21 Jun 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ushiriki wa Umma tuliofanya kuhusu ukulima katika Seneti, tulianza na Mswada ulioletwa na Sen. Wambua. Tulienda Kitui na Sen. Beth Syengo. Niliona mapenzi mengi kutoka kwa watu wa Kitui. Sen. Wambua ameleta Mswada kuhusu ndengu na Sen. Beth Syengo ameleta Mswada kuhusu pamba. Zote zinakuzwa sehemu tofauti. Tulienda mahali panaitwa Ngomeni, ambapo ni nyumbani kwa Sen. Beth Syengo. Huo wakati kulikuwa na ukame kabisa. Sababu ilioyonifanya niamue kwamba mimi nitakufa na huu Mswada kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ukulima ni kwamba, hata kulikuwa na shida na njaa nyingi pale, wale wakulima ...
view
21 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
21 Jun 2023 in Senate:
pale zikililia usaidizi na kunasuliwa kutoka kwa mitego wamewekewa wakiritimba, wanaoitwa cartels, walioingilia ukulima wa ndengu. Nyumba nyingi sana katika Kenya hii zinakula ndengu. Ukiangalia magonjwa mengi tunao, utapiamlo unaotusumbua kwa watoto wachanga katika sehemu zile ni kame. Ni jambo rahisi kutatuliwa na kununua mimea kama ndengu na kupatia wale watoto. Mswada huu wa Sen. Wambua umekuja wakati mzuri sana. Tuko na Mswada ambao tunafaa kueneza huduma za ukulima na maafisa wa ukulima. Pia tutaangalia
view
21 Jun 2023 in Senate:
and vitu zingine kama hizo. Leo, nimeona barua mahali ambayo inafaa kununua vitu kama hizi. Bw. Spika wa Muda, ningeomba wakati tunaangalia, tuweze pia kuweka ndengu, ziwe ni mimea ambayo inawezasaidika na Commodities Fund . Hii ni kwa sababu ilivyo kwa sasa, mimea iliyoko katika sheria ya Crop Act ndiyo inaweza kupewa fedha. Ukipika ndengu, kiasi ya 200 grams, hua unapata kiwango cha protini cha 14.2
view
21 Jun 2023 in Senate:
na fiber 15.4. Magonjwa mengi ya tumbo yanatokana na kukosa fiber katika mwili, sana soluble fiber . Ndengu iko na soluble fiber inaitwa pectin ambayo inazuia sana saratani ya utumbo. Kwa hivyo, ni chakula kizuri kwa miili yetu. Mama mja mzito akikula 202 grams ya ndengu, anapata asilimia 80 ya foliate. Kwa hivyo, wakati wanapojifungua, watoto wao wanakuwa wazima, werevu na wajanja kama, Sen. Murango, na mambo yanakua shwari. Kuna magnesium na vitu vingine vingi.
view
21 Jun 2023 in Senate:
inasaidia wale watu wanasumbuliwa na high blood pressure . Wale watu wanaotaka kupunguza kilo kidogo, ndengu ni mzuri sababu kuna kitu kinaitwa butylate katika ndengu. Tutakaa chini ya miti ili tuongee maneno kama haya. Lakini, cha msingi ni kwamba ndengu ni zao muhimu sana katika mwili wa binadamu. Wale wanajeshi wetu, kabla waende kupigana na Al Shabaab pande ile, wanafaa wapewe mkebe ya ndengu ili waende nayo itawasaidia. Watoto wetu shuleni wanaohangaika na utapiamlo na wale wana afya nzuri, ili kuhakikisha afya zao zinaendelea kuwa nzuri, wanafaa chakula chao kisikose ndengu, sababu tutakuwa tunazikuza hapa. Shule, idara za Serikali na ...
view
21 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
21 Jun 2023 in Senate:
Ni vizuri kuwe na usawa. Tuunge mkono Mswada huu ulioletwa na Sen. Wambua na tuupitishe. Pia tuingize katika uratibu na taratibu za Crops Act na Commodity Fund ili wananchi wanaolima ndengu peke yake, waweze kufaidika na hili zao. Tusisahau pia ule Mswada wa pamba ulioletwa na Sen. Beth Syengo. Bw. Spika wa Muda, Kamati yangu iliamua haitakaa chini iletewe makaratasi na memoranda zilizoandikwa. Tumezunguka mpaka siku ya Jumapili. Kuna jambo Sen. Wambua alileta ambalo tunafaa tuskize jinsi ambavyo tunafanya ushiriki wa umma. Ilibidi arudi mfukoni ili kuunga mkono ajenda iliyo muhimu sana katika Mswada huu wa ndengu. Kwa hivyo, ni ...
view
21 Jun 2023 in Senate:
Nawahakikishia Sen. Wambua, Sen. Beth Syengo, Sen. Maanzo na Sen. Mundigi Munyi na wale Maseneta waliotoka zile kaunti 35 zinazokuza ndegu ya kwamba tuko pamoja, kuanzia saa hii mpaka mwisho. Waswahili walisema, mgala muue na haki yake umpe.
view