleta tofauti kubwa na vile mambo yalivyokuwa wakati wa nyuma. Kwa hivyo, hakikisho la Rais kwamba ataendelea kuunga mkono ugatuzi, limekuja katika wakati mwafaka.
view
9 Apr 2019 in Senate:
Ningependa kumpongeza Rais pia kwa kuunga mkono na kutoa hakikisho kwamba ile hatua ya ujengaji madaraja, yaani, “ Building Bridges Initiative ” itaendelea kuwa, kwa sababu imeweza kuleta amani kwa muda mchache ambao tumekuwa nao - karibu mwaka mmoja. Alisema kwamba ataendelea kuiunga mkono kwa sababu ni njia ambayo inawaleta Wakenya pamoja. Joto la kisiasa limeweza kupungua licha ya wale ambao wanatangatanga wakitafuta kuungwa mkono kwa ugombezi wa Rais wa mwaka wa 2022, ambao kwa sasa sio muhimu kwa nchi. Cha muhimu sasa hivi ni kuweza kujenga nchi ili wananchi wapate fursa ya kupata kazi, biashara ziweze kuinuka na pia ...
view
9 Apr 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, tangu mkataba au mwafaka upatikane baina ya Rais Kenyatta na „Rais wa wananchi,‟ Mhe. Raila Amolo Odinga, joto la siasa limepungua. Wananchi wanaweza kufanya kazi, biashara zimeanza kufunguka na vile vile, hali ya uchumi wa nchi imeweza kupanuka na kufunguka. Biashara hususan katika Mji wa Mombasa zimeanza kuinuka, na hilo ni jambo nzuri kwa sababu ugatuzi unategemea pakubwa biashara katika maeneo yale, ili waweze kupata ushuru na kuinua hali ya maisha ya watu.
view
9 Apr 2019 in Senate:
Jambo ambalo limenisikitisha ni kwamba vita dhidi ya ufisadi vimekuwa ni domo kaya. Hii ni kwa sababu kila mwaka tunaambiwa kuwa watu watashtakiwa na mahakama The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
9 Apr 2019 in Senate:
zinafanya kazi. Hata hivyo, hakujakuwa na jambo lolote ambalo limefanyika ili tuweze kusema kwamba vita dhidi ya ufisadi imeanza kuzaa matunda. Imekuwa ni ahadi juu ya ahadi kila mwaka kwamba tunapigana na ufisadi.
view
9 Apr 2019 in Senate:
Mhe. Rais alisema kuwa Mawaziri wanane na Principal Secretaries wanane waliweza kuwachishwa kazi au kuamrishwa wajiondoe katika mamlaka. Hata hivyo, hayo ni mambo ambayo yalifanyika mda mrefu uliopita na hatujaona matokeo yoyote katika vita dhidi ya ufisadi.
view
9 Apr 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nilitarajia Rais asizitize pesa zaidi ziongezwe katika idara ya mahakama ili tuweze kuanzisha mahakama nyingi zaidi ambazo zitaweza kusaidia kupambana na kesi za ufisadi. Kwa sasa inachukua zaidi ya miaka miwili kukamilisha kesi moja ya ufisadi. Iwapo mahakama zitaongezewa pesa, ina maana kwamba wataweza kuajiri mahakimu na makarani zaidi. Pia wataweza kuongeza ujenzi wa mahakama ili kesi ziweze kwenda kwa haraka.
view