Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 171 to 180 of 356.

  • 20 Sep 2023 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika. Nitarudia jina langu, Murango. Kazi ya mlango ni kufunga ama kufungua. Nimekuja hapa kupinga Taarifa ambayo imeletwa hapa kuhusu, Sen. Orwoba. Hii ni kwa sababu, kuna njia tofauti za kujieleza. Kuna wale ambao wanajieleza vizuri kama Sen. Sifuna. Kuna wale ambao wanakaa katikati kama sehemu nyeti; hawataki kusema upande ambao walipo. Hata hivyo, mimi niko hapa kupinga Taarifa hii kwa sababu tumeona mambo ambayo imefanyika katika hili Bunge hapo awali wewe mwenyewe ukiwa Naibu Spika. Tunakumbuka kuna mambo ilifanyika pale na Seneta wa Migori, kisha ukatoa kauli ambayo tulikuja tukakaa chini na tukaipindua. Hii imefanyika ... view
  • 20 Sep 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 20 Sep 2023 in Senate: kutoka nje. Alikuwa pia anafaa kuitwa katika kamati ya Powers and Privileges . Kwa nini hakuitwa? Lakini huyu kwa sababu ni mama, amepewa adhabu ambayo haifai. Katika maneno ambayo wanasema, na sitayataja hapa, huwa hakuna ushahidi wa mambo ambayo imeongelewa baina ya mwanaume na mwanamke. Sio siri kama imefanyika ama haijafanyika. Sisemi kwamba imefanyika. Hata hivyo, tunastahili tuketi chini kisha tumwangalie huyu kama mwenzetu na tumpe adhabu inayofaa, sio kumfukuza kwa miezi sita ambayo hata kanyaga katika hivi vikao, tukijua ya kwamba anakazi ya kufanya kama mama katika hili Bunge la Seneti. view
  • 20 Sep 2023 in Senate: Bw. Naibu Spika, mimi ninangoja kwa sababu ninajua kuna mtu atakaidi lile agizo lako tena hapa ndio nione kama yeye pia atafanyiwa kama Sen. Orwoba. Katika historia ya hii nchi, tunajaribu sana kuangalia na kupunguza ubaguzi wa wanawake. Hii ndio maana kunasheria maalum ambayo ililetwa, kwamba lazima kuwe na theluthi mbili katika kila kikao ili tuweze kuwapatia wanawake nguvu. Sasa hivi tumeketi hapa wengi tukiwa wanaume kujaribu kufukuza mwanamke. Mimi ninapinga kwa dhati kama Sen. Murango hilo --- view
  • 20 Sep 2023 in Senate: Bw. Naibu Spika, Kanuni za Kudumu 122 (a) inasema kwamba kosa moja kubwa sana ambalo unaweza kufanya, nikukosa kutoka nje ukiambiwa na Spika utoke kwa sababu umekosa nidhamu. Ninajua ya kwamba kila kitu tunayosema hapa kuna rekodi maalum. Ninajua hiyo rekodi maalum iko kwa sababu ninachoongea ninajua ni ukweli mtupu. Wakati jambo kama lile lilifanyika, mwenye alikuwa amefanya makosa alikuja akaitwa, kukawa na kikao alafu akarudi baada ya siku moja ama mbili. Tunayeongelea hapa kwa mambo aliyosema, anafukuzwa kwa kipindi cha miezi sita. Bw. Naibu Spika, hata kama kuna makosa imefanywa na mtu yeyote, kipindi cha miezi sita ni nusu ... view
  • 20 Sep 2023 in Senate: On a point of information, Mr. Speaker, Sir. view
  • 29 Aug 2023 in Senate: Asante sana, Mstahiki Spika, kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia. Kwanza naunga mkono Hoja hii ambayo iliwasilishwa na Kiongozi wa Walio Wengi ya kwamba wale walioteuliwa waweze kuketi na kutafuta jawamu katika mazungumzo. Hata hivyo, tusiwe watu wa kutafuta vita ndipo tuanze kutafuta amani. view
  • 29 Aug 2023 in Senate: Hili ni jambo ambalo lingemalizwa kitambo. Ningeuliza watu waliomba kuwe na mazungumzo, wanapokwenda kuongea tusije kusikia kuwa kuna matata mengi yanatokea sehemu ile kwa sababu Waswahili husema mfungwa hachagui gereza. Kwa sababu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 29 Aug 2023 in Senate: washachaguwa kwamba wanataka kuwa katika gereza la mazungumzo, kusiwe na utata wowote pale wanapozungumza. Kama alivyosema Seneta wa Meru, iwe ni jambo la mwisho kwa sababu hakuna maana ya uchaguzi ikiwa hakuna mshindi. Vile vile, ni kama tukae sote tuteuliwe tuje hapa Seneti. Tukiendelea hivyo, hata mimi pia niliowashinda kule Kirinyaga watasema kuwe na mazungumzo. Wale walioshindwa ugavana watasema pia kuwe na mazungumzo. Kwa hivyo, iwe ni mara ya mwisho kwamba tunafanya hili. Tukilifanya tumalize, kuwe na amani. Pia wanaongoza wasije kwa misingi na misimamo mikali. Waje na misimamo na kauli zitakazotolewa kwa ajili ya wananchi wa Kenya wala sio ... view
  • 2 Aug 2023 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir. Apologies for coming late, I was in another meeting with the Cabinet Secretary for Roads, Transport and Public works, which was just decided yesterday. I am content with the reply by the Cabinet Secretary for Environment, Climate Change and Forestry regarding the Njukini Water Project. I also wish to comment that the reason why we ask these Questions in the Senate is because we only have one stop shop to get answers. With that, I am well advised on what is going on. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus