6 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, ijapokuwa sheria ilibadilishwa na ikawa fedha za county assembly na fedha za county executive ziko mbalimbali, lakini bado utapata kwamba Waziri ama Mwanakamati ambaye anahusika na mambo ya fedha za kaunti husika anahujumu utendakazi wa Bunge la Kaunti kwa sababu pesa zinazokuja kutoka kwa mfuko wa Serikali kuu sio hizo ambazo zinakwenda katika kulipa mishahara au marupurupu ya MCAs.
view
6 Jun 2023 in Senate:
Kwa hivyo, kuna haja ya kubadilisha ama kurekebisha sheria ya fedha, yaani, Public Finance Management (PFM) Act kuhakikisha kwamba bunge la kaunti lina fedha zake mbali na zile fedha ambazo ziko katika serikali ya kaunti. Hii ni kwa sababu serikali ya kaunti mara nyingi wakiitisha pesa, wanapunguziwa ama wanatolewa pesa kidogo kidogo ili kuhakikisha kwamba kazi zao zinahujumiwa.
view
6 Jun 2023 in Senate:
Nakubaliana na wenzangu ambao wametoa kauli kwamba swala hili lizungumzwe na Bunge nzima; kauli nzima ya Bunge hili iweze kuzamia swala hili ili wabunge wetu wa county assembly waweze kupata marupurupu ya kisawa sawa. Vile vile, SRC wapewe onyo kwamba kupunguza marupurupu haya kunahujumu ugatuzi katika nchi yetu. Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii.
view
31 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu ya 53(1) kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa kuhusu kuchelewa kwa
view
31 May 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
31 May 2023 in Senate:
kuchapishwa kwa paspoti nchini ambako kunaathiri mipango ya safari ya mahujaji wanaokwenda Makkah nchini Saudi Arabia kwa ibada yao ya Hajj mwaka huu. Katika taarifa hiyo, Kamati iangazie yafuatayo- (1) Iiarifu Seneti chanzo cha ucheleweshaji wa usindikaji wa Paspoti katika Idara ya Uhamiaji, ikizingatia madhara na usumbufu unaoletwa na uchelewashaji huo kwa mahujaji wanaokwenda Makkah, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hajj katika mwezi Juni, 2023. Ibada ya Hajj inatarajiwa baadaye mwezi ujao kuanzia 20.06.2023. (2) Ieleze ni hatua gani Serikali inachukua kuharakisha usindikaji na uchapishaji wa pasipoti hizo ikizingatiwa kwamba mahujaji watalazimika kuvunja na kughairi safari zao iwapo jambo hilo ...
view
30 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kupeleka vikao vya Bunge la Seneti katika Kaunti ya Turkana. Bw. Spika, mji mkuu wa Turkana ni Lodwar ambao uko takriban kilomita 748 kutoka jiji la Nairobi. Safari ya Turkana ni ya siku mbili. Inabidi upumzike Kitale kama
view
30 May 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
30 May 2023 in Senate:
unakwenda kwa gari kama walalahoi au “mahustlers” wengi. Baaadaye, siku ya pili uendelee na safari mpaka Lodwar. Bw. Spika, hii itatoa fursa kubwa kwa Bunge la Seneti kusoma maeneo ya Turkana na maeneo jirani. Vile vile, itatoa fursa kwa watu wa Turkana kusoma Bunge lao linafanya kazi namna gani. Itakuwa ni fursa ya Bunge la Kaunti ya Turkana kupata fursa ya kuona vikao vya Seneti na vile kamati tofauti tofauti za Seneti zinavyofanya kazi. Kamati hizi ama mabunge haya ya kaunti, mara nyingi huwa yamelema kikazi kwa sababu ya kutopata nafasi ya kusoma kutokana na vile kazi zinavyotendwa katika mabunge ...
view
25 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia ombi la taarifa kutoka kwa Seneta---
view