9 Jul 2024 in Senate:
Bw. Mstahiki Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa hii nafasi. Kwanza, nashukuru Kiongozi wa Walio Wengi na Kiongozi wa Walio Wachache Katika Seneti kwa kuketi pamoja na kuona ni vizuri tuwe na kikao kujadili yaliyotupata na yaliyowapata watoto wetu. Pili, ningependa kutuma risala za rambirambi kwa waliofariki katika mapambano ya kutafuta haki. Pia, nina watakia nafuu ya haraka waliojeruhiwa na walio katika hospitali tunapozungumza sasa hivi. Jambo lililotupata kutoka kwa wale Gen Z waliojitokeza ni kwa sababu ya mambo ambayo yamekuwa yakiendelea. Ukiniruhusu, nitaanza kwa kujibu kwa sababu kuna matamshi yaliyotolewa na Sen. Methu na yakarudiwa pia na Seneta ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Uchumi Samawati, jambo tulilolianza kama Kamati bila kulazimishwa ni kuhakikisha ukweli unajulikana. Seneti ina utaratibu na anayejali kusoma anajua kuna utaribu fulani. Siku ya leo ilikuwa iwe siku ya mwisho tuliyokuwa tumewaalika Waziri na washika dau wote waliohusika na haya mambo ya mbolea ili tumalize na tulete taarifa ya mwisho ya mambo yaliyotendeka. Niseme ya kwamba, tunapofanya uchunguzi, sio jambo linalochukua siku moja au mbili. Tumemaliza uchunguzi hata kabla taasisi ya usalama ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kumaliza. Kwa hivyo, hata kama sisi hatujapelekwa mafunzo, sisi tumemaliza na tarehe 21 ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
waliambiwa ni vijana na kesho. Kesho ikapita na kukaja kesho kutwa. Kesho kutwa ikapita na kukawa na mtondo na mtondogoo, kitondo na hata ikafika kitojo. Wameona siku yao haifiki na malalamishi yao hayasikizwi. Juzi, nilikuwa kwa mkutano uliokuwa na kijana mmoja aliye mhandisi wa programu za tarakilishi. Tulikutana naye mahali alipokuwa anafanya kazi ya uchukuzi na upakiaji wa mizigo katika shirika la uchukuzi la G4S. Yeye ni mhandisi. Amejaribu kutafuta kazi bila kufanikiwa. Tunapoangazia ufisadi, inafaa tuangazie hadi kwa gatuzi zetu. Ukienda kwa gatuzi yangu ya Kirinyaga, utapata kuna mgao wa asilimia 30 unaofaa kwenda kwa akina mama, vijana na ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
Hivyo basi, naomba, pia katika gatuzi zetu ambapo pesa zinaenda kwa wingi sana, lazima tuhakikishe sheria ya ununuzi wa bidhaa inazingatiwa. Haiwezekani ya kwamba ukizunguka katika gatuzi nyingi hakuna kijana hata mmoja amefaidika. Ni wale mabwenyenye wachache wanaoandikisha wasichana wao na Gen Z wanakosa kazi. Kwa upande wa ukulima, maji ni tatizo. Kwa hivyo, hata tunapojaribu kuwapa njia mbadala na kuwaambia watafute kazi, tunasahau ya kwamba vifaa na mtaji wa kufanya kazi haupo. Ukienda kwa benki zetu, riba ni kuanzia asilimia 18 hadi 20. Wakati tunatangaza nyadhifa za kazi na kuwaambia wale vijana wawe na uzoefu wa miaka mitano, je, ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
. Ukienda kwa Kaunti ya Kirinyaga, utapata wale walioomba mikopo kutoka kwa benki wakiwepo wanarika na kufanya kazi walizopewa, pesa zao zilizama na hata wa leo hawajawahi kuzipata. Ili wapate zile pesa, lazima watoe mlungula. Kazi ngumu ya msaraghambo na ya kutafuta fedha na kufanya kazi inakuwa haina faida. Imefikia mahali pa wale vijana kutoka nje kutukumbusha ya kwamba kuna shida katika nchi hii na lazima tuiangalie. Tukienda kwa idara ya michezo iliyogatuliwa na kuangalia pale kwetu Kirinyaga, pia najawa na huzuni. Vijana wamefanywa watu wa kucheza kandanda vijijini na malipo ni viatu na sare tu za kucheza mpira. Hakuna ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
