8 Aug 2023 in Senate:
Hapa tunazungumzia madeni ya Serikali ya kitaifa pekee. Serikali za kaunti zikitaka kukopa, wanaambiwa kuwa hawana uwezo au wasubiri. Mara nyingi, Wizara ya Fedha na Mipango haiko tayari ku-guarantee kwamba serikali za kaunti zinaweza kukopa. Ipo haja ya kugawanywa madeni ili serikali za kaunti ziweze kukopa kiwango fulani na kiasi fulani kiwe cha Serikali ya kitaifa. Kwa mfano, Serikali kuu inaweza kukopa asilimia 70 na serikali za kaunti zikope asimilia 30 ya 55; au iwe asilimia 60 kwa 40. Hiyo itakuwa bora kwa sababu kwa sasa hatujui jinsi serikali za kaunti zinaweza kukopa kwa kuwa ni kama ni lazima wale ...
view
2 Aug 2023 in Senate:
Asante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Statement mbili ambazo zimeletwa Bungeni; moja ya Lake Victoria na nyingine ya matatizo ya akili, yani
view
2 Aug 2023 in Senate:
na maswala ya madhara ya mental hospital . Nikianzia hii ya pili ni kwamba ni ukweli matatizo ya afya ya akili imekuwa kidonda sugu. Utapata kwamba kama Maseneta waliotangulia walivyosema, vituo vya matibabu katika Kenya viko viwili pekee yake: Mathari na Port Reitz katika Kaunti ya Mombasa. Lakini hakujakuwa na uwekezaji wa kutosha katika taasisi hizi kiasi ambacho wengi wanaoenda pale wanateseka baadala ya kuangaliwa na madaktari ama wauguzi walio katika hospitali zile. Bw. Spika, tatizo kubwa pia ni kuwa kuna unyanyapaa katika familia za wale ambao wameathirika kwa sababu mtu wa akili pungwani mara nyingi huwa hausishwi kwa jambo ...
view
2 Aug 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
2 Aug 2023 in Senate:
Reitz, iangalie kwa makini ni vipi watu wale wanaangaliwa kwa sababu matatizo ya akili sasa yameingia katika kila jamii ya Kenya. Vile vile, maswala ya mazingira ni muhimu sana. Kule Mombasa tumeona uchafuzi wa mazingira umeingia katika Bahari la Hindi. Ukienda katika ufuo wa bahari, kwa mfano, ukitoka Nyali Bridge ya zamani uzunguke mpaka Statehouse, utapata uchafuzi wa mazingira umekithiri sana. Utapata kwingine hata maji machafu yanayotoka kwenye nyumba zetu yanaingia moja kwa moja katika bahari ambapo yanaharibu mazingira ya samaki kutaga mayai na pia kuzaana. Vile vile, wale samaki watakapovuliwa hawatakuwa halali kuliwa na binadamu kwa sababu mazingira yao ...
view
2 Aug 2023 in Senate:
inamaanisha kwamba samaki akila takataka zile, zikiingia katika mwili wake, baadaye tukikkula wale samaki, tutakuwa tunadhuru afya yetu. Ndio maana visa vingi vya saratani ya mwili vinatokana na mazingira na kukula vyakula vinavyoathiriwa na mazingira kama hayo. Bw. Spika, ningependa pia Kamati ya Mazingira itakapokuwa inaangalia swala hili, pia wazuru Mombasa kwa sababu ile mchafuko inayoendelea katika Bahari Hindi yanaathiri pakubwa uzalishaji wa samaki, uvuvi na maisha yetu sisi katika eneo la pwani. Asante kwa kunipa fursa hii.
view
2 Aug 2023 in Senate:
Yes, I want to inform my colleague, the Majority Leader, that Kenya Breweries Limited still supports Kenya Breweries Football Club. I thank you.
view
1 Aug 2023 in Senate:
Bw. Spika, nasimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu No. 53(1), kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Barabara, Uchukuzi na Makao kuhusu kuzorota kwa miundombinu na huduma katika Jengo la Bima Towers katika Kaunti ya Mombasa. Katika Taarifa hiyo, kamati inafaa kuchunguza na kuripoti katika Seneti-
view
1 Aug 2023 in Senate:
(1) sababu zilizopelekea lifti katika jengo hilo kutofanya kazi kwa muda wa zaidi ya miaka miwili pamoja na ukosefu wa huduma za maji safi katika jengo hilo, ikizingatiwa kwamba jumba hilo lina ofisi mbalimbali za Serikali ya Kaunti ya Mombasa na Serikali Kuu, ambapo mamia ya watu huzuru kila siku kutafuta huduma za dharura katika ofisi hizo; na,
view
1 Aug 2023 in Senate:
(2) iarifu Seneti chanzo cha utepetevu katika usimamizi ikizingatiwa kwamba jengo hilo lilikabidhiwa serikali kipindi kifupi kilichopita.
view