9 Apr 2019 in Senate:
Tunatarajia kwamba pendekezo litafanywa kesi za ufisadi ziweze kukamilishwa kwa muda wa miezi sita kama vile kesi zinazohusu uchaguzi. Kesi hizi zikiendelea kukaa katika mahakama, washtakiwa wanapata fursa zaidi ya kujinasua na mwisho mashahidi wanapotea. Kwa hivyo, wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanaepuka kifungo ama adhabu kwa sababu hakuna ushahidi. Kwa hivyo, mahakama inapaswa iongeze dhamana ili tuhakikishe kwamba vita dhidi ya ufisadi inapamba moto. Nilisikitishwa kwamba Idara ya Kiongozi wa Mashtaka ya Serikali pamoja na Idara ya Upelelezi yani (DCI) haikupewa mwongozo wowote na Serikali kuhusu ni jambo gani wataweza kufanyiwa ili kuhakikisha kwamba uchunguzi unafanyika kwa haraka na stakabadhi za ...
view
9 Apr 2019 in Senate:
mtaa na usalama. Kwa hivyo, ikiwa wazee kama hawa watauliwa, itakuwa ni vigumu kwa vyombo vya Serikali kupata habari kuhusu mambo ya mitaa inavyokwenda. Bw. Spika wa Muda, tumeelezewa kwamba zaidi ya watu 15 katika eneo la Kwale wamepotea. Mombasa vile vile, zaidi ya watu 90 wamepotea na wengine wengi wameuawa katika hali za kutatanisha. Tumekubaliana kwamba nchi lazima iongozwe kwa sheria. Iwapo watu watauawa kiholela, inamaanisha kwamba imani kwa Serikali kulinda mali na maisha ya watu itapungua. Kwa hivyo, kuna hatari ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao na kusababisha maafa bila ya kujua kwamba Serikali ipo. Bw. Spika wa ...
view
9 Apr 2019 in Senate:
Kwa mfano, zaidi ya madereva 6,000 pamoja na wasaidizi wao ikiwemo wanaofanya kazi katika vituo vya mafuta wamepoteza kazi. Vile vile, biashara nyingi zimefungwa kwenye barabara ya kutoka Mombasa kuja Nairobi, kuanzia Mariakani hadi Mlolongo. Watu wa sehemu hizo walikuwa wanapata pesa wakati mizigo mingi ilikuwa inasafirishwa kutumia barabara. Simaanishi kwamba SGR isitumike. Ninacho maanisha ni kwamba wenye lori watengewe sehemu za kubebea mizigo. Hapo awali, kulikuwa na kile ninachoweza kusema “uchumi uliofungwa” na hatimaye tukawa na soko huru ili kuwezesha kila mtu aweze kufanya biashara na marketforces ziliamua bei ya kuuza mali. Iwapo tutaruhusu mizigo yote ibebwe kutumia SGR, ...
view
9 Apr 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, hatukatai kwamba kuna maendeleo lakini tunasema kwamba ni lazima biashara ifanywe kulingana na njia za haki. Hatuwezi kusema kwamba mizigo yote isafirishwe kwa reli kwa sababu reli kwa sasa haina uwezo huo. Iwapo mashirika ya biashara au wenye makampuni ya kusafirisha mizigo yatafunga biashara zile, watu wengi watapoteza kazi na vile vile, uchumi wetu utaathirika. Hii ni kwa sababu magari yote yanayosafiri yana nunua mafuta. Katika kila lita moja ya mafuta ambayo yanauzwa ambayo ni zaidi ya shilling mia moja, shilling 30 zinaingia kwa Serikali kama ushuru. Kwa hivyo, Serikali itapoteza ushuru, watu watapoteza kazi na ...
view
9 Apr 2019 in Senate:
Katika Hotuba yake, Rais hakueleza ni biashara gani mbadala ambazo zitafanyika kwa watu wa Kaunti ya Mombasa, baada ya kupoteza biashara yao ya Bandari kwa kupelekwa Naivasha. Alichosema ni kwamba SGR ikifika Naivasha, biashara zote za
view
9 Apr 2019 in Senate:
zitafanyiwa Naivasha. Sisi tunajivunia kwamba Bandari ndio rasilimali yetu kubwa. Iwapo utendakazi wa Bandari utaondolewa kutoka mjini Mombasa mpaka Naivasha, ina maana kwamba raslimali ile haitatufaa sisi. Hiyo ina maana kwamba Mji wa Mombasa uko katika hatari kubwa ya kufa katika siku zinafuata.
view
9 Apr 2019 in Senate:
Tumeona miradi mingi iliyoanzishwa na Serikali. Kwa mfano, katika Kaunti ya Tana River, wameanzisha mradi wa Galana-Kulalu. Mradi huo ulitakiwa upewe gatuzi la Tana River na Kilifi ili ufanywe kama mradi wa pamoja. Kama vile tunavyosema Kaunti ya Mombasa tupewe mradi wa Dongo Kundu Special Economic Zone ili uweze kusaidia kama biashara mbadala wa ile Bandari ya Mombasa ambayo kwa sasa inaondolewa pole pole. Ikiwa tutaruhusiwa kufanya Dongo Kundu Special Economic Zone, itasaidia pakubwa kuinua hali ya watu na uchumi wa Kaunti ya Mombasa. Hii ni kwa sababu watu watapata kazi, mizigo itaingia na watu watauza kama vile Dubai. Hiyo ...
view
9 Apr 2019 in Senate:
Kwa kumalizia, Bw. Spika wa Muda, tumeona kwamba katika maeneo mengine, Serikali imeanzisha miradi mikubwa kama vile ya kujenga mabwawa. Katika Kaunti ya Mombasa, maji bado ni changa moto kwa sababu hatuna mradi mwingine wa maji isipokuwa Mzima. Ijapokuwa mradi huu ulijengwa katika miaka ya 40 na kuwekwa Mzima One, Mzima Two na Mzima Three lakini mpaka leo, miaka 55 ya Uhuru, hatujajenga lakini nyingine ya Mzima Two kutoka Mzima Springs hadi Kaunti ya Mombasa. Kila mwaka, shirika la World Bank linatoa pesa za kufanya utafiti yaani
view
9 Apr 2019 in Senate:
wa kujenga laini nyingine lakini mpaka sasa, haijafanyika. Kwa hivyo, lazima tutafute njia za kujenga gatuzi za pwani. Matatizo mengi tunayopata kama changa moto za kiusalama, madawa ya kulevya, itikadi kali na ugaidi zote zinatokana na vijana kukosa kazi za kufanya katika Kaunti ya Mombasa. Tunaangalia kutoka Lamu hadi Lunga Lunga ambao ni ufuo wa bahari, tumetajiwa hapa kwamba mwaka jana tulikuwa na mkutano mkubwa wa mambo ya Blue Economy . Mpaka leo, hatujaona matunda ya mikutano kama hiyo.
view
9 Apr 2019 in Senate:
Katika eneo la bahari, kuna miradi mingi ambayo inaweza kufanyika ili kuhakikisha wananchi wanapata ruzuku na biashara ili kuhakikisha kwamba wanajenga nchi yao. Kwa sasa, tunaagiza samaki kutoka China wakati tuko na ufua mkubwa wa bahari ambao unaweza kutupa samaki wa kutosha ili wananchi wasife njaa na wasaidie katika sehemu zingine.
view