Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 481 to 490 of 1995.

  • 1 Aug 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. view
  • 1 Aug 2023 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nichangia Hoja ya kuongezewa muda kwa Kamati ya Muda inayo chunguza mashaka kule Shakahola. Kwanza, nampongeza Mwenyekiti wa Kamati hii na wanachama wake wote nikiwa mmoja wao kwa kazi nzuri ambayo wamefanya mpaka sasa. Tumeweza kuzuru maeneo ya Shakahola mara mbili na tukaona hali ilivyokuwa kule. Tulipozuru sehemu za makaburi, tulipata mwili mmoja ambao ulikuwa umepatikana na ukawa unapelekwa katika hifadhi ya maiti kule Malindi. Kazi iliyofanyika ni kubwa, lakini kazi iliyobaki ni kubwa pia. Hii ni kwa sababu mpaka sasa, hatujaweza kujua kama makaburi ambayo bado yana watu yamekwisha ... view
  • 1 Aug 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 1 Aug 2023 in Senate: Vile vile, kazi ya kutafuta Deoxyribonucleic Acid (DNA) pia ina changamoto kwa sababu hatuna vifaa vya kupima DNA hapa. Mpaka, ziwasilishwe Afrika Kusini ambako pia inachukuwa muda kuweza kuwatambua wale waliofariki na jamaa zao tofauti tofauti. Wengi ambao walienda kule Shakahola walibadili majina yao. Kama unaitwa Mohamed Faki, kule unajiita jina lingine ambalo hata kama umeweza kupatikana, jina lako na stakabadhi zako zinaonyesha majina tofauti na yale ambayo ulikuwa unajulikana nayo. Kwa hivyo, imekuwa ni vigumu kabisa kuweza kuwatambua watu wale na kuwaunganisha na familia zao ili waweze kuzikwa. Bw. Spika wa Muda, muda uliyokuwa umepeanwa ni miezi mitatu lakini ... view
  • 1 Aug 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 1 Aug 2023 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ni swala ambalo linaibuka na pia ningependa Mwenyekiti, aliangalie swala hilo wakati tutakapo ongezewa muda kwa sababu ni tatizo ambalo litahujumu sheria zetu za kuhusu haki za kibinadamu. Nikimalizia, leo tukiwa katika chakula za mchana, tulikuwa na Seneta wa Kaunti ya Bungoma. Yeye pia alinieleza kwamba majuzi, kuna watu kama hao wamepatikana Nakuru. Walikuwa wanaelekea sehemu za Ethiopia kuenda kwa maswala kama haya ya Shakahola. Ni mambo ambayo bado yako, dini kama hizi bado ziko na fikra kama hizi bado ziko. Kwa hivyo, inafaa tuweze kumaliza swala hili na tuliangalie vizuri ili kuwe na msingi wa ... view
  • 25 Jul 2023 in Senate: Bw. Spika, nimesimama kuambatana na Kifungu cha 52 (1), cha Kanuni za Kudumu za Seneti kutoa Kauli kuhusu siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili iliyoadhimishwa mnamo Tarehe 7 Julai, 2023. Bw. Spika, Kiswahili ni Lugha ambayo inatumiwa na kuzungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 katika Bara la Afrika. Hii ndiyo lugha inayokuwa na kusambaa kwa kasi zaidi ulimwenguni, ikizingatiwa kuwa mataifa ya Uchina na Japan yameanza kufunza lugha hii nchini mwao. Afrika Kusini pia ni taifa ambalo lugha hii imeanza kufunzwa. Moja ya maazimio ya Umoja wa Afrika ni kwamba siku moja lugha yetu hii ndiyo itakayo kuwa ... view
  • 25 Jul 2023 in Senate: Nchini Kenya, sherehe hizi ziliadhimishwa na jamii ya Waswahili katika eneo la Mama Ngina Water Front, Kaunti ya Mombasa. Maeneo haya ni baadhi ya turathi za Waswahili na mahali hapa tangu zamani palijulikana kama Mzimle. Bw. Spika, wakati maadhimisho haya yakifanyika, inapaswa tuzingatie hatua tulizopiga katika kuendeleza lugha ya Kiswahili. Hapa Seneti tumeweza kufasiri Kanuni zetu za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili lakini bado zipo hatua nyingi zinazofaa kupigwa ili tuwe na matumizi ya Kiswahili katika Seneti. Kwa mfano, bado hatuweza kufasiri Miswada ya Sheria, Ardhihali na ripoti za kamati kwa lugha ya Kiswahili. Hatua hii itasaidia pakubwa kuwapa ufahamu ... view
  • 25 Jul 2023 in Senate: Niko na nyingine ya feri. view
  • 25 Jul 2023 in Senate: Bw. Spika, nimesimama chini ya kifungu cha 52(1) cha Kanuni za Kudumu za Seneti kutoa Kauli kuhusu swala la kitaifa kuhusiana na kuzorota huduma za feri katika kivuko cha Likoni. Mheshimiwa Spika, kivuko cha Likoni kinaunganisha sehemu ya Pwani kusini na kisiwa cha Mombasa. Vile vile, kinaunganisha Kenya na Tanzania kupitia barabara ya Malindi-LungaLunga-Horohoro-Tanga-Bagamoyo. Barabara hii ni ya kimataifa. Kina umuhimu mkubwa kwa maisha ya wanabiashara, sio kwa kaunti za Mombasa na Kwale pekee, bali pia kwa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Hivi karibuni, huduma katika kivuko hicho zimedorora sana. Kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari na watu wanaotumia ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus