12 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, tukiangalia wakulima, hivi majuzi Serikali ilileta mfumo wa kuleta mbolea. Ijapokuwa ni jambo nzuri, ni jambo la kushangaza kwamba Serikali yetu imetoka hapa mpaka nchi ya Zambia kuenda kuwasaidia wakulima nchini humo kuzalisha mahindi mengi ili walete Kenya wakati hatujaweza kuwahudumia wakulima wetu kikamilifu. Badala ya kuwa na vipimo vya kupima Zambia, tutaleta mahindi ama tutaleta mazao kiasi gani, tuwe na vipimo vyetu hapa Kenya ili kuona kwamba wakulima wetu wote wanazalisha chakula cha kutosha ili kulisha nchi yetu ya Kenya. Katika maswala ya maji, kunajengwa mabwawa kila mara lakini tatizo sugu la maji bado halijatatuliwa. Kwa ...
view
12 Apr 2023 in Senate:
Ndio, Bw. Naibu Spika.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Kwa Kiingereza, tunaweza kusema ni puppets wa Serikali zilizoko. Na hii haikuanza sasa---.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Samahani, Bw. Naibu Spika, kama umeielewa hivyo. Mategemeo yangu ni kwamba ni watu ambao hawana msimamo katika mambo ambayo wametumwa kufanya. Kwa hivyo, hata tukiwa na sheria nzuri namna gani, wale ambao watatumwa kutekeleza sheria zile, ikiwa ni watu waoga ambao wanajali mkate wao kwanza kuliko kujali yale mambo ambayo yanafanyika, itakuwa ni kazi ya bure.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Ninampongeza ndugu yetu, Sen. Mungatana, MGH, kwa maswala haya. Tukiangalia maswala mengi ambayo kwa mfano, haki za wale---
view
12 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, kwanza, ninashukuru kwa maongozo yako. Lakini, najaribu kufikiria dada yangu, Sen. Veronica Maina, sijui amesimama kwa msingi gani ya Kanuni zetu za Kudumu za Bunge. Yale anayoyazungumza ni mambo ambayo--- Mimi sijataja Serikali ya Kenya Kwanza . Nimesema Serikali zote. Hata Serikali ya Jubilee ilimweka ndani Sen. Cherarkey bila msingi wowote na wakamnyima bond. Hata Sen. Olekina aliwekwa ndani na Serikali hiyo.
view
12 Apr 2023 in Senate:
Kwa hivyo, sijataja Serikali ya Kenya Kwanza . Hiyo iko katika HANSARD . Aangalie ni wapi nimetaja Serikali ya Kenya Kwanza .
view
12 Apr 2023 in Senate:
Pili, kama amesoma Mswada huu kikamilifu, kuna mahali ambapo kuna Tume ya
view
12 Apr 2023 in Senate:
Ukiangalia kuna Commission established under Section 3 of the KNHRC na
view