Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 211 to 220 of 424.

  • 11 Oct 2023 in Senate: polisi wa manispa. Hata hivyo, kutoka siku hiyo, wale watu bado wanazurura kule na wanawakejeli viongozi kule. Katika uchunguzi wa yale maneno kwa sababu ni mambo ya aibu, umefika wapi na tunatarajia lini kwamba hatua itachukuliwa dhidi ya wale watu? Asante, Bw. Spika wa Muda. view
  • 11 Oct 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Ni kwa sababu sisi watu wa mashambani tulikuwa tunapitia mambo magumu sana hapo awali. Ukienda kwa daktari, hauitwi jina lako bali unaitwa kulingana na ugonjwa wako. Kuna magonjwa mengine ambayo hayafai kutajwa. Mswada huu--- view
  • 11 Oct 2023 in Senate: Wewe wacha mambo yako. view
  • 11 Oct 2023 in Senate: Bw. Spika, nilinde kutokana na watu wenye--- Mswada huu utasaida sana kuhifadhi data za wagonjwa. Jambo la pili, kuna kaunti ambazo hazina wauguzi na wataalamu wa kutosha. Utapata kwamba kaunti zenyewe ni kubwa pia. Hapo kuna uwezekano wa kuwa na daktari mtaalamu mmoja katika eneo moja. Mgonjwa anapohudumiwa katika zahanati ambazo ziko katika wadi, yule mtaalam mmoja anaweza husishwa. Ikiwa mtu amevunjika mguu, atapigwa picha ambayo itatumwa kutafsiriwa, kisha ripoti kurudishwa na mgonjwa apate matibabu. Itapunguza msongamano katika hospitali zetu. Sasa hivi, ripoti zetu za afya huandikwa kwa karatasi na daftari. view
  • 11 Oct 2023 in Senate: Katika enzi hizi, ukienda kwa daktari unaandikiwa madawa na ugonjwa wako kwa karatasi ambayo huenda utembee na ikatapakaa kila mahali. Ninadhani umefika wakati ambapo data ya mgonjwa inapaswa kuhifadhiwa kwa njia inayofaa. Sio lazima kila mtu ajue unagonjeka wapi, hususan wakati huu ambapo kuna magonjwa mengi ambayo yanaleta unyanyapaa. Unaenda kutafuta kazi, stakabadhi zako zilionekana huko ilhali unaugua ugonjwa kama wa mnyama, kisha unaelezwa hayo yote. Mwishowe, unabaguliwa. view
  • 11 Oct 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 11 Oct 2023 in Senate: Nikimalizia, hata nchi ambazo zimeendelea zaidi zinatumia teknolojia ya kisasa. Wagonjwa wanatibiwa na daktari aliye mbali kabisa kwa sababu yule daktari ambaye yuko karibu, anapewa muongozo. Kwa hivyo, itapunguza gharama ya kusafiri hadi nchi za mbali kama India. Daktari atakuhudumia hata ukiwa tu hapa nchini. Ninaunga mkono. Sidhani kamwe kutakuwa na shida wakati Mswada huu utapita. Ninasema hivi kwa sababu hata Serikali ya kitaifa iko na vitambulisho vyetu. Hayo haimaanishi kwamba hatuwezi kutumia vitambulisho vyetu na stakabadhi katika kaunti zetu. Ni vizuri kuunga Mswada huu mkono ili tupige hatua katika nyanja za matibabu. view
  • 5 Oct 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. Nimeangalia hili jarida na nikaona ya kwamba Kirinyaga iko na Kshs100--- view
  • 5 Oct 2023 in Senate: Ni Kshs100, sio bilioni. view
  • 5 Oct 2023 in Senate: Bw. Spika, kuna wale wanaratibu mgao unaopewa makaunti kwa sababu ya madini au zile bidhaa zinazotokana na mahali pale. Tungependa kujua kama ni hii Kshs100 iliyopewa Kirinyaga na imetokana na madini gani? Kwa sababu, hili jarida niko nalo ni ghali kuliko Kshs100. Haina haja ya kuratibu Kshs100 za kupea Kaunti nzima. Ninaamini kuna hesabu inapaswa kuangaliwa kama iko sawa. Kama mkaazi wa Kirinyaga, ninajua eneo lililo chini ya Mwea ni muhimu kwa uchimbaji wa kokoto na marigafu mengi ya kutengeneza barabara. Kwa hivyo, kupata Kshs100 imeleta mshtuko kidogo. Bw. Spika, ninaunga mkono mambo kama haya yanaletwa katika Bunge la Seneti. ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus