26 Sep 2023 in National Assembly:
Bw. Naibu wa Spika, ni ya kitambo sana.
view
26 Sep 2023 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, Mathayo 20:16- “Yesu akamaliza kwa kusema, “hivyo, walio wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.” Siri ni kufika ukiwa umechelewa ili uweze kuongea mapema.
view
26 Sep 2023 in National Assembly:
Nitachangia kwa ufupi. Mswada tunaojadili, mambo ni matatu; tuupitishe vile ulivyo, tufanye marakebisho kisha tupitishe ama tupige kura ya kuukataa. Kwa mfano, nyumba ambayo panya ameingia, hawaweza ichoma, kama vile Sen. Osotsi alisema kuwa amekataa huu Mswada. La pili, unaweza tafuta mtaalamu wa panya, kama Sen. Mbugua, akusaidie kutafuta panya; hii ni kupiga msasa na kufanyia Mswada marekebisho. Hatimaye unaweza lala na panya kwa nyumba kwani haiumi, kisha kukicha unafanya mpango tofauti. Kukosa kupitisha Mswada huu hakutaondoa sheria ambazo zimepitishwa na
view
26 Sep 2023 in National Assembly:
kule mashinani ambazo wanatumia uratibu kama wa Seneti. Tunafaa tu- ringfence pesa inayotolewa na wagonjwa kwenye hospitali itumike kwenye hospitali zile. Inapowekwa kwenye mfuko moja kama sadaka, pesa zile kurudishwa kwenye hospitali ni vigumu sana. Pia, zinapowekwa kwenye bajeti ya kaunti, pesa hizo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
26 Sep 2023 in National Assembly:
zitatengwa kujenga barabara na kutengeneza miundo msingi. Zile fedha wakati mwingi hazirudi kwenye bajeti ya hospitali. Mswada hauko kamili, lakini kuna nafasi ya kuufanyia marakebisho. Kwa sasa, tuvumilie tu, tuupitishe ili tutengeneze njia ya kuhakikisha kuwa zile pesa zinazoletwa na wagonjwa zinatumika kwenye hospitali. Kuna hospitali kubwa na ndogo. Wakati matabibu sawa inakosa kwenye hospitali, gatuzi zinatabia ya kuhamia kwenye hospitali zilizosawa kwenye gatuzi zingine. Unapata mkusanyiko wa watu kwenye hospitali. Kuna kaunti tayari zinatumia mfumo huu. Huu si Mswada wa kwanza, na kukosa kuupitisha Mswada huu haimaanishi zile hospitali zitakosa kuendelea. Kwa sababu ya Muda, nitamalizia mchango wangu hapo.
view
21 Sep 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika. Nawapa pole walio wekewa yale madawa yanayoitwa “mchele”. Kama Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga kunakokuzwa mchele, ninawahakikishia kuwa hatuongei kuhusu hii mchele kama mchele ya kawaida kwa sababu huenda ikatuharibia biashara. Inafaa kuitwa kwa jina inayofaa; kwamba ni madawa mabovu ambayo yanayowekewa katika vilabu vingi hapa nchini na watu walio na nia mbaya. Kwanza pole sana kwao. Pili ningetaka kuunga mkono Hoja hii iliyoletwa hapa na Seneta wa Kaunti ya Nandi, Sen. Cherarkey. Jambo linalonishangaza ni kuwa shirika la ndege la Kenya Airways lina tikiti ghali kuliko ndege zingine. Ndege sio matatu, haziwezi fupisha njia zinazotumia. Hakuna ...
view
20 Sep 2023 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Ningetaka kuunga mkono ombi lililoletwa na shemeji yangu Sen. Mwaruma, Seneta wa Taita Taveta. Shida ambayo walimu wako nayo ni kwamba walimu wanaofunza katika maeneo magumu hawapewi pesa ambazo wanastahili kupewa. Hili ni swala nyeti. Sehemu ninayotoka huko Kirinyaga hii imekuwa shida kubwa mpaka hata watoto kutoka sehemu ya Mwea ambao wanafaa kuenda shule---
view
20 Sep 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, ningeomba Seneta wa Vihiga awe anahudhuria hivi vikao ili ajue mambo inavyoendelea kwa sababu hilo jambo lilitatuliwa kitambo sana. Sen. Osotsi ameingilia mtiririko wa mawazo yangu. Nikieleza hapa ameshaharibu. Nilikuwa ninasema ya kwamba katika Kirinyaga---
view
20 Sep 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, tukiendelea hivi itabidi wengine tutoe nguo ili tudhihirishe shida zenye tuko nazo.
view
20 Sep 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, siwezi kutoa nguo kwa sababu nimeambiwa na Sen. Sifuna nitoe. Hii ni kwa sababu yeye ni mwanaume kama mimi. Shida ambazo tuko nazo katika eneo ya Kirinyaga zinaambatana na ombi ambalo limeletwa katika Bunge hili na Sen. Mwaruma. Ukienda huko Kirinyaga na Embu unapata kwamba walimu ambao wako kwenye mazingira ambayo inafanana, wengine wanapewa pesa za ziada kwa sababu ya kuishi kwenye mazingira magumu na wengine hawapewi. Watoto wa chekechea kutoka Kaunti ya Kirinyaga huvuka mpaka kwenda Kaunti ya Embu ambako kuna lishe shuleni. Ilhali mazingira kwenye Kaunti ya Embu ni sawa na Kaunti ya Kirinyaga. Maswala ...
view