8 Aug 2023 in Senate:
Wamesema kumekuwa na vita Ukraine, lakini vita vya Ukraine vimekuwepo sasa zaidi ya mwaka. Vita vya Ukraine vilianza February mwaka uliopita kwa hivyo kwa sasa haviwezi vikawa ni nyenzo inayochangia kupungua kwa dhamani ya sarafu ya Kenya.
view
8 Aug 2023 in Senate:
Kipengee cha 211 ya Katiba yetu kinaipa Bunge hili fursa ya kutunga sheria zinazoangalia maswala ya kukopa na pia kuweka wazi sheria ambayo itamruhusu Waziri wa Fedha kuweza kutoa ripoti kwa Bunge. Nikizungumzia Bunge nazungumzia Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa. Huu Mswada unapotaka kupunguza hii fursa ya kuleta ripoti, ukipelekwa kwa Bunge la Kitaifa pekee yake, ina maana wanakiuka Katiba katika kipengee cha 211.
view
8 Aug 2023 in Senate:
Tukiangalia baadhi ya marekebisho kama vile 2(b) (c) (d) na (e), zote zinasema kwamba Waziri wa Fedha atapeleka ripoti katika Bunge la Kitaifa kabla ya tarehe 30th mwezi wa nne, kila mwaka. Ina maana ile nafasi ya kuripoti itakuwa haiji tena katika Bunge la Seneti. Itakuwa inapelekwa kwa Bunge la Kitaifa pekee yake na hiyo itakuwa inakiuka Katiba katika kipengee cha 211. Kipengee cha 211(b) inasema katika muda wa siku saba baada ya kauli kutoka kwa Bunge lolote yaani Bunge la Kitaifa au la Seneti, Waziri anaweza kuitwa akaeleza ripoti ya mikopo iliyochukuliwa na vile pesa zimetumika katika mikopo hiyo. ...
view
8 Aug 2023 in Senate:
Iwapo sheria hii itapita inamaanisha kwamba deni letu litakuwa limekwenda zaidi ya asilimia 55 ambalo limependekezwa katika Mswada huu. Tukibadilisha, Waziri husika atakuwa na muda wa miaka mitano. Kwa maoni yangu, miaka mitano ni mingi kwa sababu kila mwaka Seneti na Bunge la Taifa hujadili
view
8 Aug 2023 in Senate:
(BPS) ambapo Serikali inatoa mapendekezo ya jinsi ya kupunguza madeni kwa muda mfupi na baada ya muda mrefu. Mwaka ujao, Mwezi wa tatu au wa nne, tutakuwa tunajadili kuhusu BPS. Tutajadili kuhusu mapendekezo yatakayotolewa na iwapo yatasaidia kupunguza madeni
view
8 Aug 2023 in Senate:
kutoka asilimia 64 hadi asilimia 55 ambayo inapendekezwa katika Mswada huu. Hatuna shida na kubadilishwa kwa mfumo wa deni kutoka Kshs10 trillioni hadi asilimia 55 ya
view
8 Aug 2023 in Senate:
. Serikali karibu inapita kiwango cha Kshs10 trillioni. Kwa hivyo, mabadiliko haya hayataipa Serikali afueni kwa sababu tayari wamevuka mpaka unaofaa wa Kshs10 trillioni hadi asilimia 55 ya GDP . Kuna haja ya Serikali kupewa muda. Muda huo unafaa kupendekezwa na Bunge. Kulingana nami, unafaa kuwa muda wa miaka mitatu. Vipengee vingine ambavyo vinaleta shida ni 2(b) na (c) ambavyo vinasema kwamba Waziri anaweza kukiuka kiwango hicho cha asilimia 55 na baadaye kuleta ripoti Bungeni ili kukubaliwa kufanya hivyo. Hatuwezi kama Bunge kukataa wajibu wetu wa kutunga sheria. Vipengee hivi vikipita ina maana kwamba Serikali itakuwa na freehand or blank
view
8 Aug 2023 in Senate:
ya kuongeza kiwango cha deni kulingana na jinsi wanavyotaka kisha baadaye watuambie kuwa waliongeza kwa sababu ya jua kali, uvamizi wa mashamba na nzige katika sehemu fulani au kwa sababu hakukuwa na hiki au kile nchini. Hatutaki Kipengee 2(c) kwa sababu itanyima Seneti na Bunge la Taifa nafasi ya kuhoji jinsi pesa zitakavyotumika. Ni bora Waziri aje katika Bunge na kusema anataka kuongeza deni kwa sababu fulani kisha Bunge likubali au likatae kuliko atumie pesa halafu baadaye aje aseme aliongeza deni kwa sababu, kwa mfano, alijenga makazi mapya ya Rais au Naibu wa Rais, au waliongeza Chief Administrative Secretaries (CASs) ...
view
8 Aug 2023 in Senate:
La, Bw. Spika wa Muda. Nimesema kwamba iwe ofisi huru. Yani
view
8 Aug 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ofisi ya kudhibiti madeni ni muhimu sana. Kwa hivyo, haifai kuwa Idara katika Ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango katika nchi yetu. Kuna madeni ya Serikali ya kitaifa na serikali za kaunti ambazo zinatambulika kikatiba. Kuna serikali za kaunti ambazo ziko tayari kukopa kulingana na fedha wanazopata. Mapato yao yanawawezesha kukopa ili kutekeleza mipango yao kwa haraka na kuendeleza maendeleo kisha walipie pole pole kulingana na uwezo wa kaunti zao.
view