27 Apr 2023 in Senate:
(1) Iarifu Seneti lini wakandarasi wa ujenzi wa barabara hizo tatu watarudi kuendelea na mradi wa ujenzi wa barabara hizo, ikikumbukwa kwamba, muda mahsusi uliotangazwa kuchukua ujenzi huo umekamilika.
view
27 Apr 2023 in Senate:
(2) Iwapo Kenya National Highways Authority (KENHA) inatambua kwamba kutokamilika kwa barabara hizo, imekuwa kero kwa wahudumu wa usafiri na wananchi kwa jumla katika maeneo hayo. (3) Ibaini ni hatua gani Kenya National Highways Authority (KENHA) itachukua dhidi ya wanakandarasi hao, walioondoka kwenye maeneo ya kazi bila kukamilisha mradi huo, ikizingatiwa kwamba hasara kubwa zinazokadiriwa na kampuni za uchukuzi, kwa kuharibika kwa magari yao kutokana na ubovu wa barabara hiyo. Mheshimiwa Spika, jumamosi iliyopita, wasafiri wengi waliokuwa wanakwenda
view
27 Apr 2023 in Senate:
walichelewa kwa sababu barabara ya kutoka Barclays mpaka Jomvu, maeneo ya Kibarani ilifurika, kusababisha magari kutoweza kupita. Wengi waliokuwa wanasafari kuelekea SGR na Airport walitatizwa na mvua kubwa iliyosababisha maji mengi kwenye barabara hiyo. Asante, Mheshimiwa Spika
view
25 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika.
view
25 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ambayo imeletwa Bungeni na Sen. Mteule, Sen. Miraj. Kabla ya janga la COVID-19, mwaka wa 2020, ndege nyingi zilikuwa zinakuja Mombasa, kwa mfano, Turkish Airlines, Qatar Airways na nyingi nyinginezo zilizokuwa zikileta abiria na kufanya biashara katika Mji wa Mombasa. Bali na Jomo Kenyatta hapa Nairobi, MIA ni mojawapo ya vile viwanja vikubwa viwili ambavyo vina uwezo wa kuchukua ndege zote zinazoweza kuruka ulimwenguni. Ni masikitiko kwamba kutokana na ukosefu wa ndege hizo, biashara katika kaunti ya Mombasa na kaunti jirani imedorora kwa sababu ya ukosefu wa wageni wanaokuja kutalii ...
view
25 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
25 Apr 2023 in Senate:
kwamba uwanja ule haukai bure na Kenya Airways pekee yake au ndege mbili au tatu ambazo ni za kukodi zinakuja moja moja kutoka Ulaya. Iwapo ndege hizi zitaruhusiwa, Turkish, Qatar na Emirates zilizokuwa zinakuja, zikiruhusiwa zitasaidia pakubwa kuinua biashara katika ukanda mzima wa Pwani. Ukanda wa pwani unafika hadi sehemu za Kitui na kwengine ambako hamna viwanja kama hivi. Tungependa swala hili liingiliwe kwa undani zaidi kwa sababu hakuna lengo la Kenya Airways kupata hasara kila mwaka kwa sababu hamna ndege nyingine zinatua pale ilhali uwanja ni mkubwa na unaeza kuhimili ndege aina yeyote katika ulimwengu huu. Asante.
view
18 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nilileta Kauli hapa kuhusu kusitishwa kwa huduma za umeme katika Coast General Teaching and Referral Hospital katika Kaunti ya Mombasa. Hadi leo, sijapata ripoti yoyote wala Mwenyekiti wa Kamati ya Afya hakuitaji Kauli hiyo katika ripoti yake ya miezi sita tangu Kamati ilipoanza kazi mwezi wa Oktoba mwaka jana.
view
18 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bwana Spika, kwa kunielekeza. Nilileta Kauli hapa katika Seneti kuhusu kukatwa kwa nguvu za umeme katika Hospitali kuu ya Pwani yani Coast General and Referral Hospital . Niliomba Taarifa ile ninafikiri mwanzo wa mwezi wa tatu na hadi leo sijapata ripoti yoyote kuhusu mikakati ambayo Kamati imefanya ili kuchunguza na kuupata ukweli kuhusu kusisitshwa huduma katika hospitali kuu. Ni muhimu kwa sababu nguvu za umeme zinahitajika katika hospitali hususan katika vile vitengo vya wagonjwa mahututi, watoto waliozaliwa kabla ya umri wao na sehemu zingine zinazohitaji nguvu za umeme. Ningependa Mwenyekiti wa Kamati, atoe shauku kuwa hakuweka Kauli ile chini ...
view
13 Apr 2023 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view