29 Jun 2023 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise pursuant to Standing Order No.53(1) to seek a Statement from the Standing Committee on Labour and Social Welfare regarding the management of talent in the counties. In the Statement, the Committee should- (1) Outline plans in place by the national and county governments, if any, to provide infrastructural support and economic incentives for upcoming and established artists in Kirinyaga County. (2) State whether there are plans by the County Government of Kirinyaga to establish a recording studio, arts academy or any other income generating projects for artists in Financial Year 2023/2024. (3) Update the Senate ...
view
29 Jun 2023 in Senate:
Asante sana, Bi Spika wa Muda. Nimesimama hapa siku ya leo kuunga mkono Hoja hii ambao umeletwa na Sen. Kavindu Muthama kwa sababu janga lilotukumba mwaka 1998 ni janga ambalo kila Mkenya anasikia uchungu. Mnamo tarehe 7 Agosti, 1998, Mohammed Rashed alifikishwa kortini kule Marekani na akashtakiwa kwa kuwaumiza watu 12. Hao watu 12 walikuwa wananchi wa America ambao walikuwa wameumia. Hawakutaja kwamba Wakenya 224 walikuwa pia wameumia. Waliohukumiwa baaadaye ndio walikuja sasa kubadilisha ile nambari ya watu waliokuwa wameumia. Mnamo tarehe 5 Agosti 2020, America ilisema kwamba kuna pesa ya ridhaa ambayo ilikuwa inafaa kulipwa watu walioumia ambayo ilikuwa ...
view
29 Jun 2023 in Senate:
Naona Sen. Kavindu Muthama ananiashiria nikomee hapo. Ningependa kukueleza kwamba Spika wa Muda yupo na anajua kuwa lazima tumalize leo. Bi. Spika wa Muda, kwa vile Sen. Kavindu Muthama ananiashiria nimalize, nitamalizia hapo.
view
27 Jun 2023 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise, pursuant to Standing Order No. 53(1), to seek a Statement from the Standing Committee on Labour and Social Welfare regarding the unprocedural reduction of the salaries of Early Childhood Development Education (ECDE) teachers in Kirinyaga County. In the Statement, the Committee should: (1) explain the circumstances that led to the suspension, in the months of March and April, 2023, of salaries of ECDE teachers in Kirinyaga County and the eventual manual payment of a fraction of the same in May 2023; (2) conduct a comprehensive assessment of the impact of this unprocedural salary review on ...
view
26 Jun 2023 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Nasimama bila aibu kupinga Ripoti iliyowasilishwa na Kamati inayopendekeza kutimuliwa kwa Naibu wa Gavana, Dkt. Oduol. Nimeskia Seneta wa Nairobi, Sen. Sifuna, akitaja majina ya watu ambao hawakuunga mkono Ripoti hii. Ningependa kuwaambia waliotajwa kuwa ukisikia shetani anapiga makofi wakati unaokoka, kuna shida kubwa hapo.
view
26 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, Kipengee cha 158 cha sheria kuhusu usimamizi wa fedha kinasema wazi kwamba afisa mhasibu mkuu katika kaunti ni gavana. Inasemekana kwamba Dkt. Oduol alinunua kiti. Hilo ni jambo ambalo Gavana wa Siaya anafaa kuulizwa wala sio naibu wake. Tusijifanye wanafiki hapa. Ningependa kumwuliza Kiongozi wa Wachache asimame ikiwa anajua bei ya kiti alichokalia. Ikiwa anajua, tutajua kuwa Naibu wa Gavana wa Kaunti ya Siaya ana makosa. Ikiwa hajui, ni makosa kumwekelea mwenzake kosa ilhali yeye hausiki katika ununuzi wa bidhaa katika Kaunti ya Siaya.
view
26 Jun 2023 in Senate:
Ningependa Sen. Sifuna atulie ili asikilize busara.
view
26 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
26 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, nilikuwa mwakilishi wa wadi na Kiongozi wa Wengi katika Kaunti ya Kirinyaga kutoka mwaka 2017 hadi 2022. Manaibu wa magavana wananyanyaswa sana na magavana. Hawawezi hata kusema chochote pahali popote. Ukiuliza Maseneta ikiwa wanajua manaibu wa magavana kama watano, hawawezi kuwataja. Mimi kama Seneta wa Kirinyaga, sitaki kuwa mmoja wa wale wanaotumika katika huu mradi wa Mrengo wa Azimio la Umoja wa kumwondoa mamlakani Naibu Gavana wa Siaya.
view
26 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, kwa heshima kubwa, naondoa maneno ambayo nilisema hapo awali.
view