Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 591 to 600 of 2123.

  • 8 Aug 2023 in Senate: Tukiangalia baadhi ya marekebisho kama vile 2(b) (c) (d) na (e), zote zinasema kwamba Waziri wa Fedha atapeleka ripoti katika Bunge la Kitaifa kabla ya tarehe 30th mwezi wa nne, kila mwaka. Ina maana ile nafasi ya kuripoti itakuwa haiji tena katika Bunge la Seneti. Itakuwa inapelekwa kwa Bunge la Kitaifa pekee yake na hiyo itakuwa inakiuka Katiba katika kipengee cha 211. Kipengee cha 211(b) inasema katika muda wa siku saba baada ya kauli kutoka kwa Bunge lolote yaani Bunge la Kitaifa au la Seneti, Waziri anaweza kuitwa akaeleza ripoti ya mikopo iliyochukuliwa na vile pesa zimetumika katika mikopo hiyo. ... view
  • 8 Aug 2023 in Senate: Iwapo sheria hii itapita inamaanisha kwamba deni letu litakuwa limekwenda zaidi ya asilimia 55 ambalo limependekezwa katika Mswada huu. Tukibadilisha, Waziri husika atakuwa na muda wa miaka mitano. Kwa maoni yangu, miaka mitano ni mingi kwa sababu kila mwaka Seneti na Bunge la Taifa hujadili view
  • 8 Aug 2023 in Senate: (BPS) ambapo Serikali inatoa mapendekezo ya jinsi ya kupunguza madeni kwa muda mfupi na baada ya muda mrefu. Mwaka ujao, Mwezi wa tatu au wa nne, tutakuwa tunajadili kuhusu BPS. Tutajadili kuhusu mapendekezo yatakayotolewa na iwapo yatasaidia kupunguza madeni view
  • 8 Aug 2023 in Senate: kutoka asilimia 64 hadi asilimia 55 ambayo inapendekezwa katika Mswada huu. Hatuna shida na kubadilishwa kwa mfumo wa deni kutoka Kshs10 trillioni hadi asilimia 55 ya view
  • 8 Aug 2023 in Senate: . Serikali karibu inapita kiwango cha Kshs10 trillioni. Kwa hivyo, mabadiliko haya hayataipa Serikali afueni kwa sababu tayari wamevuka mpaka unaofaa wa Kshs10 trillioni hadi asilimia 55 ya GDP . Kuna haja ya Serikali kupewa muda. Muda huo unafaa kupendekezwa na Bunge. Kulingana nami, unafaa kuwa muda wa miaka mitatu. Vipengee vingine ambavyo vinaleta shida ni 2(b) na (c) ambavyo vinasema kwamba Waziri anaweza kukiuka kiwango hicho cha asilimia 55 na baadaye kuleta ripoti Bungeni ili kukubaliwa kufanya hivyo. Hatuwezi kama Bunge kukataa wajibu wetu wa kutunga sheria. Vipengee hivi vikipita ina maana kwamba Serikali itakuwa na freehand or blank view
  • 8 Aug 2023 in Senate: ya kuongeza kiwango cha deni kulingana na jinsi wanavyotaka kisha baadaye watuambie kuwa waliongeza kwa sababu ya jua kali, uvamizi wa mashamba na nzige katika sehemu fulani au kwa sababu hakukuwa na hiki au kile nchini. Hatutaki Kipengee 2(c) kwa sababu itanyima Seneti na Bunge la Taifa nafasi ya kuhoji jinsi pesa zitakavyotumika. Ni bora Waziri aje katika Bunge na kusema anataka kuongeza deni kwa sababu fulani kisha Bunge likubali au likatae kuliko atumie pesa halafu baadaye aje aseme aliongeza deni kwa sababu, kwa mfano, alijenga makazi mapya ya Rais au Naibu wa Rais, au waliongeza Chief Administrative Secretaries (CASs) ... view
  • 8 Aug 2023 in Senate: La, Bw. Spika wa Muda. Nimesema kwamba iwe ofisi huru. Yani view
  • 8 Aug 2023 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ofisi ya kudhibiti madeni ni muhimu sana. Kwa hivyo, haifai kuwa Idara katika Ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango katika nchi yetu. Kuna madeni ya Serikali ya kitaifa na serikali za kaunti ambazo zinatambulika kikatiba. Kuna serikali za kaunti ambazo ziko tayari kukopa kulingana na fedha wanazopata. Mapato yao yanawawezesha kukopa ili kutekeleza mipango yao kwa haraka na kuendeleza maendeleo kisha walipie pole pole kulingana na uwezo wa kaunti zao. view
  • 8 Aug 2023 in Senate: Hapa tunazungumzia madeni ya Serikali ya kitaifa pekee. Serikali za kaunti zikitaka kukopa, wanaambiwa kuwa hawana uwezo au wasubiri. Mara nyingi, Wizara ya Fedha na Mipango haiko tayari ku-guarantee kwamba serikali za kaunti zinaweza kukopa. Ipo haja ya kugawanywa madeni ili serikali za kaunti ziweze kukopa kiwango fulani na kiasi fulani kiwe cha Serikali ya kitaifa. Kwa mfano, Serikali kuu inaweza kukopa asilimia 70 na serikali za kaunti zikope asimilia 30 ya 55; au iwe asilimia 60 kwa 40. Hiyo itakuwa bora kwa sababu kwa sasa hatujui jinsi serikali za kaunti zinaweza kukopa kwa kuwa ni kama ni lazima wale ... view
  • 2 Aug 2023 in Senate: Asante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Statement mbili ambazo zimeletwa Bungeni; moja ya Lake Victoria na nyingine ya matatizo ya akili, yani view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus