Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 691 to 700 of 2110.

  • 3 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 3 May 2023 in Senate: Mauaji ya mbari yanayotokea kule Marsabit na sehemu zingine zinazokaliwa na jamii za wafugaji, ni jambo la kusikitisha katika karne ya ishirini nchini. view
  • 3 May 2023 in Senate: Wameshindwa kusoma masomo yaliyotokea Rwanda mwaka wa 1994. Leo ikiwa karibu miaka thelathini, tangu matokeo ya Rwanda, na bado nchini watu wanauwana kiholela kimbari kupigania uongozi. view
  • 3 May 2023 in Senate: Wengine wetu tunashangaa ilikuwaje babu zetu wakatujumuisha na watu wengine Kenya. Kwetu Pwani hakuna itikadi ama hulka ya kuua mwenzako kwa njia yeyote. Yale uliyoyasikia juzi ya Shakahola, ni wageni waliokuja kutoka sehemu zingine ndio wamepata msitu na kuanza kufanya itikadi zao mbovu. view
  • 3 May 2023 in Senate: Ni masikitiko kwamba Serikali tuliyonayo, miaka 60 ya uhuru, bado tunauwana na kupoteza maisha kiholela. Vijana na akina mama wanauliwa bila makosa yoyote waliyofanya katika maeneo yao. Ukiangalia vyema, mambo haya yanafanywa chini ya uangalizi wa Serikali. view
  • 3 May 2023 in Senate: Tulipoenda Shakahola juzi, tulipata kwamba zaidi ya watu 110 walipoteza maisha yao kwa sababu ya mafunzo ya itikadi kali ya mmoja wa wanaojiita makasisi au mapasta katika eneo lile. Pasta yule amekwenda kortini na kutoka kama mara 50. Kuanzia mwaka wa 2018, Serikali ilikuwa inajua kwamba alikua akifundisha watoto wasiende shule na ana itikadi ya kufundisha watu wasiende hospitali wakiwa wagonjwa. Lakini Serikali ilimuangalia tu. view
  • 3 May 2023 in Senate: Masikitiko ni kwamba kama ingekua ni Muislamu aliyefanya mambo yale nina hakika angekua ameenda mbele ya Mwenyezi Mungu kufikia sasa. Sheikh Abdi Rogo alipigwa risasi mbele ya bibi yake. Alikuwa ndani ya gari na bibi yake na mtoto, akapigwa risasi na kuuliwa. Bibi yake kutoka wakati huo mpaka sasa hajapata amani. Sheikh Makaburi Abubakar alitoka kortini Shanzu na kupigwa risasi na kuuliwa pale bila ya hatia yeyote. view
  • 3 May 2023 in Senate: Ni masikitoko kwamba watu wanauwana Marsabit, Samburu na Turkana wakati Serikali iko pale, iko macho na haifanyi chochote. Jana tumepeleka ardhilhali katika Ofisi ya Rais na tulitimuliwa na polisi kama 200. Wabunge 20 wanatimuliwa na askari 200. view
  • 3 May 2023 in Senate: Tulikuwa tumepeleka Petition kwa Serikali. Ni makosa kupeleka Petition kwa Serikali? Tunaona kwamba Serikali inatumia vibaya mamlaka yake. Mahali watu wanaumia na kufa, hakupelekwi usalama. Lakini hapa katikati ya mji, Wabunge 11 ama 20 wamekwenda kupeleka Petition kwa Ofisi ya Rais, tunaskumwa na kupigwa na view
  • 3 May 2023 in Senate: na kufukuzwa kama wahalifu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus