Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 651 to 660 of 2110.

  • 13 Jun 2023 in Senate: Swala la marupurupu ya mahakimu ni swala nzito sana. Hii ni kwa sababu ndio watu ambao wameidhinishwa na Katiba kujaribu kutatua mizozo katika nchi yetu. Kwa hivyo, ikiwa hawatalipwa malipo ya kisawasawa pamoja na marupurupu ambayo wanatakikana kupata, basi hali yetu ya kupata haki itatatizika. Bw. Spika, mahakimu wengi wanafanya kazi nzuri katika nchi yetu. Vile, kuna mahakimu ambao ni watepetevu na hawatakelezi majukumu yao kisawasawa. Ijapokuwa kuna mfumo mpya wa wao kupeleka hesabu zao kila mwezi, tumeona kwamba imekuwa ni donda sugu katika sehemu ambazo ziko nje ya Mji wa Nairobi na miji mingine mikubwa. Bw. Spika, tumeona ijapokuwa ... view
  • 8 Jun 2023 in Senate: Asante, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa Ugavi wa Raslimali kwa Kaunti zetu. Mgao wa Raslimali za Kaunti 2023 ni sheria muhimu ambayo inagawanya fedha zinazotoka kwa Serikali Kuu kwenda kwa serikali gatuzi. Bunge hili lilipitisha Mswada wa Division of Revenue Act (DORA) ambayo ilileta Kshs385.425 billioni, kutoka kwa Serikali Kuu Kwenda kwa serikali za kaunti. Ijapokuwa sheria hii ilipita shingo upande, ndio sheria ambayo iko. Kwa hivyo, sheria ambayo tunaijadili kwa sasa, imeundwa ikizingatia kwamba pesa zitakozota kutoka Serikali kuu kuja kwa serikali za kaunti ni Kshs385.425 billion. Ugavi wa rasilimali hii umezingatia mfumo wa ... view
  • 8 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 8 Jun 2023 in Senate: asilimia 10; ukubwa wa ardhi, asilimia nane; ukulima, asilimia 10; afya, asilimia 17, barabara, asilimia nane; ukuaji wa miji, asilimia tano; na umaskini, asilimia 14. Katika kujadili wa Mswada huu, Kamati yetu ilipata fursa na kuchukua maoni kutoka kwa Baraza la Magavana, Wizara ya Fedha, Tume ya Ugavi wa Rasilimali na washikadau wengine. Vile vile, Kamati ilipata maombi kutoka kaunti 17 ambazo zilitaka kuongezwa pesa za msingi kutoka mwaka 2023/2024. Baadhi ya mambo yaliyozungumziwa na mabunge ya kaunti ni pamoja na maswala ya usalama katika kaunti zilizo mbali. Kwa mfano, Kaunti ya Mandera inagharamika pakubwa kupeleka usalama wanapofanya public participation ... view
  • 8 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika, ningependa kumfahamisha ndugu yangu Seneta wa Elgeyo Marakwet, Sen. Kisang’ kwamba pesa ambazo tulipitisha kwa DORA ni Kshs385,425,000,000. Za maktaba haziko hapo. Waziri wa Fedha alipokuja katika Kamati yetu, alitaka kutuchanganya; alisema hizo Kshs425 milioni zilikuwa ni za kutoa huduma za maktaba ambazo zinatoka kwa Serikali Kuu zinakuja katika serikali za kaunti. Lakini, tukamwambia Kshs385,425,000,000 ndizo pesa ambazo zinakuja kama view
  • 8 Jun 2023 in Senate: aani, pesa ambazo zinatoka kwa Serikali Kuu zinakuja kwa serikali za kaunti. Mwishowe alikubali kwamba hakuna Kshs425 milioni ambazo ni za maktaba. Watatafuta katika fedha zao zingine lakini katika zile za mgao wa kitaifa, ni Kshs385,425,000,000. view
  • 7 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii ili niweze kujiunga na wenzangu kutoa rambirambi zetu kwako, kwa Katibu wa Bunge na familia ya mwendazake, Bi. Marya Adjibodou. Bw. Spika, kwa hakika ni pigo kubwa, sio kwa familia yake peke bali pia kwa Bunge hili la Seneti. Bi. Marya alikuwa mfanyikazi ambaye alikuwa anafanya kazi yake kwa uangalifu zaidi na kwa haraka, iwapo atahitajika kufanya hivyo kwa haraka. Bw. Spika, nilimjua Bi. Marya kutoka mwaka wa 1980 tulipokuwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Alikuwa akisomea Bachelor of Arts na mimi nilikuwa nikisomea uanasheria. Nilimpata hapa nilipokuja kwa muhula wangu wa ... view
  • 7 Jun 2023 in Senate: Mwenyezi Mungu alilaze roho yake pahali pema peponi. Asante. view
  • 6 Jun 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuongezea kauli yangu juu ya taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Cherarkey, Seneta wa Kaunti ya Nandi. Masaibu yanayokumba Wabunge wa Kaunti zetu ni ya kusikitisha. Ikikumbukwa kwamba ugatuzi ulikuja kuleta tofauti baina ya mabaraza ya miji yalikuwa yanahudumu wakati wa nyuma na mfumo mpya wa Serikali ambao unatumika katika nchi yetu ya Kenya. view
  • 6 Jun 2023 in Senate: Marupurupu wanayopata ni machache sana kulingana na hali ya maisha ilivyo hususan kwa wale ambao wako katika miji mikubwa na miji midogo pia. Tukiangalia, kwa mfano, katika Kaunti ya Mombasa, Wabunge hawa wa Bunge la Kaunti ya Mombasa wanahitajika kupata ofisi na nyumba ambazo zinastahili hadhi yao. Nyumba hizi haziwezi kukodishwa bila pesa. Kwa hivyo, yale marupurupu wanayopata hayawawezeshi kukabiliana na maisha kisawasawa. Ndio mara nyingi, wanapatikana wakihujumu kazi zao kupitia kwa ile ruzuku ndogo ndogo wanazopata kutoka kwa wakuu wa kaunti. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus