Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 711 to 720 of 1995.

  • 16 Nov 2022 in Senate: sababu ya wasiwasi. Sasa hivi, Serikali imepiga marufuku mikutano kufanyika katika mahoteli kama hayo. Bw. Spika, iwapo agizo hili litatekelezwa, itaamaanisha ya kwamba wale wawekezaji wa biashara za hoteli, watakosa kupata faida yoyote, mwaka huu wa 2022. Agizo hili litaadhiri uchumi kwa sababu mapato yanayotokana na utalii yataweza kupungua na hata yale malengo ya Serikali ya kukusanya pesa walizotarajia mwezi wa sita, bajeti iliposomwa, hayataweza kutimizwa. Ningependa swala hili liangaliwe kwa haraka, kwa sababu tayari tunafikia mwisho wa mwaka na wangependelea angalau wapate faida kidogo, ili waweze kuregesha raslimali zao mwaka huu wa 2022. Asante, Bw. Spika. view
  • 16 Nov 2022 in Senate: Asante Spika wa Muda, kwa kunipa fursa ya kuchangia Hoja iliyoletwa na Sen. Mungatama, MGH, Seneta wa Kaunti ya Tana River. Masuala ambayo ameyazungumzia Sen. Mungatana, MGH ni mazito sana ikizingatiwa kwamba maji ni uhai na tumekuwa na maafa ya mara kwa mara katika eneo la Mto Tana, ikiwemo ukame ambao sasa unaendelea pakubwa. Vilevile, kuna mafuriko ambayo yanatokea mara kwa mara. Bw. Spika wa Muda, Mto Tana ni sehemu ambayo iko na nafasi kubwa ya kuinua uchumi wa Kaunti yake na hata nchi nzima kwa jumla. Hii ni kwa sababu mahali ambapo Mto Tana unaingia katika Bahari ya Hindi, ... view
  • 16 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 16 Nov 2022 in Senate: Ninaunga mkono maoni ya Mhe. Ali Roba, kwamba kufanywe tena uchunguzi upya kuhusiana na mradi huu. Tuangalie hatari gani imeletwa kwa mazingira na wananchi wote, baada ya kuidhinishwa kwa mradi huu kuanzia sehemu ya juu kule ambako maji yanakwenda, mpaka sehemu ya chini ambayo ni mtoni, ambako maji yale yalikuwa yanafika kusaidia wananchi ambao wako katika sehemu zile. Bw. Spika wa Muda, mradi wa Galana-Kulalu ungesaidia pakubwa maswala haya. Mradi wa Bura ambao pia uko katika Kaunti ya Tana River, pia ungesaidia. Hii miradi yote imesalia kuwa kitendawili. Hadi sasa, miradi hii haijaleta latija ambayo iliyotakiwa. Kwa mfano, kilimo cha ... view
  • 15 Nov 2022 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Ripoti ambayo imeletwa Bungeni ya uteuzi wa wagombea wa ubunge wa EALA. Kwa hakika wote ambao wameteuliwa wanatajiriba. Ni vizuri tuchague watu ambao watakuwa na uwezo wa kusongesha mbele Bunge hili la Afrika Mashariki. Bw. Spika, tukiangalia katika zile taasisi za East Africa Cooperation, Mahakama ya East Africa imefanya maamuzi ambayo yamesaidia maswala ya haki za binadamu katika maeneo yetu kwa sehemu kubwa kuliko yale ambayo yamefanywa na Bunge hili. Hayo yote yametokana na maswala kwamba wale wanaoenda kutuwakilisha ni watu ambao wanaenda kutafuta kazi. Si watu wanaoenda kuangalia yale maswala ... view
  • 10 Nov 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyowasilishwa na Sen. Crystal Asige. Naunga mkono Taarifa hii ya Sen. Crystal Asige kwa sababu mambo yanayoangaziwa katika Taarifa hii ni ya kimsingi. Nilibahatika kuwa mwanachama wa Rotary Club of Mombasa. Kila baada ya wiki mbili, huwa tunakwenda kuwalisha watoto walemavu katika Shule ya Port Reitz. Ukiona wale watoto wanavyoishi, utagundua kwamba ipo haja ya kuwasaidia ili waishi angalau maisha mazuri kidogo. Wakati tunapokwenda kuwatembelea wanafunzi katika Shule ya Port Reitz ambayo ni ya watoto walemavu, huwa tunapata kuwa walimu hawatoshi ukilinganisha na idadi ya wanafunzi. Mbali na kuwapelekea chakula, sisi ... view
  • 10 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 10 Nov 2022 in Senate: Mwisho, Bw. Spika, ni kwamba wakati watoto hao wanapokua, ni vigumu sana kupata vyeti kuonyesha kwamba ni walemavu. Lazima mtoto kama huyo alipe Kshs1,500 katika hospitali za kaunti ili apewe cheti cha kuonyesha kwamba ni mlemavu, ndiposa aweze kupata marupurupu ama fadhila zingine za kuonyesha kwamba ni mlemavu. Katika jamii, sisi tunatakikana tuwasaidie zaidi kuliko tunavyojisaidia sisi wenyewe. Bw. Spika, naunga mkono Taarifa hii. view
  • 10 Nov 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika. Nimesikia Mhe. Munyi Mundigi, Seneta wa Embu akizungumzia swala la Muguka. Swala hili kwa watu wa Mombasa limezua utata kwa sababu ulaji wa Muguka umeharibu nyumba nyingi na vijana wengi sana. Hao vijana badala ya kufanya kazi wanarandaranda, wanawacha mabibi zao nyumbani--- view
  • 10 Nov 2022 in Senate: Bw. Spika, singependa kujulishwa chochote na Seneta wa Meru kwa sababu najua athari za Miraa na Muguka . Vijana wengi wameathirika na mambo haya. Mbali wanalia kwamba ushuru na kodi wanazotozwa ziko juu, ningependekeza ziongezwe maradufu ili mmea huo usiweze kufika Mombasa na Pwani kwa jumla ili vijana wetu waokoke. Kila kijana ambaye amemaliza shule hukimbia kukaa kula view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus