15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, ndio namalizia. Kuna tofauti kati ya ruling ambayo ni hukumu tribunal imetoa na amri ambayo imetolewa kuambatana na hiyo hukumu. Bw. Spika, tumeweza kukukabidhi stakabadhi zote ambazo ni muhimu kuhusiana na swala hili. Tumetoa hukumu iliyosomwa jana na amri iliyoambatana na hukumu hiyo. Kwa hivyo, iliyobakia ni wewe utoe uamuzi wako. Kuna ndugu zetu wengine, kama Sen. Chute kutoka Mandera, ambao wamekuja hapa kufanya kazi. Kwa hivyo---
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, ninamaliza. Tunaomba tuweza kumaliza swala hili haraka, ili tuweze kurejelea shughuli zetu za kawaida kama Bunge la Seneti la Jamhuri ya Kenya. Asante sana, Bw. Spika.
view
8 Mar 2023 in Senate:
Thank you Mr. Speaker, Sir. I wanted to add an issue to the Statement sought by Sen. Crystal Asige. First, I thank her for bringing that Statement in pursuit of the rights of PWDs. The relevant Committee in considering this aspect of the Statement, they should also consider whether the nominations, which have been done in those counties comply with the law. This is because, the law says that the nomination should not exceed one- third of the elected Members of the County Assembly (MCAs). There are some County Assemblies that have more than a third of nominated Members serving ...
view
8 Mar 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika. Nimesimama kuambatana na Kifungu cha 52(1) cha Kanuni za Kudumu za Seneti kuzungumzia swala la dharura ambalo ni kuzuiliwa ama kukatwa kwa umeme katika Hospitali Kuu Ya Pwani, yaani Coast General Hospital, hapo jana, tarehe 7, Machi, 2023. Bw. Spika, hospitali hii ndiyo taasisi kubwa ya afya katika eneo zima la Pwani. inahudumia Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River, Lamu na Taita Taveta. Kwa hivyo, utendakazi wake unaangaziwa Pwani nzima Kwa jumla. Kudorora kwa huduma katika hospitali hii kutasababisha maafa kwa wengi ambao tegemeo lao ni hospitali hii. Bw. Spika, kuna huduma muhimu katika hospitali hii zinazoendeshwa na ...
view
8 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
8 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, hospitali hii ndio tumaini la wananchi wengi katika eneo zima la Pwani, kwa hivyo, ni muhimu iweze kutoa huduma bora ili kuokoa maisha. Kwa hivyo, ningeomba Taarifa hii iwasilishwe kwa Kamati ya Kudumu ya Afya na walichunguze swala hili kwa undani ili mambo yaliyoshuhudiwa juzi yasirudiwe. Asante, Bw. Spika.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Kwa hoja la nidhamu, Bw. Spika. Nimesimama kulingana na kanuni zako hususan Kanuni Namba Tano kuhusu mavazi ambayo Maseneta wanastahili kuvaa wakiwa katika Bunge hili. Seneta mwanaume anafaa kuvaa koti, shati, tai, suruali ndefu, soksi na viatu, nguo za huduma ama nguo za kidini. Nimemuona ndugu yangu Sen. Chimera pale amevaa vazi ambalo sidhani lina ruhusiwa katika Bunge hili. Kwa hivyo, ningependa utoe mwongozo kuhusu vazi ambalo Sen. Chimera amevaa katika Bunge hili. Asante, Bw. Spika.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, hakuna koti la mikono mifupi.
view
2 Mar 2023 in Senate:
Koti ni la mikono mirefu ambalo linatoka kutoka kwenye bega mpaka kwenye viganja. Hatuwezi kusema kwamba lile ni koti. Hata kama ingekuwa ni suti ya Kaunda, iwe ya mikono mirefu. Suti ya Kaunda ambayo Sen. Onyonka anavaa ni ya mikono mirefu na inaziba sehemu hizi mpaka kwenye vitanga.
view