27 Mar 2018 in Senate:
Yes, Mr. Deputy Speaker, Sir, it is fine with me.
view
21 Mar 2018 in Senate:
Asante, Bwana Spika wa muda. Ripoti iko sawa isipokuwa mapendekezo yake ndio yalikuwa yanatatiza waheshimiwa Maseneta. Ripoti hii inaeleza kwamba wa kwanza katika majadiliano alikuwa ni Sen. Isack Kipkemboi Melly ambaye alipata alama 78. Ripoti hii inatilia maanani uzoefu wake wa awali. Kwa kizungu inaitwa
view
21 Mar 2018 in Senate:
Kwa Kiswahili tunasema ‘uzoefu wa awali.’ Kwa hivyo, uzoefu wake wa awali ulitiliwa maanani kwamba alikuwa amefanya kazi kama msimamizai wa maswala ya wanafunzi katika chuo kikuu na pia amekuwa Seneta kwa wa miaka mitano. Ijapokuwa ripoti inasema kuwa ana uzoefu wa awali wa miaka kumi kwa mambo ya fedha ilivyotakikana na Section 5 (2) (b), aliweza kuwashinda wenzake kwa alama tatu. Kwa hivyo, inaonekana kwamba huyu ni mwerevu. Tunaweza kumuita kwa kiingereza genius kulingana na mahojiano yaliyofanyika. Bwana, Spika wa muda, naunga mkono kwamba tubadilishe majina ya Sen. Isack Kipkemboi Melly na Bi. Margaret Sawe wakubaliwe kama washindani kwa ...
view
15 Mar 2018 in Senate:
Asante sana, Bwana Spika. Swala la SGR ni nyeti sana kwa sababu linaathiri watu kutoka Mombasa mpaka labda Naivasha wakati itakamilika. Ijapokuwa SGR kwa sasa inafanya kazi, kuna baadhi ya watu ambao wameathirika kutoka sehemu ya Mombasa 001 mpaka 020 ambao hawajalipwa ridhaa kwa ardhi zao zilizochukuliwa kwa maswala ya SGR. Vile vile, kuna sehemu ya baharini kule Eneo Bunge la Changamwe ambapo mikoko na miti mingine ya thamani imeharibiwa na mpaka sasa, hakujakuwa na njia yoyote ya kurekebisha madhara kama yale ambayo yametokea kwa mazingira. Kwa hivyo, ninaunga mkono Petition ya watu wa Kajiado. Imekuja kwa wakati mwafaka kwa ...
view
15 Mar 2018 in Senate:
Asante Bw. Spika. Neno ‘ halumbe’ ambalo Mhe. Seneta wa Makueni amelizungumzia ni ‘Halambe’ kwa lugha ya Kigiriama. Jina la Kiswahili hasa ni ‘halambe.’ Kama alivyotangulia kusema maana ya ‘halambe’ ni kuvuta pamoja. Harambee ilikuja kwa sababu ya matamshi. Kwa mfano, dada yangu pale, Sen. Kihika, anaweza kusema ‘hera’ badala ya ‘hela.’
view
15 Mar 2018 in Senate:
Bw. Spika, neno ‘Harambee’ linalotumika katika Coat of Arms halihusiani kamwe na ‘ambe’ambaye anasemekana ni Mungu katika sehemu zingine za dunia. Kwa hivyo nakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Haki, Maswala ya Sheria na Haki za Kibinadamu, kwamba ombi la ndugu Aluoch Polo Aluochier halina msingi na linafaa kutupiliwa mbali. Asante.
view
14 Mar 2018 in Senate:

13 Mar 2018 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I requested for a statement but the response has not been given to me.
view