12 Apr 2023 in Senate:
Samahani, Bw. Naibu Spika, kama umeielewa hivyo. Mategemeo yangu ni kwamba ni watu ambao hawana msimamo katika mambo ambayo wametumwa kufanya. Kwa hivyo, hata tukiwa na sheria nzuri namna gani, wale ambao watatumwa kutekeleza sheria zile, ikiwa ni watu waoga ambao wanajali mkate wao kwanza kuliko kujali yale mambo ambayo yanafanyika, itakuwa ni kazi ya bure.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Ninampongeza ndugu yetu, Sen. Mungatana, MGH, kwa maswala haya. Tukiangalia maswala mengi ambayo kwa mfano, haki za wale---
view
12 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, kwanza, ninashukuru kwa maongozo yako. Lakini, najaribu kufikiria dada yangu, Sen. Veronica Maina, sijui amesimama kwa msingi gani ya Kanuni zetu za Kudumu za Bunge. Yale anayoyazungumza ni mambo ambayo--- Mimi sijataja Serikali ya Kenya Kwanza . Nimesema Serikali zote. Hata Serikali ya Jubilee ilimweka ndani Sen. Cherarkey bila msingi wowote na wakamnyima bond. Hata Sen. Olekina aliwekwa ndani na Serikali hiyo.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Kwa hivyo, sijataja Serikali ya Kenya Kwanza . Hiyo iko katika HANSARD . Aangalie ni wapi nimetaja Serikali ya Kenya Kwanza .
view
12 Apr 2023 in Senate:
Pili, kama amesoma Mswada huu kikamilifu, kuna mahali ambapo kuna Tume ya
view
12 Apr 2023 in Senate:
Ukiangalia kuna Commission established under Section 3 of the KNHRC na
view
12 Apr 2023 in Senate:
Hizi ni taasisi ambazo zimetajwa hapa. Nimesema kwamba ikiwa taasisi hizi zina watu ambao hawana msimamo, wandani wa wale wanaoongoza Serikali, ina maana kwamba yale yote ambayo yanatarajiwa kufanyika kulingana na sheria hii hayataweza kufanyika.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Tumesema kwamba licha ya kuwa na sheria, lazima pia tuwe na watu wenye msimamo wa kusimamia sheria zile ili zikitekelezwa, watu waweze kupata haki zao kikamilifu.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu wa Spika, katika Bunge lililokwisha, kulikuwa na Mswada watu wa Kaunti ya Nakuru, walipokuwa wanaomba kupata nafasi ya kuwa jiji, yani City County, waliwakusanya randa randa wote wa mjini wakaenda wakawatupa msituni kule Kaunti ya Baringo.
view