Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 901 to 910 of 2123.

  • 12 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu Spika, hili si swala la mjadala, kama Spika alitoa uamuzi, unaweza uleta uamuzi huo kesho ili tusome. view
  • 12 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu Spika, kama hawangependa kuita walio wengi wachache, ningependa kuondoa swala hilo. Nimekubali kuondoa swala hilo. view
  • 12 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu Spika, wazo alilotoa Sen. Mungatana kwamba Bunge hili lipate fursa ya kujadili mambo kulingana na maslahi ya wananchi na Kenya kwa jumla, wangeenza wao kwa kuhakikisha kwamba uchaguzi wa wenyekiti wa Kamati zote ambazo ziko katika Bunge hili umegawanywa sawa. view
  • 12 Oct 2022 in Senate: Yes, go ahead. view
  • 12 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu Spika, kuna taa tatu pale ambazo zinatuongoza kuhusiana na mambo ya saa. Sijaona hata moja likiwashwa. Ningependa uniruhusu nimalize maelezo yangu. Sen. Mungatana ameleta swala nyeti kwamba Bunge hili lisimame na haki na usawa. Hii itaanza wakati upande wa walio wengi watakubali kuwa nguvu zetu ziko sawa kwa hivyo kamati zigawanywe kisawa. Kamati saba kwao na nane kwetu ile sote tuweze kufanya kazi pamoja. Bunge la Seneti halitafanya kazi kulingana na maslahi ya mtu mwingine. Bunge liloondoka Maseneta wa upande wa walio wengi walikuja hapa wakapiga kura na Kamati zote wakachukua. Tunaomba mwanzo mpya katika Bunge hili--- view
  • 12 Oct 2022 in Senate: La, Bw. Naibu Spika. view
  • 12 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu Spika, tulikuwa na Sen. Kinyua kwenye chuo kikuu mwaka mmoja. Kwa hiyvo, hana cha kunifahamisha. Nikimalizia, swala hili la Kamati ni muhimu sana. Ningeomba Kiongozi wa walio wengi, Sen. Cheruiyot na Kiongozi wa walio wachache, Sen. Madzayo waketi chini ili waamue zile Kamati ambazo zitaongozwa baina ya pande zote mbili. Mambo ya nusu mkate itaangaliwa baadaye katika chama cha UDA. view
  • 12 Oct 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. I have a Communication on substantiation of facts that a Senator arranges to be true. view
  • 11 Oct 2022 in Senate: Hoja ya nidhamu, Bw. Naibu Wa Spika! view
  • 11 Oct 2022 in Senate: Bw. Naibu wa Spika, singependa kumhujumu ndugu yangu, Sen. (Dr.) Murango ambaye anazungumza Kiswahili kwa ufasaha. Hata hivyo, ninasikitika kwamba anasoma mchango wake. Ameangalia hivi chini anasoma wala hata haangalii iwapo Naibu wa Spika kama anasikiliza au hasililizi. Hivyo si sawa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus