Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 321 to 330 of 356.

  • 9 Mar 2023 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir. I rise, pursuant to Standing Order No. 53(1) to seek a Statement from the Standing Committee on National Security, Defence and Foreign Relations on the status of investigations into the death of Mr. Kennedy Njoroge and Mr. Ndung’u Njoroge in Mwea Subcounty. In the Statement, the Committee should - (1) Inform the Senate of the circumstances leading to the deaths of the two brothers; Mr. Kennedy Njoroge and Mr. Ndung’u Njoroge, that occurred in Mwea Sub- County on 14th February, 2023. (2) Appraise the senate of the state of investigations into the deaths of the ... view
  • 8 Mar 2023 in Senate: Asante sana, Mstahiki Spika. Ninampa kongole Mwenye Ardhilhali aliyeomba kuhusu malipo ya uzeeni na nyongezo ya mishahara ya walimu. Ni kitu kinafaa kuzingatiwa kwa maana kwa muda mrefu mambo yanayokumba waalimu mengi hayajakuwa ya kutia moyo sana. Ya kwanza, kuna uhawilisho ambao umekuwa ukiendelea; kupelekwa eneo tofauti na bado wanalipwa mishahara ile ile. Kwa hivyo, ni vizuri hiyo nyongeza izingatiwe na ada ya walimu pia iangaliwe. Nilikuwa nimeomba Ardhilhali ambayo ilienda kwa Kamati ya Leba na Maslahi ya Jamii kuhusu malipo ya wale madiwani waliokuwepo. Ni vizuri pia ile izingatiwe kwa sababu tunapokaa sana bila kuwalipa halafu tunalipa wakati miaka ... view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kama mwenyekiti wa Kiswahili kitukuzwe katika Afrika Mashariki na Jangwa la Sahara, ni vizuri nifanyie Kiswahili haki kwa kuwakaribisha wanafuzi wa kutoka shule ya St. Anne Gituba. St. Anne Gituba ni shule moja ya maana sana kutoka Kaunti ya Kirinyaga. Kama mimi niko hapa, pia wao wanaweza kufika hapa. Nimesikia kuwa hapa kuna viongozi wa wanafuzi kutoka chuo kikuu cha Makueni. Mimi sikufanikiwa kuwa kiongozi katika chuo kikuu lakini nilikuwa kiranja katika darasa la saba. Kwa hivyo, nadhani hata huo ni uongozi. Bw. Naibu Spika, nafasi ambayo wanafunzi wako nayo sasa hivi ni muhimu sana. ... view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika. Kwanza, ninamshukuru Kiongozi wa Wengi na Kiongozi wa Wachache. Hii ni kwa sababu ninaelewa ya kwamba uchache ya Walio Wachache sio wingi wetu tulio Wengi. Kwa hivyo, ninadhani ni jambo la busara amefanya. Sijui iwapo leo ilikuwa siku yangu katika diary ya shetani. Hii ni kwa sababu, yale mambo yaliyokuwa yanafanyika hapa ndani na hata nje, nimekuwa na matatizo mara mbili. Kwanza, nilikuwa na shule tatu ambazo zimezuru hapa leo. Sijui kwa nini mambo fulani yamefanyika wakati walipokuwa hapa. Iwapo wameenda wakifikiria hivyo ndivyo tunavyofanya hapa, niko na shida kubwa sana. view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Wakati ulipofika ukanipa nafasi ya kuzungumza, katika kile kizaazaa, nilikaribisha shule ya Kaunti ya Murang’a kama ya Kirinyaga. Kwa hivyo, hao wanafikiria hata sijui majina ya shule ambazo zimekuwa hapa leo. view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Bw. Naibu Spika, kuna kitabu kinachoitwa Hekaya za Abunwasi. Kinasema eti mtego wa panya huingia waliyomo na wasiokuwemo. Pengine leo mtego haukuwa wangu lakini hata kama mimi ni ng’ombe, nimeshikwa katika huo mtego. Ninasema hivi kwa sababu aibu ni kubwa upande wangu kama Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga. view
  • 22 Feb 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Hata hivyo, kuna mambo ambayo tunajifunza. Iwapo umeangalia, lile kopo la maji ambalo hukuwa pale halipo. Maseneta wamekunywa maji sana hapa kwa sababu kulikuwa kumechemka. view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Chupa za maji ambayo nimekunywa ndizo hizi hapa. Hizi ni nusu tu ya chupa zote za maji niliyokunywa nilipokuwa hapa. Kule nje pia, nimefanya vivyo hivyo. Sasa ninaomba tuweze kwenda mbele kama Bunge ili tutekeleze majukumu yaliyo mbele yetu. Hilo ndilo litatufanya sisi tuonekane kama Maseneta. Kwa bahati mbaya, wote walikuwa wameenda katika Bunge la Kitaifa kisha wakaishia hapa. Sen. Methu na Sen. Joe Nyutu walikuwa wamemalizana na wao. Hata hivyo, kwa sababu diary ya shetani ilikuwepo, ikawa sasa ni zamu ya wale niliokuwa nao. Kuna wengine ambao walikuwa nje na wameenda nyumbani wakiwa wamekasirika sana. Kwa hivyo, twende pamoja. ... view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Mr. Speaker, Sir, thank you for giving me this opportunity. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus