12 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada ambao umeletwa Bungeni na Sen. Mungatana, MGH, Seneta wa Kaunti ya Tana River, kule ambako mamba wanashindana na wananchi kwa huduma za maji. Mswada huu ni muhimu sana ikizingatiwa kwamba Katiba yetu ya mwaka 2010 iliweka bayana haki za jamii - social rights na haki za kiuchumi - economic rights . Kifungu cha 43 cha Katika ya Kenya kinatoa wazi haki hizo, zikiwemo haki ya afya bora pamoja na haki za kimsingi za kuzaa, haki ya kuwa na nyumba ama makaazi ya kuishi, haki ya kuwa na hali ya juu ...
view
12 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, tukiangalia wakulima, hivi majuzi Serikali ilileta mfumo wa kuleta mbolea. Ijapokuwa ni jambo nzuri, ni jambo la kushangaza kwamba Serikali yetu imetoka hapa mpaka nchi ya Zambia kuenda kuwasaidia wakulima nchini humo kuzalisha mahindi mengi ili walete Kenya wakati hatujaweza kuwahudumia wakulima wetu kikamilifu. Badala ya kuwa na vipimo vya kupima Zambia, tutaleta mahindi ama tutaleta mazao kiasi gani, tuwe na vipimo vyetu hapa Kenya ili kuona kwamba wakulima wetu wote wanazalisha chakula cha kutosha ili kulisha nchi yetu ya Kenya. Katika maswala ya maji, kunajengwa mabwawa kila mara lakini tatizo sugu la maji bado halijatatuliwa. Kwa ...
view
12 Apr 2023 in Senate:
Ndio, Bw. Naibu Spika.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Kwa Kiingereza, tunaweza kusema ni puppets wa Serikali zilizoko. Na hii haikuanza sasa---.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Samahani, Bw. Naibu Spika, kama umeielewa hivyo. Mategemeo yangu ni kwamba ni watu ambao hawana msimamo katika mambo ambayo wametumwa kufanya. Kwa hivyo, hata tukiwa na sheria nzuri namna gani, wale ambao watatumwa kutekeleza sheria zile, ikiwa ni watu waoga ambao wanajali mkate wao kwanza kuliko kujali yale mambo ambayo yanafanyika, itakuwa ni kazi ya bure.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Ninampongeza ndugu yetu, Sen. Mungatana, MGH, kwa maswala haya. Tukiangalia maswala mengi ambayo kwa mfano, haki za wale---
view
12 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, kwanza, ninashukuru kwa maongozo yako. Lakini, najaribu kufikiria dada yangu, Sen. Veronica Maina, sijui amesimama kwa msingi gani ya Kanuni zetu za Kudumu za Bunge. Yale anayoyazungumza ni mambo ambayo--- Mimi sijataja Serikali ya Kenya Kwanza . Nimesema Serikali zote. Hata Serikali ya Jubilee ilimweka ndani Sen. Cherarkey bila msingi wowote na wakamnyima bond. Hata Sen. Olekina aliwekwa ndani na Serikali hiyo.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Kwa hivyo, sijataja Serikali ya Kenya Kwanza . Hiyo iko katika HANSARD . Aangalie ni wapi nimetaja Serikali ya Kenya Kwanza .
view