20 Jun 2023 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuongeza kauli yangu katika Mswada ambao umeletwa bungeni na Sen. Tabitha Mutinda. Bi. Spika wa Muda, Mswada huu wa maafisa wa nyanjani wa ukulima na ufugaji ni Mswada ambao utasaidia pakubwa kuongeza mazao katika sehemu ya ukulima na vile vile pia mazao katika sehemu ya ufungaji wa wanyama katika nchi yetu ya Kenya. Kwa sasa ijapokuwa huduma za ukulima na ufugaji zimegatuliwa, tukiangalia ile bajeti ambayo inatolewa katika nyanja hizo, katika kaunti zetu ni ndogo sana. Ni kiasi ambacho hakiwezi kufanya jambo lolote la kuweza kusaidia ukulima katika sehemu zile. Kwa ...
view
20 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Kuna mambo mengi sana ambayo tunaweza kuzungumzia lakini tunachunga muda. Mswada huu utachangia pakubwa kuongeza mapato ya wakulima na ya kaunti zetu. Vile vile, itazuia uagizaji wa chakula kama mchele, ngano na vinginevyo kutoka mataifa mengine. Bi. Spika wa Muda, hapo zamani, mchele mzuri kama Basmati ulikuwa unatoka Mwea. Kwa wale ambao wanakumbuka, kulikuwa na Mwea Pishori ambayo ilikuwa inauzwa mpaka soko za nje. Lakini hivi sasa, mchele wetu unatoka Pakistan kwa sababu ukulima wetu umezorota miaka nenda, miaka rudi. Ninaunga mkono Mswada huu.
view
13 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii. Nilikuwa na hofu kwamba nimefanyiwa hujma ili nisiweze kuzungumza. Lakini, nimeskia Kiongozi wa Waliowengi akipeleka malalamishi kwa Kamishna.
view
13 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
13 Jun 2023 in Senate:
Swala la marupurupu ya mahakimu ni swala nzito sana. Hii ni kwa sababu ndio watu ambao wameidhinishwa na Katiba kujaribu kutatua mizozo katika nchi yetu. Kwa hivyo, ikiwa hawatalipwa malipo ya kisawasawa pamoja na marupurupu ambayo wanatakikana kupata, basi hali yetu ya kupata haki itatatizika. Bw. Spika, mahakimu wengi wanafanya kazi nzuri katika nchi yetu. Vile, kuna mahakimu ambao ni watepetevu na hawatakelezi majukumu yao kisawasawa. Ijapokuwa kuna mfumo mpya wa wao kupeleka hesabu zao kila mwezi, tumeona kwamba imekuwa ni donda sugu katika sehemu ambazo ziko nje ya Mji wa Nairobi na miji mingine mikubwa. Bw. Spika, tumeona ijapokuwa ...
view
8 Jun 2023 in Senate:
Asante, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa Ugavi wa Raslimali kwa Kaunti zetu. Mgao wa Raslimali za Kaunti 2023 ni sheria muhimu ambayo inagawanya fedha zinazotoka kwa Serikali Kuu kwenda kwa serikali gatuzi. Bunge hili lilipitisha Mswada wa Division of Revenue Act (DORA) ambayo ilileta Kshs385.425 billioni, kutoka kwa Serikali Kuu Kwenda kwa serikali za kaunti. Ijapokuwa sheria hii ilipita shingo upande, ndio sheria ambayo iko. Kwa hivyo, sheria ambayo tunaijadili kwa sasa, imeundwa ikizingatia kwamba pesa zitakozota kutoka Serikali kuu kuja kwa serikali za kaunti ni Kshs385.425 billion. Ugavi wa rasilimali hii umezingatia mfumo wa ...
view
8 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
8 Jun 2023 in Senate:
asilimia 10; ukubwa wa ardhi, asilimia nane; ukulima, asilimia 10; afya, asilimia 17, barabara, asilimia nane; ukuaji wa miji, asilimia tano; na umaskini, asilimia 14. Katika kujadili wa Mswada huu, Kamati yetu ilipata fursa na kuchukua maoni kutoka kwa Baraza la Magavana, Wizara ya Fedha, Tume ya Ugavi wa Rasilimali na washikadau wengine. Vile vile, Kamati ilipata maombi kutoka kaunti 17 ambazo zilitaka kuongezwa pesa za msingi kutoka mwaka 2023/2024. Baadhi ya mambo yaliyozungumziwa na mabunge ya kaunti ni pamoja na maswala ya usalama katika kaunti zilizo mbali. Kwa mfano, Kaunti ya Mandera inagharamika pakubwa kupeleka usalama wanapofanya public participation ...
view
8 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, ningependa kumfahamisha ndugu yangu Seneta wa Elgeyo Marakwet, Sen. Kisang’ kwamba pesa ambazo tulipitisha kwa DORA ni Kshs385,425,000,000. Za maktaba haziko hapo. Waziri wa Fedha alipokuja katika Kamati yetu, alitaka kutuchanganya; alisema hizo Kshs425 milioni zilikuwa ni za kutoa huduma za maktaba ambazo zinatoka kwa Serikali Kuu zinakuja katika serikali za kaunti. Lakini, tukamwambia Kshs385,425,000,000 ndizo pesa ambazo zinakuja kama
view