8 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
8 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, hospitali hii ndio tumaini la wananchi wengi katika eneo zima la Pwani, kwa hivyo, ni muhimu iweze kutoa huduma bora ili kuokoa maisha. Kwa hivyo, ningeomba Taarifa hii iwasilishwe kwa Kamati ya Kudumu ya Afya na walichunguze swala hili kwa undani ili mambo yaliyoshuhudiwa juzi yasirudiwe. Asante, Bw. Spika.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Kwa hoja la nidhamu, Bw. Spika. Nimesimama kulingana na kanuni zako hususan Kanuni Namba Tano kuhusu mavazi ambayo Maseneta wanastahili kuvaa wakiwa katika Bunge hili. Seneta mwanaume anafaa kuvaa koti, shati, tai, suruali ndefu, soksi na viatu, nguo za huduma ama nguo za kidini. Nimemuona ndugu yangu Sen. Chimera pale amevaa vazi ambalo sidhani lina ruhusiwa katika Bunge hili. Kwa hivyo, ningependa utoe mwongozo kuhusu vazi ambalo Sen. Chimera amevaa katika Bunge hili. Asante, Bw. Spika.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, hakuna koti la mikono mifupi.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Koti ni la mikono mirefu ambalo linatoka kutoka kwenye bega mpaka kwenye viganja. Hatuwezi kusema kwamba lile ni koti. Hata kama ingekuwa ni suti ya Kaunda, iwe ya mikono mirefu. Suti ya Kaunda ambayo Sen. Onyonka anavaa ni ya mikono mirefu na inaziba sehemu hizi mpaka kwenye vitanga.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Sen. Korir, ungenipa nafasi niongee.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Lile vazi alilovaa Sen. Chimera sio vazi ambalo linakubalika kulingana na Kanuni zako. Kama lingekuwa ni vazi la kienyeji, tungeweza kumsamehe. Suti ya Kaunda sio vazi la Kiafrika.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Bw. Spika singependa kumtatiza ndugu yangu Sen. Madzayo, lakini msemo ambao ameutumia haufai kutumika hapo. Hawezi kusema hasira ya mkizi furaha ya mvuvi. Yaani hasira za Sen. Sifuna ilikua ni furaha kwa Spika. Haiwezekani kuwa hivyo.
view
14 Feb 2023 in Senate:
Msemo aliotumia Sen. Madzayo haufai kutumika hivyo.
view