30 May 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
30 May 2023 in Senate:
unakwenda kwa gari kama walalahoi au “mahustlers” wengi. Baaadaye, siku ya pili uendelee na safari mpaka Lodwar. Bw. Spika, hii itatoa fursa kubwa kwa Bunge la Seneti kusoma maeneo ya Turkana na maeneo jirani. Vile vile, itatoa fursa kwa watu wa Turkana kusoma Bunge lao linafanya kazi namna gani. Itakuwa ni fursa ya Bunge la Kaunti ya Turkana kupata fursa ya kuona vikao vya Seneti na vile kamati tofauti tofauti za Seneti zinavyofanya kazi. Kamati hizi ama mabunge haya ya kaunti, mara nyingi huwa yamelema kikazi kwa sababu ya kutopata nafasi ya kusoma kutokana na vile kazi zinavyotendwa katika mabunge ...
view
25 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia ombi la taarifa kutoka kwa Seneta---
view
25 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu wa Spika. Kabla sijachangia maombi ya Taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Hamida, ningependa kumkumbusha Sen. (Dr.) Khalwale kuwa hili ni Bunge. Mambo ya Bunge ni mambo ya Bunge na mambo ya Rais ni mambo ya Rais. Kwa hivyo, mambo ya Bunge lazima yazungumzwe Bungeni. Ningependa kuchangia Taarifa kuhusiana na kuachiliwa kwa wafungwa wanaotumikia vifungo vidogo vidogo gerezani. Ninawapongeza Maseneta wa Kenya Women Senators Association (KEWOSA) ambao juzi walizuru gereza la kina mama la Langata, ambapo waliwatoa takriban wafungwa 100. Wafungwa hao walikuwa wamefungwa kwa makosa madogo madogo. Bw. Naibu wa Spika, hii sio mara ya kwanza kwa ...
view
25 May 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
25 May 2023 in Senate:
Tulitoa zaidi ya wafungwa 100 kutoka gereza lile. Baada ya hapo, Jaji Mutende aliyekuwa akihudumu katika kituo kile, alifanya ziara katika gereza lile, akaangalia zile faili za wafungwa wote waliokuwa na makossa madogo madogo, na wote wakaruhusiwa kwenda nyumbani. Ni kwa sababu ya kazi ambayo Bunge la Seneti lilikua limefanya. Bw. Naibu wa Spika, ni muhimu swala hili liangaliwe kwa undani. Tulipokuwa tunahudumu katika Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Binadamu, tulizuru gereza la Industrial Area. Hapo, wafungwa wanaishi katika hali ngumu sana, hususan wale walioko rumande wanaosubiri kesi zao zimalizwe ndio waende nyumbani. Hao wafungwa wanazuiliwa kwa dhamana ...
view
25 May 2023 in Senate:
Bw. Naibu wa Spika, mkumbushe Sen. Gataya Mo Fire, hatuko Runyenjes hapa.
view
25 May 2023 in Senate:
Magereza yetu yote yalijengwa kabla ya uhuru. Kwa muda wa takriban miaka 60, Kenya haijajenga gereza hata moja. Kwa hivyo, nafasi ni ndogo katika magereza yetu na wafungwa wengi wanapata shida. Kwa hivyo, jinsi ya kutatua msongomano katika jela zetu ni swala ambao lazima liangaliwe kwa undani zaidi. Wanaohukumiwa aghalabu wapate afueni kutokana na hali mbaya ya magereza yetu.
view
24 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa kuunga mkono Ardhihali ambayo imeletwa Bungeni na Julius Wairiuku Wanjohi kuhusiana na kutotekelezwa kwa maazimio ya kuwaajiri wafanyikazi katika Kaunti ya Nyeri. Bw. Naibu Spika, ni masikitiko kwamba ni miaka 10 sasa na hao wafanyikazi hawajaandikwa kazi na Kaunti ya Nyeri. Kama tunavyojua, stimulus package ilikwisha, Serikali za kaunti zikaanza kazi na hawa wakasahaulika kabisa kutokana na utepetevu wa Serikali ya Kaunti ya Nyeri. Ningependa kuongezea kuwa hawa wakufunzi wanafanya kazi muhimu. Wale wote ambao hawafaulu kwenda kwa taasisi ama chuo kikuu, hujifunza kazi za mikono katika taasisi hizi ambazo wakufunzi hawa wanafanya ...
view
24 May 2023 in Senate:
Mr. Deputy Speaker, Sir, I beg to give Notice of the following Motion - THAT, AWARE THAT rapid urbanization, as experienced in most Kenyan towns contributes to a significant portion of greenhouse gas emissions leading to environmental degradation; FURTHER AWARE THAT factors associated with urbanization, including changes to a more sedentary lifestyle, diet and environment have resulted in an increase in the prevalence of non-communicable diseases such as cardiovascular disease, diabetes, and cancer; APPRECIATING THAT prioritizing sustainability and environmental responsibility creates liveable, healthy and resilient communities for present and future generations; NOW THEREFORE, the Senate urges the:
view