vijana hujitokeza wengi sana. Sijawahi kuelewa sababu ya vijana The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
9 Jul 2024 in Senate:
watokelezee 1,000 halafu tunawachukua watano tu. Lazima tutafute njia mbadala ambayo hata kama ni ya kiteknologia ili wale ambao wanatafuta zile ajira watakuwa wanafanya zile application pale kabla ya kufika uwanjani, ili tuweze pia kumaliza kabisa ufisadi unaoendelea na pia ubaguzi wakati wa kupeana kazi. Kwa hivyo, mimi kama Mwenyeketi wa Kamati ya Ukulima, Uvuvi na Uchumi Samawati, yaliyosemwa nimeyasikia na nimeahidi ya kwamba sisi tumefanya msaragambo au kazi ngumu na tumemaliza. Tarehe 21 tumewaita wale washikadau wote kuhakisha kwamba tumemaliza ile taarifa ya upelelezi ya mbolea gushi. Tutakuja kuiwasilisha hapa na tumefuata Katiba na sheria zote za Seneti ambazo ...
view
11 Jun 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika. Ningetaka kujiunga na wenzangu kuunga mkono Mswada ulio mbele yetu siku ya leo. Ninafurahi kusema kwamba, nikiangalia pesa ambazo zinaenda kwenye Kaunti ya Kirinyaga, ambako mimi ni Seneta, iko na nyongeza kubwa sana katika mwaka huu. Ninaona ya kwamba katika mgao wa kawaida wako na zaidi ya Shilingi bilioni tano na katika conditional grants wako na Shilingi 36 milioni. Tukiangalia mwaka uliopita ambapo walipata Shilingi 5.4 bilioni, saa hii ninaona watapata Shilingi 6.8 bilioni. Katika nyongeza ya pesa ya mwaka huu, ningetaka kuona hospitali ambazo kwa muda hazijamilizwa kujengwa, zikijengwa. Ningependa kuona zahananti za Kiandieri, Kiaritha Nguka, ...
view
11 Jun 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika. Ningetaka kujiunga na wenzangu kuunga mkono Mswada ulio mbele yetu siku ya leo. Ninafurahi kusema kwamba, nikiangalia pesa ambazo zinaenda kwenye Kaunti ya Kirinyaga, ambako mimi ni Seneta, iko na nyongeza kubwa sana katika mwaka huu. Ninaona ya kwamba katika mgao wa kawaida wako na zaidi ya Shilingi bilioni tano na katika conditional grants wako na Shilingi 36 milioni. Tukiangalia mwaka uliopita ambapo walipata Shilingi 5.4 bilioni, saa hii ninaona watapata Shilingi 6.8 bilioni. Katika nyongeza ya pesa ya mwaka huu, ningetaka kuona hospitali ambazo kwa muda hazijamilizwa kujengwa, zikijengwa. Ningependa kuona zahananti za Kiandieri, Kiaritha Nguka, ...
view
11 Jun 2024 in Senate:
zilijengwa na county kwa mbao zikiwekwa chuma ili watoto wetu wawe na usalama wakati wanapovuka, kuenda na kurudi kutoka shuleni. Ningependa kuona madawa katika hospitali zetu. Ningependa ninapo uliza swali nijibiwe kama Seneta kwa sababu saa hii tuko pamoja wakati tunapotafuta pesa lakini wakati tunapopeleka pesa mashinani huwa tunachukuliwa kama tingatinga ambazo zinajenga barabara; ujenzi ukikamilika zinabebwa ili zisiharibu barabara hizo. Ningependa wanakandarasi wale ambao walifanya kazi katika Kaunti ya Kirinyaga na hawajalipwa, waweze kulipwa pesa zao. Pia, ningependa kuona pesa za bursary ambazo zinapewa wanafunzi wetu zimeongezeka ili waweze kwenda shule. Bw. Spika, kazi kubwa ya Seneta ni hii ...
view