8 Jun 2023 in Senate:
aani, pesa ambazo zinatoka kwa Serikali Kuu zinakuja kwa serikali za kaunti. Mwishowe alikubali kwamba hakuna Kshs425 milioni ambazo ni za maktaba. Watatafuta katika fedha zao zingine lakini katika zile za mgao wa kitaifa, ni Kshs385,425,000,000.
view
7 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii ili niweze kujiunga na wenzangu kutoa rambirambi zetu kwako, kwa Katibu wa Bunge na familia ya mwendazake, Bi. Marya Adjibodou. Bw. Spika, kwa hakika ni pigo kubwa, sio kwa familia yake peke bali pia kwa Bunge hili la Seneti. Bi. Marya alikuwa mfanyikazi ambaye alikuwa anafanya kazi yake kwa uangalifu zaidi na kwa haraka, iwapo atahitajika kufanya hivyo kwa haraka. Bw. Spika, nilimjua Bi. Marya kutoka mwaka wa 1980 tulipokuwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Alikuwa akisomea Bachelor of Arts na mimi nilikuwa nikisomea uanasheria. Nilimpata hapa nilipokuja kwa muhula wangu wa ...
view
7 Jun 2023 in Senate:
Mwenyezi Mungu alilaze roho yake pahali pema peponi. Asante.
view
6 Jun 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuongezea kauli yangu juu ya taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Cherarkey, Seneta wa Kaunti ya Nandi. Masaibu yanayokumba Wabunge wa Kaunti zetu ni ya kusikitisha. Ikikumbukwa kwamba ugatuzi ulikuja kuleta tofauti baina ya mabaraza ya miji yalikuwa yanahudumu wakati wa nyuma na mfumo mpya wa Serikali ambao unatumika katika nchi yetu ya Kenya.
view
6 Jun 2023 in Senate:
Marupurupu wanayopata ni machache sana kulingana na hali ya maisha ilivyo hususan kwa wale ambao wako katika miji mikubwa na miji midogo pia. Tukiangalia, kwa mfano, katika Kaunti ya Mombasa, Wabunge hawa wa Bunge la Kaunti ya Mombasa wanahitajika kupata ofisi na nyumba ambazo zinastahili hadhi yao. Nyumba hizi haziwezi kukodishwa bila pesa. Kwa hivyo, yale marupurupu wanayopata hayawawezeshi kukabiliana na maisha kisawasawa. Ndio mara nyingi, wanapatikana wakihujumu kazi zao kupitia kwa ile ruzuku ndogo ndogo wanazopata kutoka kwa wakuu wa kaunti.
view
6 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, ijapokuwa sheria ilibadilishwa na ikawa fedha za county assembly na fedha za county executive ziko mbalimbali, lakini bado utapata kwamba Waziri ama Mwanakamati ambaye anahusika na mambo ya fedha za kaunti husika anahujumu utendakazi wa Bunge la Kaunti kwa sababu pesa zinazokuja kutoka kwa mfuko wa Serikali kuu sio hizo ambazo zinakwenda katika kulipa mishahara au marupurupu ya MCAs.
view
6 Jun 2023 in Senate:
Kwa hivyo, kuna haja ya kubadilisha ama kurekebisha sheria ya fedha, yaani, Public Finance Management (PFM) Act kuhakikisha kwamba bunge la kaunti lina fedha zake mbali na zile fedha ambazo ziko katika serikali ya kaunti. Hii ni kwa sababu serikali ya kaunti mara nyingi wakiitisha pesa, wanapunguziwa ama wanatolewa pesa kidogo kidogo ili kuhakikisha kwamba kazi zao zinahujumiwa.
view
6 Jun 2023 in Senate:
Nakubaliana na wenzangu ambao wametoa kauli kwamba swala hili lizungumzwe na Bunge nzima; kauli nzima ya Bunge hili iweze kuzamia swala hili ili wabunge wetu wa county assembly waweze kupata marupurupu ya kisawa sawa. Vile vile, SRC wapewe onyo kwamba kupunguza marupurupu haya kunahujumu ugatuzi katika nchi yetu. Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii.
view
31 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu ya 53(1) kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa kuhusu kuchelewa kwa
view
31 May 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view