25 Jul 2023 in Senate:
Mheshimiwa Spika, hili daraja la miguu lilianzishwa 2020 na liligharimu Serikali karibu Kshs1.4 bilioni. Daraja ni jipya na halina sababu ya kurekebishwa kwa muda mrefu kama vile ilivyopangwa. Itakumbukwa kwamba, daraja la kuvukia kwa miguu kwa wasafiri wanaotembea kutoka Likoni hadi kisiwani lilizinduliwa wakati wa janga la Corona, ili kuondoa msongamano na kurahisisha usafiri. Kwa hivyo, kabla ya kulifunga daraja hili, ni muhimu kwa Halmashauri ya Bandari kuweka mikakati mbadala kupunguza msongamano katika kivuko cha Likoni. Kuna wawekezaji wanaomiliki vyombo vya usafiri baharini na ambao wako tayari kutoa huduma hizo katika kivuko cha Likoni, lakini Halmashauri ya Bandari imekataa kuwapa ...
view
18 Jul 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, nimemusikiza mweshimiwa Wafula kwa makini. Lakini Kenya hii inajulikana watu ambao walikula pesa ya mahindi na anayejulikana ni mmoja pekee yake hapa na hatuna haja ya kumtaja na kuna ushahidi. Asante.
view
18 Jul 2023 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia hoja ambayo imeletwa Bungeni na Seneta wa Embu, Sen. Munyi Mundigi. Kwanza kabisa, ninampongeza Seneta wa Kaunti ya Embu kwa kuleta Hoja hii alasiri ya leo. Mapema, alikuwa ameomba taarifa hapa kwa nini watu wake wamekosa mbolea ili waweze kupanda miti na wazalishe chakula kwa uzuri zaidi kwao. Pia, nilisikia kwa masikitiko mchango ulioletwa na Sen. Wafula, Seneta wa gatuzi la Bungoma, ambaye anawakilisha chama cha Ford Kenya katika Bunge hili. Chama ambacho ndio baba na mama wa upinzani katika nchi yetu ya Kenya. Hayati Masinde Muliro, hayati Kijana Wamalwa, ...
view
18 Jul 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
18 Jul 2023 in Senate:
za uchumi ambazo serikali hii ya Kenya kwisha inaendeleza katika nchi hii yetu ya Kenya.
view
18 Jul 2023 in Senate:
Bi Spika wa Muda, naomba unilinde.
view
18 Jul 2023 in Senate:
Bi Spika wa Muda, sikusema kwamba ni Serikali ya Kenya Kwisha. Nimesema Kenya Kwisha. Kuna tofauti ya Serikali ya Kenya Kwisha na neno Kenya kwisha. Mungenisikiza kwa makini kwa sababu mnataka kulifanya Bunge la Seneti kuwa kama yale mabaraza ya mitaa kule mnakotoka. Madam Temporary Speaker, polisi ndio chanzo kikubwa cha kutawanya na kukurupuka kwa maandamano katika nchi yetu ya Kenya. Kulingana na takwimu na vile vile mambo ambayo yalinipata mimi mwenyewe binafsi kama Seneta wa Mombasa. Tarehe kumi na mbili, jumatano iliyopita, tulikuwa tumetoa arifa ya kuandamana katika Kaunti ya Mombasa. Taarifa ilipelekwa mapema kwa polisi lakini polisi walikaa ...
view
18 Jul 2023 in Senate:
Bi Spika wa Muda, wajua Sen. Cherarkey tulimlea sisi hapa. Hata mimi ndiye nilimsaidia mpaka akaapishwa kama wakili. Heshima ni kitu muhimu. Yeye amekuwa nje ya Bunge, ameingia tu na kuanza kuruka na kusema kwamba mambo ya miraa hivi na vile. Zingine huwa sio hoja za nidhamu; ni mtu apate tu fursa ya kupiga kelele. Hakuna chochote kilichokosa nidhamu hapo. Nimesema kwamba, kuwekwe mashine ya kupima watu kama wamekula miraa ama mogoka. Hiyo haimaanishi tumetusi mtu yeyote. Kwa kumalizia, ni kwamba polisi ndio watu wa kwanza kuvuruga maandamano.
view
18 Jul 2023 in Senate:
Bi Spika wa Muda, tukiingia hapa kupitia huo mlango kila 2.30 alasiri, tunakaguliwa iwapo tuko na silaha. Hakuna anayebeba silaha hapa lakini tunaangaliwa silaha. Kwa hivyo, itakuwa sio makosa kwa wale ambao wanatoka sehemu zile ambazo wana vitu kama hivyo, waweze kupimwa kama wametumia ama hawajatumia. Kwa kumalizia ni kwamba polisi---
view
18 Jul 2023 in Senate:
Bi Spika wa Muda, bado dakika moja.
view