Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 181 to 190 of 1994.

  • 22 May 2024 in Senate: liliweza--- view
  • 22 May 2024 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ninachangia Mswada huu wa Sen. Kibwana na yeye yuko mstari wa mbele akisikiliza mchango wangu. view
  • 22 May 2024 in Senate: Bw. Spika wa Muda, zao la pareto lilikuwa linafanya vizuri sana. Hata hivyo, liliunganishwa na mazao mengine katika sheria ya AFA, na karibu ukulima wake kufa. Ninafikiri kuwa katika Kaunti ya Nakuru ambapo lilikuzwa kwa wingi halipo sasa. Kwanza kabisa kupea mazao haya sheria zao husika itasaidia pakubwa kuinua tena ukuuzaji na uuzaji wa mazao mbalimbali. view
  • 22 May 2024 in Senate: Jambo la pili ni kwamba kumekuwa na ukosefu wa utafiti wa mazao kama haya. Kule pwani ukipanda mnazi leo ni lazima ungojee miaka kumi ili upate zao la nazi. Siku hizi kuna variety ya mbegu zinazotoka kule Vietnam ambazo zinafanya mti wa nazi uwe tayari kwa muda wa miaka mitatu na unazaa karibu nazi 400 kwa kila zao. Utafiti ukifanyika utasaidia kuleta miti ambayo itakuwa inazaa kwa muda mdogo na pia kuongeza yale mazao ili wakulima wapate faida. view
  • 22 May 2024 in Senate: Zao la korosho linafanya vizuri sana katika kaunti ya Kilifi, Kwale, Lamu na sehemu ya mpeketoni. Zao hili litafanya vizuri zaidi kama kutakuwa na utafiti wa mbegu zitakazoweza kuzaa kwa muda mfupi na kuongeza mazao ya wakulima. Hivi majuzi, nimelezwa kuwa, kulikuwa na mbegu nyingi za zao la korosho kule Kenya Agricultural and Livestock Research Organization (KALRO) Mtwapa. Gavana wa Tharaka Nithi, Mhe. Njuki, alizinunua zote. Hivi sasa, nasikia zao hili limeanza kufanya vizuri sana katika kaunti za Tharaka na Makueni ambako lilinaweza kukuzwa. Jambo la kusikitisha ni kwamba; kaunti zetu za pwani hazijawekeza kwa zao hili. Kwa mfano, hapo ... view
  • 22 May 2024 in Senate: na pia kujiendeleza kimaisha. Lakini, mtambo ulipofungwa na kuuzwa, mpaka hivi sasa, wakulima wametatizika. Kwa muda wa miaka 10, Serikali ya Kaunti ya Kilifi haikuweza kuekeza pesa kununua mtambo ule ili iwe ni raslimali yao. Kwa hivyo, kaunti zetu hazijawekeza katika mazao haya na ukulima kwa jumla. Ukiangalia bajeti za kaunti ya Lamu, Mombasa, Kwale, Kilifi na Taveta Taita, ni asilimia ndogo sana ambayo tunaekeza katika ukulima. Ilhali, mazao haya yana uwezo ya kuwanasua watu wetu kutoka lindi la umaskini na ukosefu wa pesa. Bw. Spika wa Muda, Kifungu cha 22 cha Mswada huu kinasema kwamba kaunti zitatunga sheria kuhusiana ... view
  • 22 May 2024 in Senate: Nazi nazi yenyewe inaweza pikwa, kukaushwa na ikafanywa mafuta. Hata kama siwezi kwenda katika kiwanda kikubwa, viwanda vidogo vya kukamua mafuta vinaweza kuchangia pakubwa kuinua hali ya nazi na maisha ya watu wa pwani. Kama alivyosema Sen. Hamida; hupotezi chochote kwa nazi kwa sababu makuti inaweza kutumika kufunika paa la nyumba yako. Hata kama kuna joto, huwezi kuihisi ukiwa na paa la makuti. Unaweza kupata kamba kutoka kwa makumbi ya nazi. Pia unaweza kutengeneza godoro kutoka kwa zao ya nazi. Nazi ina faida nyingi sana kwa watu wetu. Kwa hivyo, sheria hii itasaidia pakubwa. Pia naona majukumu ya kaunti zetu ... view
  • 22 May 2024 in Senate: Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. I wish to second the report of the Standing Committee on Finance and Budget of the Senate regarding the adoption of the report of the Status of Implementation of Projects Funded by the Conditional Grant for Construction of the County Headquarters in Nyandarua, Isiolo, Tharaka-Nithi, Lamu and Tana River counties. The committee held extensive negotiations with the concerned counties. Four of them were very cooperative, except Tana River County, where the Governor, despite being-invited on three occasions, failed to honour the invitations. However, we proceeded to consider the matter without their input. We got ... view
  • 21 May 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa hii kuhusu Siku ya Kimataifa ya Chai iliyoletwa Bungeni na Sen. Cherarkey. Mombasa ndio soko kubwa kabisa la chai ulimwenguni. Ni faraja kubwa kwa watu wa Mombasa kwamba kwa miaka mingi sasa, wamekuwa wenyeji wa soko la chai ulimwenguni. Sio chai ya Kenya pekee ambayo inauzwa katika soko la chai la Mombasa. Kuna chai kutoka Burundi, Rwanda, Tanzania na sehemu nyingi ambapo chai hizo huchanganywa na chai ya Kenya – kwa sababu chai ya Kenya ni bora zaidi – ili kuboresha chai zingine ambazo zinauzwa ulimwenguni. view
  • 21 May 2024 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus