3 May 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
3 May 2023 in Senate:
Sen. Cherarkey, katika mazungumzo yake, amesema kwamba Serikali imetoa Kshs385 billioni katika mwaka wa 2023/2024 kwa mgao wa fedha. Tukiangalia makadilio ambayo Serikali ilipeleka Bungeni ya mwaka wa 2023/2024, wanatarajia kukusanya zaidi ya Kshs2.571 trillioni ambazo ni ongezeko la asilimia 17. Haiwezekani kwamba Serikali itapata ongezeko la asilimia 17 katika mapato yake, halafu itoe chini ya asilimia tano ya zile pesa ambazo itakusanya katika mwaka wa 2023/2024 wa kifedha. Sen. Cherarkey anatupotosha mawazo kwa kusema kwamba tayari Serikali imetoa pesa nyingi tukilinganisha na pesa ambazo zitakusanywa na Serikali katika muhula huu. Pesa hizi zote zinakusanywa katika kaunti zetu. Hakuna mahali ...
view
3 May 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia hoja ambayo imeletwa Bungeni na Sen. Chute, Seneta wa Marsabit.
view
3 May 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
3 May 2023 in Senate:
Mauaji ya mbari yanayotokea kule Marsabit na sehemu zingine zinazokaliwa na jamii za wafugaji, ni jambo la kusikitisha katika karne ya ishirini nchini.
view
3 May 2023 in Senate:
Wameshindwa kusoma masomo yaliyotokea Rwanda mwaka wa 1994. Leo ikiwa karibu miaka thelathini, tangu matokeo ya Rwanda, na bado nchini watu wanauwana kiholela kimbari kupigania uongozi.
view
3 May 2023 in Senate:
Wengine wetu tunashangaa ilikuwaje babu zetu wakatujumuisha na watu wengine Kenya. Kwetu Pwani hakuna itikadi ama hulka ya kuua mwenzako kwa njia yeyote. Yale uliyoyasikia juzi ya Shakahola, ni wageni waliokuja kutoka sehemu zingine ndio wamepata msitu na kuanza kufanya itikadi zao mbovu.
view
3 May 2023 in Senate:
Ni masikitiko kwamba Serikali tuliyonayo, miaka 60 ya uhuru, bado tunauwana na kupoteza maisha kiholela. Vijana na akina mama wanauliwa bila makosa yoyote waliyofanya katika maeneo yao. Ukiangalia vyema, mambo haya yanafanywa chini ya uangalizi wa Serikali.
view
3 May 2023 in Senate:
Tulipoenda Shakahola juzi, tulipata kwamba zaidi ya watu 110 walipoteza maisha yao kwa sababu ya mafunzo ya itikadi kali ya mmoja wa wanaojiita makasisi au mapasta katika eneo lile. Pasta yule amekwenda kortini na kutoka kama mara 50. Kuanzia mwaka wa 2018, Serikali ilikuwa inajua kwamba alikua akifundisha watoto wasiende shule na ana itikadi ya kufundisha watu wasiende hospitali wakiwa wagonjwa. Lakini Serikali ilimuangalia tu.
view
3 May 2023 in Senate:
Masikitiko ni kwamba kama ingekua ni Muislamu aliyefanya mambo yale nina hakika angekua ameenda mbele ya Mwenyezi Mungu kufikia sasa. Sheikh Abdi Rogo alipigwa risasi mbele ya bibi yake. Alikuwa ndani ya gari na bibi yake na mtoto, akapigwa risasi na kuuliwa. Bibi yake kutoka wakati huo mpaka sasa hajapata amani. Sheikh Makaburi Abubakar alitoka kortini Shanzu na kupigwa risasi na kuuliwa pale bila ya hatia yeyote.
view