12 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Spika, sijajichanganya. Nimesema kuwa upande wa walio wengi wachache. Kikatiba, upande huu wetu ndio wa wengi, lakini kwa sababu---
view
12 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Spika, kwanza ningependa kupata muongozo kama Bunge hili limetoa uamuzi kuhusiana na swala hilo. Nimekaa katika vikao vyote vya Bunge hili kutoka vianze na sijasikia Spika akitoa uamuzi kuhusiana na swala hili.
view
12 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Spika, hili si swala la mjadala, kama Spika alitoa uamuzi, unaweza uleta uamuzi huo kesho ili tusome.
view
12 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Spika, kama hawangependa kuita walio wengi wachache, ningependa kuondoa swala hilo. Nimekubali kuondoa swala hilo.
view
12 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Spika, wazo alilotoa Sen. Mungatana kwamba Bunge hili lipate fursa ya kujadili mambo kulingana na maslahi ya wananchi na Kenya kwa jumla, wangeenza wao kwa kuhakikisha kwamba uchaguzi wa wenyekiti wa Kamati zote ambazo ziko katika Bunge hili umegawanywa sawa.
view
12 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Spika, kuna taa tatu pale ambazo zinatuongoza kuhusiana na mambo ya saa. Sijaona hata moja likiwashwa. Ningependa uniruhusu nimalize maelezo yangu. Sen. Mungatana ameleta swala nyeti kwamba Bunge hili lisimame na haki na usawa. Hii itaanza wakati upande wa walio wengi watakubali kuwa nguvu zetu ziko sawa kwa hivyo kamati zigawanywe kisawa. Kamati saba kwao na nane kwetu ile sote tuweze kufanya kazi pamoja. Bunge la Seneti halitafanya kazi kulingana na maslahi ya mtu mwingine. Bunge liloondoka Maseneta wa upande wa walio wengi walikuja hapa wakapiga kura na Kamati zote wakachukua. Tunaomba mwanzo mpya katika Bunge hili---
view
12 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Spika, tulikuwa na Sen. Kinyua kwenye chuo kikuu mwaka mmoja. Kwa hiyvo, hana cha kunifahamisha. Nikimalizia, swala hili la Kamati ni muhimu sana. Ningeomba Kiongozi wa walio wengi, Sen. Cheruiyot na Kiongozi wa walio wachache, Sen. Madzayo waketi chini ili waamue zile Kamati ambazo zitaongozwa baina ya pande zote mbili. Mambo ya nusu mkate itaangaliwa baadaye katika chama cha UDA.
view
12 Oct 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. I have a Communication on substantiation of facts that a Senator arranges to be true.
view