Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 171 to 180 of 1994.

  • 23 May 2024 in Senate: Bw. Naibu Spika, namsikiza ndugu yangu Sen. Wafula, lakini anazungumzia masuala ya moto na wazima moto. Kauli iliyoletwa Bungeni na Sen. Ali Roba ni kuhusiana na mafuriko na tabia nchini inavyoadhiri nchi zetu na zile za bonde la ufa. view
  • 22 May 2024 in Senate: Nataka kumsaidia Sen. (Dr.) Murango kwamba uhakiki inatokana na neno hakika. Kuhakiki na uhakika ni jambo moja. view
  • 22 May 2024 in Senate: Is it in order for my learned friend, Sen. Cherarkey, to refer to Sen.Tabitha Keroche as Sen. Tabitha Mutinda yet we know the two are different distinguished Senators in this House? view
  • 22 May 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa marekebisho ya sheria ya National Construction Authority yaani shirika linalosimamia ujenzi katika nchi yetu ya Kenya. Mabadiliko haya yako wazi na yatasaidia pakubwa kuchangia kina mama, vijana na pia walemavu kupata fursa ya kufanya biashara kama wanakandarasi nchini. Wanawake na vijana ndio asilimia kubwa ya idadi ya watu walioko nchini. Wengi wametengwa katika biashara na makazi kwa sababu uchumi wetu haujakuwa wa nguvu ili kuweza kumchukua kila mmoja. Mswada huu utatoa fursa ya kuwezesha wao kufanya biashara ili waweze kujikimu na pia waajiri watu wengine ambao watafanya kazi katika ... view
  • 22 May 2024 in Senate: Pia Serikali ya kitaifa hailipi pesa kwa wakati. Kwa hivyo, hata wakifanya biashara zile hawapati malipo ama faida kama vile inatarajiwa katika kufanya biashara hiyo. Wengi ambao wanaanzisha biashara wanapata changamoto nyingi hususan changamoto za raslimali yaani mtaji wa biashara ile. Utapata hata kama amepewa kandarasi, inataka alipie mali ghafi ama vitu ambazo atatumia kwenye ujenzi ama kupeleka kwenye biashara. Hivyo basi wanakosa kufanya biashara hizo kwa sababu ya pesa hizi ama mtaji raslimali inayohitajika kuanzisha biashara hizo. Vile vile Mswada huu unapendekeza kuwa wale ambao fee haizidi shilingi 15,000 waruhusiwe kufanya maombi hayo bila kulipa. Mswada huu utasaidia pakubwa ... view
  • 22 May 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa mazao ya nuts and oil crops . Mimea ya mafuta kama vile korosho, nazi, macadamia na mingine hupandwa kwa nia ya kuzalisha mafuta. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate. view
  • 22 May 2024 in Senate: Nampongeza Sen. Kibwana kwa kuweza kuudhamini Mswada huu kwa sababu utasaidia pakubwa kuinua mazao haya ya nazi pamoja na korosho katika kaunti za pwani ambapo mazao haya yanakuzwa kwa wingi. Kwa mfano, mazao ya nazi na korosho yanafanya vizuri sana katika kaunti za Kwale, Mombasa, Kilifi, Tana River na Lamu. view
  • 22 May 2024 in Senate: Ukosefu wa sheria kama hii kwa miaka mingi imefanya mazao haya yatupiliwe mbali na wananchi wanapata shida. Kifungu cha pili kinasema kwamba mazao haya ni pamoja na nazi, korosho, macadamia, njugu, sunflowe r, jojoba, simsim, bambara na mengineo mengi yatakayo tangazwa katika gazeti rasmi na Waziri wa Kilimo. view
  • 22 May 2024 in Senate: Zamani kulikuwa na sheria ambayo ilikuwa inatoa mazao yote kwa jumla; Agriculture and Food Authority (AFA) . Lakini sheria hii ilipatikana kukusanya mazao yote ya biashara na chakula pamoja na ikawa vigumu kupata uangalizi wa kimaada kwa yale mazao mbalimbali. Hivyo ndivyo basi kukakuwa na sheria kutoka 2017/2018 ambayo ilikuja na wazo kuwa kila zao liwe na sheria yake. Ndio maana sasa kuna sheria ya kahawa, chai, ukuzaji miwa na sukari. Mazao haya yote yameweka chini ya heria mbalimbali. Hii ni kwa sababu kila zao linatiliwa mkazo kivyake. view
  • 22 May 2024 in Senate: Ile sheria ya AFA haikusaidia ukuzaji wa ukulima. Kwa mfano, zao la pareto au view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus