21 May 2024 in Senate:
Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi karibuni kumekuwa na hujuma ya soko la chai katika Kaunti ya Mombasa. Hujuma hizo zimechangia mataifa mengine kufungua masoko yao ya chai. Kwa mfano, nchi ya Tanzania imefungua mnada wao wa chai. Chai yao haiji tena Kenya kwa sababu ya masuala kama haya ambayo ninayazungumzia. Tunapozungumzia jinsi ya kusaidia kuinua uchumi wa chai, ni lazima tuangalie pande zote mbili. Chai bila soko haitaweza kusaidia mkulima. Lazima chai ipate soko bora ambayo itaweza kumsaidia mkulima na yule ambaye anauza chai hiyo. Hapa katikati kuna Shirika la Kenya Tea Development Agency (KTDA). Juzi tulikuwa na mkutano ...
view
21 May 2024 in Senate:
Bw. Naibu wa Spika, ningetaka kuuliza kama ni haki kwa Sen. Mundigi kusimama ndani ya Bunge hili kutia sherehe kwa mmea ambao kulingana na Narcotic Drugs and Psychotropic Substances Control Act, ni dawa ya kulevya? Inahusiana na dawa ya kulevya. Na hata hapa Bungeni---
view
21 May 2024 in Senate:
Sen. Munyi Mundigi anapotosha taifa kwamba ni mmea ambao unafaa watu. Hii ni kwa sababu, mihadarati imepigwa marufuku kuambatana na Narcotic Drugs and Psychotropic Substances Control Act . Huu muguka---
view
21 May 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu kuhusu uhusiano wa Bunge zetu mbili. Naona Naibu wa Kiongozi wa upande wangu ana ghadhabu kidogo. Anataka nichukue dakika chache.
view
21 May 2024 in Senate:
Kwanza kabisa, Bw. Spika wa Muda, ningependa kuipongeza Kamati yako ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu kwa kupendekeza kwamba Seneti ikatae Mswada huu. Najua kwamba katika kamati yako, kuna Maseneta wenye tajriba kubwa. Kuna mawakili ambao wamesoma na kushauri Bunge hili kwamba Mswada huu hauna nia njema kwa Seneti.
view
21 May 2024 in Senate:
Ningependa kuchangia mambo matatu ili nimpe nafasi Sen. Wambua azungumze kabla ya kikao hiki kukamilika wakati utakapofika.
view
21 May 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
21 May 2024 in Senate:
Kwanza kabisa, Mswada huu ulichapishwa kinyume na Kifungu cha 113 cha Katiba yetu. Kabla ya kuchapishwa, Mswada huu haukupelekwa kwa Spika wa Seneti ili kuuidhinisha kama anakubali kuwa hauathiri kaunti. Hii ni mojawapo ya taratibu ambazo zinazingatiwa na Katiba kuhusiana na Miswada ambayo inapelekwa katika Mabunge yote. Itakumbukwa kwamba mwaka wa 2019, Seneti ilikwenda mahakamani, Mahakama ikabatilisha karibu sheria 25 ambazo zilikuwa zimepitishwa na Bunge la Taifa bila kuletwa katika Seneti. Kwa vile Mswada huu unaathiri Seneti na ulichapishwa, ukajadiliwa na kupitishwa katika Bunge la Taifa bila Spika wa Seneti kuuidhinisha, hiyo ni kinyume na Katiba. Hilo ni jambo la ...
view
21 May 2024 in Senate:
Jambo la pili ni kuwa Mswada huu unakiuka Katiba. Kuna maamuzi mengi ya mahakama ambayo yanasema kwamba ni kinyume na Katiba sheria kupitishwa na Bunge la Taifa bila kuhusisha Spika wa Seneti. Ikifanyika, sheria hiyo inafaa kubatilishwa. Maamuzi hayo yote yanasema kwamba lazima ushauri upatikane kutoka kwa Seneti kama Mswada unaathiri kaunti au la.
view
21 May 2024 in Senate:
Jambo la tatu ni kuhusiana na swali la uhusishaji wa umma, yani public
view