22 Mar 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 Mar 2022 in Senate:
maeneo yao. Vilevile, miradi wanayoifanya inaanza kukamilika na hivyo kuhitaji pesa nyingi kuweza kutekelezwa kila mwaka. Kwa hivyo, ongezeko la pesa italeta afueni sana kwa kaunti zetu kwa sababu pesa hizo zitasaidia pakubwa katika kurahisisha huduma. Kuna mambo matano ningependa kugusia katika swala hili. La kwanza, kuna pesa za Managed Equipment Services (MES). Hapo nyuma, Kamati yetu ya Seneti iliyochunguza mradi huu ilipata kulikuwa na utepetevu mwingi katika kupeleka hivi vifaa kwenye kaunti zetu. Mpaka sasa, kuna kaunti zingine ambazo hazijaweza kutumia vifaa vile. Uchunguzi nilioufanya ni kwamba ongezeko la Kshs7 bilioni utasaidia kufunga pengo lililoko sababu kandarasi nyingi zinakamilika ...
view
22 Mar 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 Mar 2022 in Senate:
Kaunti zingine bado zinasubiri Serikali kuu ilete fedha ilhali tumeona kwamba Serikali kuu pia imebanwa katika matumizi yake. Utapata kwamba mara nyingi inachelewa kupeleka pesa kwenye kaunti na hivyo kuna kuwa na misukosuko. Wafanyi kazi hawajui watapata mishahara yao lini na huduma zinadorora katika kaunti zetu. Njia ya kutatua swala hili ni kaunti zidhibiti njia zao za kuokota kodi katika maeneo yao. Sehemu nyingi zinakusanya kodi kizamani. Utapata afisa wa kaunti anazunguka barabarani na kitabu cha risiti akikusanya fedha za kaunti. Hii imepitwa na wakati kwa sababu haijulikana kama wanarudisha pesa hizi kisawasawa. Wengine wanachapisha vitabu vyao wanapozunguka kukusanya kodi. ...
view
22 Mar 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 Mar 2022 in Senate:
Mheshimiwa Spika, tunaona migomo kila mara. Kwa mfano, Kaunti ya Mombasa imekuwa na migomo mara kwa mara ya madaktari kwa sababu ya kucheleweshwa kulipwa kwa mshahara na malumbukizi ya madeni pamoja na zile mikato ya kisheria kama National Hospital Insurance Fund (NHIF), National Social Security Fund (NSSF) na mengineo. Hata kodi ya income tax inacheleweshwa kulipwa katika Kenya Revenue Authority (KRA) na inasababisha wananchi wengi kupata shida ya kuweza kupata mikopo au kuweza kulipwa mikipo yao ambayo wamechukuwa katika bengi na taasisi nyingine za kibinafsi. Ipo haja ya kuweza kuangalia tena hii mfumo wa ugatuzi kuhusiana na vile ambavyo tutaweza ...
view
22 Mar 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 Mar 2022 in Senate:
ugawaji ya rasilmali kwa kaunti zetu inamaanisha kwamba Serikali inaitakia kaunti hii zina ugatuzi kwa jumla heri kubwa. Asante kwa kunipa fursa hii.
view
2 Mar 2022 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia mjadala wa Hoja ya Nidhamu ilioletwa mbele yetu na wakili mkuu, Sen. Omogeni.
view
2 Mar 2022 in Senate:
Bunge ni taasisi huru. Tunachukua mamlaka yetu kutoka kwa Katiba. Hatuna jukumu la kuripoti kwa taasisi nyingine yeyote katika Jamhuri ya Kenya. Inasikitisha kwamba wabunge wanazuiliwa na maafisa wadogo katika idara ya Uhamiaji wakati wanaposafiri nje kuenda shughuli za Bunge.
view