Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 671 to 680 of 2123.

  • 7 Jun 2023 in Senate: Mwenyezi Mungu alilaze roho yake pahali pema peponi. Asante. view
  • 6 Jun 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuongezea kauli yangu juu ya taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Cherarkey, Seneta wa Kaunti ya Nandi. Masaibu yanayokumba Wabunge wa Kaunti zetu ni ya kusikitisha. Ikikumbukwa kwamba ugatuzi ulikuja kuleta tofauti baina ya mabaraza ya miji yalikuwa yanahudumu wakati wa nyuma na mfumo mpya wa Serikali ambao unatumika katika nchi yetu ya Kenya. view
  • 6 Jun 2023 in Senate: Marupurupu wanayopata ni machache sana kulingana na hali ya maisha ilivyo hususan kwa wale ambao wako katika miji mikubwa na miji midogo pia. Tukiangalia, kwa mfano, katika Kaunti ya Mombasa, Wabunge hawa wa Bunge la Kaunti ya Mombasa wanahitajika kupata ofisi na nyumba ambazo zinastahili hadhi yao. Nyumba hizi haziwezi kukodishwa bila pesa. Kwa hivyo, yale marupurupu wanayopata hayawawezeshi kukabiliana na maisha kisawasawa. Ndio mara nyingi, wanapatikana wakihujumu kazi zao kupitia kwa ile ruzuku ndogo ndogo wanazopata kutoka kwa wakuu wa kaunti. view
  • 6 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika, ijapokuwa sheria ilibadilishwa na ikawa fedha za county assembly na fedha za county executive ziko mbalimbali, lakini bado utapata kwamba Waziri ama Mwanakamati ambaye anahusika na mambo ya fedha za kaunti husika anahujumu utendakazi wa Bunge la Kaunti kwa sababu pesa zinazokuja kutoka kwa mfuko wa Serikali kuu sio hizo ambazo zinakwenda katika kulipa mishahara au marupurupu ya MCAs. view
  • 6 Jun 2023 in Senate: Kwa hivyo, kuna haja ya kubadilisha ama kurekebisha sheria ya fedha, yaani, Public Finance Management (PFM) Act kuhakikisha kwamba bunge la kaunti lina fedha zake mbali na zile fedha ambazo ziko katika serikali ya kaunti. Hii ni kwa sababu serikali ya kaunti mara nyingi wakiitisha pesa, wanapunguziwa ama wanatolewa pesa kidogo kidogo ili kuhakikisha kwamba kazi zao zinahujumiwa. view
  • 6 Jun 2023 in Senate: Nakubaliana na wenzangu ambao wametoa kauli kwamba swala hili lizungumzwe na Bunge nzima; kauli nzima ya Bunge hili iweze kuzamia swala hili ili wabunge wetu wa county assembly waweze kupata marupurupu ya kisawa sawa. Vile vile, SRC wapewe onyo kwamba kupunguza marupurupu haya kunahujumu ugatuzi katika nchi yetu. Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. view
  • 31 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu ya 53(1) kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa kuhusu kuchelewa kwa view
  • 31 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 31 May 2023 in Senate: kuchapishwa kwa paspoti nchini ambako kunaathiri mipango ya safari ya mahujaji wanaokwenda Makkah nchini Saudi Arabia kwa ibada yao ya Hajj mwaka huu. Katika taarifa hiyo, Kamati iangazie yafuatayo- (1) Iiarifu Seneti chanzo cha ucheleweshaji wa usindikaji wa Paspoti katika Idara ya Uhamiaji, ikizingatia madhara na usumbufu unaoletwa na uchelewashaji huo kwa mahujaji wanaokwenda Makkah, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hajj katika mwezi Juni, 2023. Ibada ya Hajj inatarajiwa baadaye mwezi ujao kuanzia 20.06.2023. (2) Ieleze ni hatua gani Serikali inachukua kuharakisha usindikaji na uchapishaji wa pasipoti hizo ikizingatiwa kwamba mahujaji watalazimika kuvunja na kughairi safari zao iwapo jambo hilo ... view
  • 30 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kupeleka vikao vya Bunge la Seneti katika Kaunti ya Turkana. Bw. Spika, mji mkuu wa Turkana ni Lodwar ambao uko takriban kilomita 748 kutoka jiji la Nairobi. Safari ya Turkana ni ya siku mbili. Inabidi upumzike Kitale kama view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus