11 Oct 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwa maswali ya ziada, nitauliza maswali mawili tu. Waziri, mnamo Mwezi wa Februari mwaka huu, kuna ndugu wawili ambao waliuawawa kinyama pale na ukaleta taarifa katika hili Bunge. Kutoka wakati huo hatujasikia kulifanyika vipi. Kwa hivyo, swali langu ni, je, wale ndugu wa damu waliouliwa, uchunguzi umefika wapi kwa sababu hatujasikia kutoka Februari kuhusu mambo ambayo yanafanyika? Swali la mwisho, kwa sababu sitaki kukuuliza kuhusu mambo ya wizi wa ng’ombe ambao unaendelea Kirinyaga; kuna jambo lilifanyika kule Kirinyaga kuhusu kiongozi mwanamke wa Bunge la Kaunti ya Kirinyaga. Mwanamke huyo alishambuliwa na watu wanaojulikana na wengine ...
view
11 Oct 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
11 Oct 2023 in Senate:
polisi wa manispa. Hata hivyo, kutoka siku hiyo, wale watu bado wanazurura kule na wanawakejeli viongozi kule. Katika uchunguzi wa yale maneno kwa sababu ni mambo ya aibu, umefika wapi na tunatarajia lini kwamba hatua itachukuliwa dhidi ya wale watu? Asante, Bw. Spika wa Muda.
view
11 Oct 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Ni kwa sababu sisi watu wa mashambani tulikuwa tunapitia mambo magumu sana hapo awali. Ukienda kwa daktari, hauitwi jina lako bali unaitwa kulingana na ugonjwa wako. Kuna magonjwa mengine ambayo hayafai kutajwa. Mswada huu---
view
11 Oct 2023 in Senate:
Wewe wacha mambo yako.
view
11 Oct 2023 in Senate:
Bw. Spika, nilinde kutokana na watu wenye--- Mswada huu utasaida sana kuhifadhi data za wagonjwa. Jambo la pili, kuna kaunti ambazo hazina wauguzi na wataalamu wa kutosha. Utapata kwamba kaunti zenyewe ni kubwa pia. Hapo kuna uwezekano wa kuwa na daktari mtaalamu mmoja katika eneo moja. Mgonjwa anapohudumiwa katika zahanati ambazo ziko katika wadi, yule mtaalam mmoja anaweza husishwa. Ikiwa mtu amevunjika mguu, atapigwa picha ambayo itatumwa kutafsiriwa, kisha ripoti kurudishwa na mgonjwa apate matibabu. Itapunguza msongamano katika hospitali zetu. Sasa hivi, ripoti zetu za afya huandikwa kwa karatasi na daftari.
view
11 Oct 2023 in Senate:
Katika enzi hizi, ukienda kwa daktari unaandikiwa madawa na ugonjwa wako kwa karatasi ambayo huenda utembee na ikatapakaa kila mahali. Ninadhani umefika wakati ambapo data ya mgonjwa inapaswa kuhifadhiwa kwa njia inayofaa. Sio lazima kila mtu ajue unagonjeka wapi, hususan wakati huu ambapo kuna magonjwa mengi ambayo yanaleta unyanyapaa. Unaenda kutafuta kazi, stakabadhi zako zilionekana huko ilhali unaugua ugonjwa kama wa mnyama, kisha unaelezwa hayo yote. Mwishowe, unabaguliwa.
view
11 Oct 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
11 Oct 2023 in Senate:
Nikimalizia, hata nchi ambazo zimeendelea zaidi zinatumia teknolojia ya kisasa. Wagonjwa wanatibiwa na daktari aliye mbali kabisa kwa sababu yule daktari ambaye yuko karibu, anapewa muongozo. Kwa hivyo, itapunguza gharama ya kusafiri hadi nchi za mbali kama India. Daktari atakuhudumia hata ukiwa tu hapa nchini. Ninaunga mkono. Sidhani kamwe kutakuwa na shida wakati Mswada huu utapita. Ninasema hivi kwa sababu hata Serikali ya kitaifa iko na vitambulisho vyetu. Hayo haimaanishi kwamba hatuwezi kutumia vitambulisho vyetu na stakabadhi katika kaunti zetu. Ni vizuri kuunga Mswada huu mkono ili tupige hatua katika nyanja za matibabu.
view
5 Oct 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Nimeangalia hili jarida na nikaona ya kwamba Kirinyaga iko na Kshs100---
view