Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 551 to 560 of 1995.

  • 31 May 2023 in Senate: kuchapishwa kwa paspoti nchini ambako kunaathiri mipango ya safari ya mahujaji wanaokwenda Makkah nchini Saudi Arabia kwa ibada yao ya Hajj mwaka huu. Katika taarifa hiyo, Kamati iangazie yafuatayo- (1) Iiarifu Seneti chanzo cha ucheleweshaji wa usindikaji wa Paspoti katika Idara ya Uhamiaji, ikizingatia madhara na usumbufu unaoletwa na uchelewashaji huo kwa mahujaji wanaokwenda Makkah, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hajj katika mwezi Juni, 2023. Ibada ya Hajj inatarajiwa baadaye mwezi ujao kuanzia 20.06.2023. (2) Ieleze ni hatua gani Serikali inachukua kuharakisha usindikaji na uchapishaji wa pasipoti hizo ikizingatiwa kwamba mahujaji watalazimika kuvunja na kughairi safari zao iwapo jambo hilo ... view
  • 30 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kupeleka vikao vya Bunge la Seneti katika Kaunti ya Turkana. Bw. Spika, mji mkuu wa Turkana ni Lodwar ambao uko takriban kilomita 748 kutoka jiji la Nairobi. Safari ya Turkana ni ya siku mbili. Inabidi upumzike Kitale kama view
  • 30 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 30 May 2023 in Senate: unakwenda kwa gari kama walalahoi au “mahustlers” wengi. Baaadaye, siku ya pili uendelee na safari mpaka Lodwar. Bw. Spika, hii itatoa fursa kubwa kwa Bunge la Seneti kusoma maeneo ya Turkana na maeneo jirani. Vile vile, itatoa fursa kwa watu wa Turkana kusoma Bunge lao linafanya kazi namna gani. Itakuwa ni fursa ya Bunge la Kaunti ya Turkana kupata fursa ya kuona vikao vya Seneti na vile kamati tofauti tofauti za Seneti zinavyofanya kazi. Kamati hizi ama mabunge haya ya kaunti, mara nyingi huwa yamelema kikazi kwa sababu ya kutopata nafasi ya kusoma kutokana na vile kazi zinavyotendwa katika mabunge ... view
  • 25 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia ombi la taarifa kutoka kwa Seneta--- view
  • 25 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu wa Spika. Kabla sijachangia maombi ya Taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Hamida, ningependa kumkumbusha Sen. (Dr.) Khalwale kuwa hili ni Bunge. Mambo ya Bunge ni mambo ya Bunge na mambo ya Rais ni mambo ya Rais. Kwa hivyo, mambo ya Bunge lazima yazungumzwe Bungeni. Ningependa kuchangia Taarifa kuhusiana na kuachiliwa kwa wafungwa wanaotumikia vifungo vidogo vidogo gerezani. Ninawapongeza Maseneta wa Kenya Women Senators Association (KEWOSA) ambao juzi walizuru gereza la kina mama la Langata, ambapo waliwatoa takriban wafungwa 100. Wafungwa hao walikuwa wamefungwa kwa makosa madogo madogo. Bw. Naibu wa Spika, hii sio mara ya kwanza kwa ... view
  • 25 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 25 May 2023 in Senate: Tulitoa zaidi ya wafungwa 100 kutoka gereza lile. Baada ya hapo, Jaji Mutende aliyekuwa akihudumu katika kituo kile, alifanya ziara katika gereza lile, akaangalia zile faili za wafungwa wote waliokuwa na makossa madogo madogo, na wote wakaruhusiwa kwenda nyumbani. Ni kwa sababu ya kazi ambayo Bunge la Seneti lilikua limefanya. Bw. Naibu wa Spika, ni muhimu swala hili liangaliwe kwa undani. Tulipokuwa tunahudumu katika Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Binadamu, tulizuru gereza la Industrial Area. Hapo, wafungwa wanaishi katika hali ngumu sana, hususan wale walioko rumande wanaosubiri kesi zao zimalizwe ndio waende nyumbani. Hao wafungwa wanazuiliwa kwa dhamana ... view
  • 25 May 2023 in Senate: Bw. Naibu wa Spika, mkumbushe Sen. Gataya Mo Fire, hatuko Runyenjes hapa. view
  • 25 May 2023 in Senate: Magereza yetu yote yalijengwa kabla ya uhuru. Kwa muda wa takriban miaka 60, Kenya haijajenga gereza hata moja. Kwa hivyo, nafasi ni ndogo katika magereza yetu na wafungwa wengi wanapata shida. Kwa hivyo, jinsi ya kutatua msongomano katika jela zetu ni swala ambao lazima liangaliwe kwa undani zaidi. Wanaohukumiwa aghalabu wapate afueni kutokana na hali mbaya ya magereza yetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus