20 Dec 2022 in Senate:
upon the Committee to be honest in their findings and make sure the voice of the people will be that of the Senators. Thank you, Mr. Speaker, Sir.
view
24 Nov 2022 in Senate:
Asante. Bw. Spika. Waswahili husema Mgala muue na haki mpe. Swala la vitambulisho limekuwa nyeti sana kwa vijana. Mimi ni Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga na kumekuwa na hali ngumu amabapo kijana hana wwazazi. Anapoendea kitambulisho anaambiwa alete cha nyanyake au cha nyanya ya nyanyake. Bw. Spika, ukiambiwa uje na hicho kitambulisho cha nyanyake nyanyako hutakipata. Ni vizuri kama Serikali tunapofanya hesabu za kutoa vitambulisho tusije tukakandamiza wale tunaotetea hapa. Ukienda mahali popote kuajiliwa ata kazi ya mlinda lango unahitajika kuwa na kitambulisho. Ukienda kutafuta pesa ya mahuluku- taabu yani “hustlers” ni lazima uwe na kitambuliso. Ili haki ifikie wale ...
view
24 Nov 2022 in Senate:
mahali zile vitu zinapaswa kuletwa vile tunavyofanya tunapo kusanya kodi. Ukitaka kujua Serikali inajua kwako, kosa kulipa kodi. Watakukujia hadi kwako. Tungependa pia hata katika kupeana vitambulisho, Serikali---
view
16 Nov 2022 in Senate:
Mr. Speaker Sir, I seek your permission to go through the various Statements that I have consecutively.
view
10 Nov 2022 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Taarifa ambayo imetolewa na Sen. Crystal Asige. Ninaunga mkono kauli iliyotolewa na Kiongozi wa Walio Wengi katika Seneti kwa sababu sheria nyingi zinatungwa na zile zinafaa kutungwa ndipo ziweze kutumika. Wahandisi wengi wanaopitisha ile michoro inayotumika katika ujenzi wa mijengo mingi katika kaunti, hawatilii maanani kwamba wanafaa kuzingatia sheria ili wale watu ambao wanaoishi na ulemavu wa wanaweza kuingia katika mijengo hiyo. Ninasema hivyo kwa sababu ukienda leo kuna michoro ya nyumba ambayo ilipitishwa na wahandisi lakini watu wanaoishi na ulemavu hawawezi kuingia ndani. Tunapoendelea kutunga sheria ambazo hazitiliwi maanani, hakuna ...
view
11 Oct 2022 in Senate:
Asante Bw. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi hii ili nizungumze kidigo kuhusu hotuba ya Rais Katika Bunge la 13. Kwa Kiswahili, kuna wahusika wakuu na wale wa kupachikwa. Nilipoangalia nakala ya hotuba ya Rais, niliona inawiana kabisa na manifesto ya Kenya Kwanza tuliyokuwa nayo. Kwa hivyo, sisi ni wahusika wakuu. Ninampa kongole Rais kwa hotuba na kauli zake Kwanza, nitaanza na kilimo. Ninatoka katika Kaunti ya Kirinyaga ambako tunalima mpunga. Huu ndio mradi mkubwa zaidi humu nchini na hata kote barani Afrika. Hapa nchini pia tuko na miradi mingine kama vile Bura, Tana, Perkerra, Bunyala na West Kano. Iwapo ...
view
11 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Wa Spika, ninaomba ulinzi kutoka kwa rafiki yangu, Sen. Faki, ambaye ameanza kuonyesha dalili za kigaidi.
view
11 Oct 2022 in Senate:
Mimi sisomi chochote lakini niko na nakala ya hotuba ya Rais, ambayo ninafuatilia kwa makini. Bw. Naibu wa Spika kuna mambo kadhaa ambayo nilikuwa nimeyaongelea na nilianza na Kilimo. Nilikuwa nimesema nimetoka Kaunti ya Kirinyaga, ambako kilimo ndilo jambo ambalo wakulima wanafanya kila siku. Huko kunakuzwa kahawa, mchele, majani chai na pia ukulima wa samaki na vitu vinginezo. Asubuhi ya leo nimepita soko la Makutano na sanduku moja la nyanya ambalo ni kilo 60, ni Kshs1,500. Kama tungefanya
view
11 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu wa Spika, ninadhani mimi ni mrefu kidogo sasa nikisimama wima, sijui kama nitafikia kipaza sauti, lakini nitaendelea tu. Hata hivyo, ninazungumza kwa Kiswahili lakini Hotuba ya Rais iko kwa Kiingereza. Kwa hivyo, hakuna uwezekano wa mimi kusoma wakati ninatoa taarifa yangu. Bw. Naibu wa Spika, ninaomba ulinzi ili nimalize kwa sababu niko karibu kusahau ambayo nikuwa ninataka kusema Rais wetu alisema ili tuweze kupata chakula cha kutosha, lazima tufanye kilimo na kupeana mbolea ya ruzuku kwa wakulima. Ninamshukuru Rais kwa sababu tayari ashaanza kufanya hivyo na hiyo mbolea ishafikia wakulima. Hili ni jambo muhimu katika kuongeza chakula inchini. ...
view
11 Oct 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view